Chui azua taharuki Wilayani Hai, ajeruhi watu kadhaa

kiwatengu

Platinum Member
Apr 6, 2012
17,647
14,794
Leo Asubuhi kuna Chui ameleta fujo na kujeruhi watu kadhaa.

Askari wa wanyama pori wafanikiwa kumuua.

Majeruhi wanne waliojeruhiwa na Chui huyo ni pamoja na
1.Emmanuel Urassa(37) ambaye amejeruhiwa maeneo ya usoni na mkononi,

2.Jesca Nkoo(21) amejeruhiwa usoni na mgongoni,

3. Urusula Cosmas (26) amejeruhiwa kichwani na puani na

4. Maliki Sakia (31) aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni.

Wanapatiwa matibabu hospitali ya Wilaya ya Hai.

IMG-20210929-WA0006.jpg

IMG-20210929-WA0007.jpg
 
Kwanini isiliwe, toa ufafanuzi
Jamiii na Utamaduni wa Makabila ya Watanzania wengi hawali nyama ya Wanyama wote walao Nyama. Ikiwemo Simba, Chui, Fisi, Mbweha, Mbwa, Mbwa Mwitu, Paka nk
Bado tuna akiba ya kutosha kwa wanyama walao Mimea na ndio tunakula kwa sasa hao walao nyama tumewaweka Sub/Kiporo kwanza. Ingawa kwa wenzetu kama China, Burundi, DRC wameshaingia kwenye Sub
 
Huyu chui ni special case anatakiwa aliwe ili kutoa funzo kwa wanyama wengine walao nyama kwambaj jamii ya Hangaya ukituzingua tunazinguana
 
Pole
Leo Asubuhi kuna Chui ameleta fujo na kujeruhi watu kadhaa.

Askari wa wanyama pori wafanikiwa kumuua.

Majeruhi wanne waliojeruhiwa na Chui huyo ni pamoja na
1.Emmanuel Urassa(37) ambaye amejeruhiwa maeneo ya usoni na mkononi,

2.Jesca Nkoo(21) amejeruhiwa usoni na mgongoni,

3. Urusula Cosmas (26) amejeruhiwa kichwani na puani na

4. Maliki Sakia (31) aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni.

Wanapatiwa matibabu hospitali ya Wilaya ya Hai.

View attachment 1957264

View attachment 1957265
Pole chui. Hakukuwa na sindano za tranquilizer mpaka mumuue ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom