Je, kanisa la mhubiri Christopher Mwakasege liko wapi?

Jamaa hana shida ya hela alikuwa mshauri wa uchumi wa mkapa enzi za uraisi wake, Pia alishawahi kuwa afisa mipango wa wilaya ya Arumeru na ana NGO yake inayojihusisha na masuala ya kiuchumi!
Na kufundisha neno la Mungu ameanza miaka ya 1980's hadi leo!
Ni mwalimu wa neno la Mungu na ni mwalimu mzuri pia wa masuala ya uchumi!
Kuna kanisa moja kutoka marekani lilishamwambiaga awe askofu wao masuala ya hela hayatamsumbua akakataa akasema hayuko kwa ajili ya hela!

Sa mbona anasemaga watu wamchangie,tena watu wenyewe wauza mahindi ya kuchoma, maandazi ndio wanajitoa kumsaidia.Je hela unazozungumzia wewe ni zipi? hizi zenye namba 500, 1000, 2000, 5000 na 10,000 ama zipi maana zenye hizi namba ndio anapitisha bakuli
 
huwa sio fan wa makanisa ya kiroho, but Mwakasege yuko level nyingine:

hata kama anahubiri kuhusu pesa; ila anakuwa na back up inayoeleweka, he talks sense mara nyingi.

Kitu nisichoelewa huwa ni kutoa mapepo.

Ni Dr (Phd) wa uchumi, anachofanya ni ku simplify matheory ya uchumi ili mtu wa kawaida aelewe, then......anapiga hela !
 
Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
Nasikia ni Mhubiri,
je kanisa lake liko wapi?

Mwakasege ni mwinjiristi, kazi yake kubwa ni kuihubiri injiri kwa mataifa na sio mchungaji yeye pia ana mchungaji wake anaye mchunga kwa hiyo hamiliki kanisa, lakini anaweza kua na kipaji cha uchungaji pia na unabii hata utume ana weza kua nao. na hata karama za kuombea wagonjwa anaweza kua nazo.
 
Mungu amesema Israel ni mtoto wake wa kwanza kasome Kutoka 4:22. Na Mungu kasema atawabariki watakaobariki Israel na kuwalaani watakaoilaani kasome Mwanzo 12:3. Unajua anaposema Isrel anamaanisha taifa la Israel na sisi wengine tunaoamini tunachukua hizo baraka za Israel kupitia Yesu Kristo. Nasi tunafanyika kuwa wana wa Mungu. Ni muhimu kwenda Israel kulibariki hilo taifa teule la Mungu.
Mwalimu Mwakasege yuko juu sana huwezi kumlinganisha na watumishi wengi kwasababu moja kubwa,hafungwi na minyororo ya madhehebu.Nimewahi kuhudhuria semina nyingi za Bwana Mwakasege sikuwahi kumsikia hata siku moja akiwaelekeza watu waende kwenye dhehebu fulani fulani.

Kuna kasoro moja kubwa ambayo nimeiona kwa Bwana Mwakasege siku za karibuni amejikita sana kuwahimiza watu kwenda Israel.Amefikia hatua ya kuandaa safari za kwenda Israel kwa wanandoa as if uponyaji unapatikana unapokwenda Israel.Bwana mwakasege ndiye aliyemshauri E Ngoyai Elowassa kwenda Israel mara baada ya kuitia hasara kubwa nchi yetu na mkataba wa RICHMOND badala ya kumshauri aombe radhi watanzania kwa uzembe anamshauri aende Israel.
 
Sa mbona anasemaga watu wamchangie,tena watu wenyewe wauza mahindi ya kuchoma, maandazi ndio wanajitoa kumsaidia.Je hela unazozungumzia wewe ni zipi? hizi zenye namba 500, 1000, 2000, 5000 na 10,000 ama zipi maana zenye hizi namba ndio anapitisha bakuli

Biblia inasema tutoe sadaka
sasa unataka watu wasitoe sadaka?
Hizo sadaka zinatumika kwenye uendeshaji wa hizo semina maana zinahitaji gharama
kumbuka yeye hana kanisa kwa hiyo kila anapokuwa inabidi atengeneze hema na kukodi viti na vitu vingine vinavyohitaji gharama!
BTW!
Kama unataka kumuelewa vizuri inabidi uwe mtu wa rohoni maana mambo ya kiroho kuyatafsiri ni ngumu kama unataka kuyatafsiri kimwili!
 
wooooote ni walewale binafsi mtu ninayemkubali ni FR. DR TITUS AMIGU MTAALAMU WA BIBLIA KUTOKA PERAMIHO SEMINARY
 
Mwakasege anajiita mwalimu wa biblia,lakini kwa ufupi ni kwamba ni muongo anaezusha aliwahi kudai eti alitaka kuuwawa,mara katakiwa kuwa askofu zote hizi ni uongo.cha mwisho ni kwamba yeye na mke wake wanatumia miujiza ya uongo kama kawaida ya walokole.

thibitisha maneno yako ili tukuamini la sivyo tutakuchukulia wewe kama mzushi mwongo na mfitini.
Mungu na akuhurumie
 
Arusha.

Ni maombi au kitu kingine? Mpeleke mgonjwa wako kwa kakobe au mzee wa hammer pale ubungo chaibora-nyumba ya ufufuo na uzima
Mkuu huyo mzee wa hammer amehamia Kawe viwanja vya Tanganyika Packers.
 
Ndio maana anahubiri kuhusu pesa na back up ya baibo, na mbado he talks sense

Sasa watu hawataki kufundishwa ujasiriamali in connection na dini, wanataka tutoane mapepo tuuu

Sina tatizo na yeye kupiga hela, anawaconvince watu hadi wanatoa wenyewe.

Ni Dr (Phd) wa uchumi, anachofanya ni ku simplify matheory ya uchumi ili mtu wa kawaida aelewe, then......anapiga hela !
 
wadau wanauliza, ni kwa nin anazunguka mikoa ile ile tu? au ndo iliyo na watu wanaoitaj kufafanuliwa biblia tu? Toa hoja melech usizunguke mbuyu,
 
Last edited by a moderator:
Biblia inasema tutoe sadaka
sasa unataka watu wasitoe sadaka?
Hizo sadaka zinatumika kwenye uendeshaji wa hizo semina maana zinahitaji gharama
kumbuka yeye hana kanisa kwa hiyo kila anapokuwa inabidi atengeneze hema na kukodi viti na vitu vingine vinavyohitaji gharama!
BTW!
Kama unataka kumuelewa vizuri inabidi uwe mtu wa rohoni maana mambo ya kiroho kuyatafsiri ni ngumu kama unataka kuyatafsiri kimwili!


............hapo ni chenga ya mwili ! ........kama unapiga ! .....kumbe unatoa pasi !:wave:
 
To the Law and to the Testimony, If they don't speak according to this word, it is because there is no light in them! Isaiah 8:20
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom