R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575
Katibu wa CCM mkoa wa Manyara akiendelea na utaratibu jukwaani kabla ya Ole Sendeka kuhutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Bashneti
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wialaya ya Mbulu mkoani Manyara, akimsalimia Msemaji Mkuu wa CCM Christopher Ole Sendeka wakati wa mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kata ya Bashneti. Kulia ni Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng'enda aliyeko katika ziara hiyo ya Msemaji Mkuu wa CCM.
Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng'enda akifungua pazia kwa kutoa hotuba fupi, kabla ya Msemaji Mkuu wa CCM, Chrstopher Ole Sendeka kuhutubia mkutano huo wa hadhara uliofanyika kata ya Bashneti, Babati mkoani Manyara leo
Msemaji mkuu wa ccm, mjumbe wa nec, christopher ole sendeka akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika kata ya bashneti, wilayani babati mkoani manyara leo.
Sendeka, amesema, chama cha mapinduzi kinamuunga mkono na kumtetea kwa nguvu zake zote rais dk. John magufuli katika jitihada zake za kuliinua taifa la tanzania.
Amesema, ccm itafanya hivyo kwa sababu kazi anayofanya ya kupambana na wazembe na wezi wa mapato kwenye vyanzo vya uchumi wa taifa inatokana na maelekezo ya ilani ya ccm.
Sendeka amesema, ccm inawataka wale wote wanaojaribu kupotosha jitihada zinazofanywa na rais za 'kupasua majipu', kuwa ni kuwaone wanaochukuliwa hatia, kuacha mara moja, kwa sababu kinachofanyika ni sahihi na kwa mujibu wa sheria.
Amesema, upasuaji majipu huo unaofanaywa na rais magufuli hauchagui bali yeyote anayebainika kuwa ni jipu hata akiwa mwana ccm haachwi.
Kwa upande wake, mjumbe wa nec, kilumbe ng'enda, amewataka watazania kutambua kuwa uchaguzi umeshamalizika kwa hivyo asitokee yeyote kuanza kuweweseka, kwa kutoa maneno ya kejeli kuhusu utendaji kazi wa rais dk. Magufuli kwa sababu baada ya uchaguzi kumalizika sasa kiichobaki ni kuchapa kazi.
Amsema, hakuna sababu za mwanasiasa yeyote kuanza mambo ya fitina za kisiasa wakati huu kwa kuwa kufanya hivyo anajisumbua.