Chui alivyouawa nje ya nyumba ya Mkurugenzi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Lutengano alisema majira ya saa saba usiku wa juzi alimsikia mbwa wake akibweka kwa nguvu huku akielekea kupambana na adui.

Alisema aliposhituka kutoka usingizini na kuchungulia nje aliona mbwa huyo akipambana na chui.

"Niliona kumbe ni chui, ingawa nilikuwa ndani, alisema Lutengano na kwamba "ndipo nilipowapigia simu watu wa Idara ya Wanyamapori."

Askari wa wanyamapori walifika nyumbani muda mfupi baadaye na kumuua chui huyo, alisema, kwa sababu nao walikuwa eneo la karibu wakifuatilia taarifa za wananchi kuwa kuna chui wanne waliokuwa wakizagaa eneo hilo.

"(Askari wanyamapori) walikuwa mitaa ya kwa Mkuu wa Wilaya wakiwindana nae kufuatia baadhi ya watu kusema wanawaona chui kama wanne hivi katika milima yetu ya Magu," alisema Lutengano.

Alisema muda mfupi tangu achungulie dirishani na kupiga simu ya kuomba msaada alisikia mlio wa bunduki karibu na geti la nyumba yake.
"Kumbe wale wa Idara ya Wanyamapori walikuwa tayari wameshafika katika eneo la tukio na kufanya kazi yao ipasavyo."

Alisema anadhani chui huyo na wenzake watatu ambao hata hivyo hakuna ushahidi kuwa walikuwa wanne, watakuwa waliingia katika makazi ya binadamu kutafuta maji ya kunywa.

Alisema watumishi wa Idara ya Wanyamapori baada ya kumuua chui huyo waliendelea na msako wa chui wengine bila mafanikio.
Ramadhani Maandakia, mtu aliyempiga risasi chui huyo alisema haikuwa kazi rahisi, hata hivyo.

Alisema yeye si mfanyakazi wa serikali bali hukodiwa na Idara ya Wanyamapori kwa ajili ya kwenda kuua wanyama wakali wanaohatarisha usalama wa watu.
"Unapopambana na chui ni mnyama hatari sana kwani pale unapomjeruhi ni lazima akufuate ili mpambane nae," alisema Maandakia.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Magu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya, Khadija Nyembo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la nyumbani kwa mkurugenzi wake.

Nyembo aliwatahadharisha wananchi kutotembea usiku wa manane kwani taarifa zinasema kuwa bado wanyama hao wanaonekana milimani na kushambulia nguruwe wa watu.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka watumishi wa Idara ya Wanyamapori kuwasaka popote wanaposikika uwapo wa chui hao ili kunusuru maisha ya watu wa Magu.

"Chui ni mnyama wa hatari sana hivyo ni lazima wauawe," alisema Nyembo.

Chanzo: Nipashe
 

Ramadhan James

JF-Expert Member
Dec 14, 2015
2,188
2,000
"Unapopambana na chui ni mnyama hatari sana kwani pale unapomjeruhi ni lazima akufuate ili mpambane nae," alisema Maandakia.


Hiyo ndio sifa kuu ya Mnyama ninaempenda Chui! hata mie niko hivyo ukinizingua , sisubiri nilianzisha mpaka kieleweke!
 

Yamakagashi

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
8,648
2,000
Hivi kwanini wao (askari pori ) huwa wanapiga risasi tu hawana vile vidubwana vya kuwapiga wakapata usingizi wa ghafla na kuwarudisha porini huko?

Ila hali ngumu kweli kwa sasa mpaka chui anaingia mjini kusaka chakula kazi tunayo
Hata mimi najiuliza sana.. Kwanini wawaue kama hawaja onja nyama ya binadamu yenye chumvi?
 

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
6,168
2,000
Ikitokea umekutana chui ghafla usimuangalie machoni wala kumtukana. Na simba simama wima na umuangalie machoni
 

Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,999
2,000
Hivi kwanini wao (askari pori ) huwa wanapiga risasi tu hawana vile vidubwana vya kuwapiga wakapata usingizi wa ghafla na kuwarudisha porini huko?

Ila hali ngumu kweli kwa sasa mpaka chui anaingia mjini kusaka chakula kazi tunayo
EH!!! Mkuu wawarudishe wanini, ili waje tena baadaye kusumbua watu? Wawaue tu.
 

Mkomavu

JF-Expert Member
Jan 25, 2016
10,514
2,000
Tatizo la mkoa wetu wa Mwanza, unaweza kumuona ni mnyama wa porini kama chui au fisi, kumbe "ni wanadamu wanafanya mambo ya kiutamaduni" yaani ni shida mtuhurumie tunaoishi huku mikoa ya watu.
Nakumbuka 2005 nilienda huko NYANGUGE loooh hatari sana
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,670
2,000
Ohoooo!!!Kuna mbinu niliipata hapa jana kwenye post moja kwamba unaweza tumia hata shati unalivua unamfunika usoni wakati anahangaika wewe unakula kunjo.
Shati utakua unapoteza bure kamuda kako, kwanza unaanzaje kumfuata na kumfunika uasoni? huwa tunamtupia mfuko wa salfet na kumuacha ahangaike nayo hadi achoke na kulala usingizi. Huwa anakua hana ujanja mbele ya mfuko wa salfeti
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom