Christopher Olonyoke Olesendeka Jiuzulu ubunge mwenyewe kabla hatujakufukuza.............


F

FRANK MICHAEL

Senior Member
Joined
May 17, 2011
Messages
150
Likes
0
Points
33
Age
32
F

FRANK MICHAEL

Senior Member
Joined May 17, 2011
150 0 33
Kazi kubwa ya mbunge ni kuwaakilisha wananchi wake katika Bunge la jamuhuri ya muungano, mhimili mkuu wa demokrasia nchini ambalo kazi yake kuu ni kutunga sheria, kuisimamia serikali ikiwa ni pamoja na kuratibu mahusiano kati ya wananchi na serikali yao waliyoiweka madarakani kwa kuhakikisha kuwa serikali hiyo inatekeleza matakwa yao.

na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 iko wazi kwa jambo hili katika sehemu yake ya utangulizi kwamba misingi ya uhuru, haki, udugu, amani, tuliyojiwekea, yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye Demokrasia, ambayo serikali yake husimamiwa na bunge lenyewe, wajumbe waliochaguliwa wanawakilishwa (siyo serikali, bali) wananchi.''

kwa mantiki hii wananchi huchaguwa wale wachache bora (aristoi) wanaodhani wanaweza kuwakilisha vema katika kuisimamia Serikali (ya wananchi) waliyoiweka madarakani.
tena kwa mantiki hii"demokrasia" ni serikali ya watu ( wananchi) iliyowekwa madarakani na watu kwa ajili yam watu.
kwa tafsiri hii iliyo sahihi mbunge wa Simanjiro Mh Christopher OLesendeka, amepoteza uhalali wa kuitwa mbunge wa Simanjiro.

Tulivyokuwa kwenye Ziara ya katibu mkuu wa Chadema wilayani Simanjiro, tumejionea mambo mengi ya kushangaza na kuhuzunisha, tumezoea kuona watu wa kilalamikia kero za maji, migogoro ya ardhi, huduma duni za afya, elimu isiyo na viwango vya kuridhisha, ugumu wa maisha, na mambo mengine ya kawaida, lakini ya simanjiro yanashtua kidogo, watu azima wanachapwa viboko na wenyeviti wa vijiji vyao wakijaribu kuhoji masuala yanayohusu maslahi ya watawala hao wa Vijiji, hiyo kama haitoshi watu wanatishiwa kuhamishwa kama wakijarib kupingana na mawazo ya viongozi wa vijiji vyao, mimi nimezaliwa Simanjiro nikakulia Simanjiro nikasoma elimu yangu ya Msingi Simanjiro, lakini Ziara hii ya Katibu mkuu wa Chadema Mh Dr Willbord Slaa imenionyesha sura ya nyingine ya Simanjiro ambayo sikuwa naifahamu huko nyuma.

Naweza kusema Simanjiro haina Mbunge na wala siyo sehemu ya Tanzania.........
simanjiro ni Wilaya ya kwanza kuwa na Barabara mbovu.........
pamoja na na hali hii hatujaahi kumuonana mbunge wetu akilipigia kelele au akitokwa na mapovu mdomoni kama kama tulivyo mzoeya yanavyomtoka akiisifia CCM...........

Naweza kusema Simanjiro ni Sehemu inayongoza Tanzania kwa kuwa na watu wenye maisha duni pamoja na kuwa mungu ametujalia rasilimali nyingi hali wanasimanjiro bado ni mbaya na sijawahi kumuona Mbunge wangu akitokwa na mapovu mdomoni kuoji Tanzanite imebadilishaje maisha ya wanasimanjiro..........

Mh mbunge wangu sikuwahi kusikia ukipaza sauti yako hiyo kama ulivyokuwa ukiipaza juzi kijenge ukimnadi mgombea udiwani wa Kimandolu wa CCM kulalamikia uwonevu wanaofanyiwa wapigakura wako wa Simanjiro na wenyeviti wa Vijiji amoja na kwamba taarifa unazo.........

Mimi kama mmoja wa watu unawowangoza mpiga kura na mwananchi wa Wilaya ya Simanjiro, kwa kuzingatia haki yangu ya kikatiba ibara ya 18 (a) na (c) ninakutaka ujiuzulu mara moja kwa kushindwa kutambua majukumu yako ya kiungozi vyinginevyo tutaitisha mkutano wa Jimbo ya kukupigia kura ya kutokuwa na Imani na wewe!
 
A

ambagae

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2009
Messages
1,653
Likes
4
Points
135
A

ambagae

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2009
1,653 4 135
He, makubwa
 
mbuguni

mbuguni

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2013
Messages
563
Likes
33
Points
45
mbuguni

mbuguni

JF-Expert Member
Joined May 15, 2013
563 33 45
Nikweli kabisa manake mm mwenyewe nipo karibu na simanjiro, ambayo ni mererani, shambarai, nasinyai, watu wana hali mbaya huko sana.
 
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Messages
11,821
Likes
767
Points
280
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined May 1, 2012
11,821 767 280
mkuu mbuguni wakati mnapewa tshirt na khanga hamkujitambua?
 
Last edited by a moderator:
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Messages
11,821
Likes
767
Points
280
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined May 1, 2012
11,821 767 280
mkuu mbuguni wakati mnapewa tshirt na khanga hamkujitambua?
 
Last edited by a moderator:
O

Olemandalo

Senior Member
Joined
Dec 7, 2012
Messages
117
Likes
1
Points
0
O

Olemandalo

Senior Member
Joined Dec 7, 2012
117 1 0
wakati mwingine muwe mnajaribu kutumia vichwa kufikiria mnavyo post upuuzi wenu humu hivi mnafikiri Mbunge ni mtu wa kuwapa watu hela za kula, kujengea ama kwa ajili yaq mavazi? ni heri mngetumia huo mda mnaopost ujinga humu kuwashika wake zenu
alafu nani kakudanganya unaweza kumfukuza mbunge? wewe nani wakumfukuza mbunge?
naona mnaanza kuwa matahira mwambie huyo Millya wenu aka anajua Sheria KAa anavyoigamba kuwa yeye kasoma sheria awafundishe sheria huwezi mfukuza mbunge kienyeji kama unavyo mfukuza mke wako.........
shame of you Oleleshwa eti unajiita kijana msomi........
 
O

Olemandalo

Senior Member
Joined
Dec 7, 2012
Messages
117
Likes
1
Points
0
O

Olemandalo

Senior Member
Joined Dec 7, 2012
117 1 0
wewe unahali zuri?
wewe mbunge wako ni Nassari wa Chadema huwa anakugawia shilingi ngapi tuambiae!
 
S

Sema Kweli

Member
Joined
Apr 12, 2013
Messages
53
Likes
0
Points
13
Age
49
S

Sema Kweli

Member
Joined Apr 12, 2013
53 0 13
Labda nianze kwa kusema tu kama kuna kujisahau kwa nini umechaguliwa basi mbunge wa simanjiro anaongoza kwa kujisahau.
na kama kuna kukosea kuchagua basi wana simanjiro walikosea sana kumchagua huyu jamaa,Nasema hivyo kwani wote tunajua wakati ule walipokuwa wakijipambanua kuwa wapinga ufisadi na makelele kibao,lakini leo hii huwezi kumsikia tena yu wapi yule mpinga ufisadi?au ndo tuseme kuwa alikuwa mgeni katika fani ndo maana alikuwa na makelele ila sasa na yeye ni mwenyeji kwa hiyo anajichukulia kama ilivyo kuwa kwa wenzie.Kizazi cha panya siku zote ni kizazi cha panya hakuna panya asie iba iwe baba,mama,au watoto siku zote panya ni mwizi na usitarajie panya asiwe mwizi.Nimeamini kuwa ndani ya ccm hakuna alie mtakatifu ila wote ni wezi na wachumi tumbo,ila siku inakuja watanzania watakapo sema ccm kwaheri tumechoka na kuibiwa na sasa tunawatoa kupe nyie msie shiba hata ngombe achinjwe mpo tuuuuuuuuu.:heh:
 
H

H20

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Messages
342
Likes
2
Points
33
H

H20

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2013
342 2 33
Kwa wale mnaomjua Sendeka ni unstable minded. Yaani hasimamii ukweli japo wakati akiongea unaweza kufikiri ni mzalendo wa kweli. Wakati alipokuwa akijinasibu kupambana na ufisadi wengi tulifikiri ni mzalendo, akarudisha majeshi nyuma sasa anatetea mafisadi huko Kimandolu. Ameacha kuhudhuria vikao vya bunge haswa kuchangia bajeti ya elimu kwani ni changamoto sana kwa watu wa jamii yake. By the way yeye pia ni walewale waliopata daraja la sufuri pale Moshi secondary ambayo hata standardization isingemsaidia kama ingefanyika wakati ule wa 80s. Haoni matatizo ya wananchi wake na mara nyingi anaunga hoja mkono kwa 100%. Inabidi wananchi wa SIMANJIRO mbadilike chagueni mtu atakayewawakilisha Bungeni. Amkeni!
 
K

kinauche

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
7,684
Likes
850
Points
280
Age
68
K

kinauche

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
7,684 850 280
Labda nianze kwa kusema tu kama kuna kujisahau kwa nini umechaguliwa basi mbunge wa simanjiro anaongoza kwa kujisahau.na kama kuna kukosea kuchagua basi wana simanjiro walikosea sana kumchagua huyu jamaa,Nasema hivyo kwani wote tunajua wakati ule walipokuwa wakijipambanua kuwa wapinga ufisadi na makelele kibao,lakini leo hii huwezi kumsikia tena yu wapi yule mpinga ufisadi?au ndo tuseme kuwa alikuwa mgeni katika fani ndo maana alikuwa na makelele ila sasa na yeye ni mwenyeji kwa hiyo anajichukulia kama ilivyo kuwa kwa wenzie.Kizazi cha panya siku zote ni kizazi cha panya hakuna panya asie iba iwe baba,mama,au watoto siku zote panya ni mwizi na usitarajie panya asiwe mwizi.Nimeamini kuwa ndani ya ccm hakuna alie mtakatifu ila wote ni wezi na wachumi tumbo,ila siku inakuja watanzania watakapo sema ccm kwaheri tumechoka na kuibiwa na sasa tunawatoa kupe nyie msie shiba hata ngombe achinjwe mpo tuuuuuuuuu.:heh:
Wabunge wengi wamesahau ni kwa nini wako bungeni. Wanaona walikuwa wanatafuta ajira na sasa wamepata. Lakini wakati mwingine wala tusiwalaumu kwa sababu kama wakati anagombea alikupa cho chote ni kwamba huna tena unachomdai. Hii ni kwa sababu anakuwa ubunge wake aliununua and you cannot put him/her to task. Lakini kama hukupokea cho chote kama kofia, khanga fedha nk, bado una haki ya kumwajibisha mbunge wako but not otherwise. Kwa hiyo jiulize, Una haki ya kumhoji Ole Sendeka? Wakati wa kampeni hakutoa cho chote? Kama alifanya na ukapokea basi ujue imekula kwako. Pole.
 

Forum statistics

Threads 1,274,856
Members 490,833
Posts 30,526,099