Christopher Bageni agonga mwamba Mahakamani, sasa anasubiri Kunyongwa tu

View attachment 1181240

Hii ni baada ya Mahakama kuifutilia mbali kesi yake ya kuomba uamuzi wa Mahakama kuu iliyomhukumu kunyongwa upitiwe upya .

Kwa faida ya wageni wa jf na wengine ni kwamba huyu Bageni ni mmoja wa washirika Abdallah Zombe kwenye Mauaji na uporaji wa mihela ya wafanyabiashara wa madini kutoka Morogoro uliotikisa nchi na kulidhalilisha jeshi la Polisi

======


DAR: RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA KIFO KWA ALIYEKUWA MKUU WA UPELELEZI WA KINONDONI YAGONGA MWAMBA

Matumaini ya kukata rufaa yamefifia baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi hayo yaliyowakilishwa na Wakili wa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni

Bageni aliiomba Mahakama iridhie kumfutiwe adhabu ya kunyongwa kwa kosa la mauaji ya Wafanyabiashara 3 wa madini kutoka Mahenge, Morogoro

Uamuzi huu wa Mahakama, umehitimisha kesi hii iliyodumu kwa miaka 13 tangu washtakiwa walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza mwaka 2006

Tangu wakati huo washtakiwa walikuwa wakipungua katika kila hatua ya kesi, hadi kubakia ndugu Christopher Bageni pekee

Washtakiwa wengine waliowahi kujumuishwa katika kesi hii kabla ya kuachiwa huru ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar(RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Abdallah Zombe, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi, Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi(ASP), Ahmed Makelle, na Askari wa Kituo cha Polisi Oysterbay, Rajabu Bakari
Umemsahau mmoja alikufa wakati akiwa Mahabusu, ana jina la kasikazini!
 
Kanikumbusha wale wauza madini waliouawa kinyama,yule RPC wa mkoa flani anaitwa Zombe alipona vipi?Maana baada ya tukio eti akapata uhamisho kwenda kuwa RPC kama sikosei Rukwa.
Kulikuwa na figisu za hovyo sana ndani ya jeshi la polisi kipindi hicho.

Tena uozo ulianzia pale Insp gen Omari Mahita alipopata madaraka enzi za Mkapa kuja kwenye utawala wa awamu ya4.

Si hao tu, watu wengi sana wameuawa kiuonevu kwa baraka za jeshi la polisi enzi hizo kwa kisingizio cha ujambazi na hakuna kiongozi aliyeshituka.
 
Maisha yana formula...nayo ni mtu unapaswa kuwa mnyenyekevu, mcha Mungu, usiye na majivuno, mpenda haki, unayechukia rushwa na maovu yote, mwenye nidhamu na usiye na chembe ya sifa ya ukatili...
Naomba mfano wa mtu mmoja tu aliyeko hai leo huko sirikaleeni mwenye sifa zako hizo
 
Kanikumbusha wale wauza madini waliouawa kinyama,yule RPC wa mkoa flani anaitwa Zombe alipona vipi?Maana baada ya tukio eti akapata uhamisho kwenda kuwa RPC kama sikosei Rukwa.
Zombe ndie alikuwa master of ceremony kwenye mauaji yale lakini sheria zilipokuja hakuguswa moja kwa moja kumtia hatiani kwa ushenzi walioufanya hivyo akaachiwa huru lakini hata hivyo nasikia akili yake imebaki kuwa ya kijelajela yaani chizi fresh hivi
 
Naomba mfano wa mtu mmoja tu aliyeko hai leo huko sirikaleeni mwenye sifa zako hizo

Tuache hayo watu serikalini...Tuzungumzie jamii kwa ujumla wakiwemo hao wa serikalini bila shaka...Je, wewe mwenzangu ukiwa mwanajamii huna sifa yoyote miongoni mwa hizi nilizozitaja???
 
Hivi unaamini atanyongwa? mimi siamini.
Mpaka rais atie saini ya kukubali anyongwe ndiyo atanyongwa. Ni muda mrefu marais wamekuwa hawatii saini hivyo wafungwa wengi waliohukumiwa kunyongwa wapo tu bila kujua hatima zao. Pamoja na hayo kitendo cha kuhukumiwa kunyongwa halafu akakaa tu gerezani bila kuwa na mategemeo ya kutoka na huku akiwa na wasiwasi pengine rais anaweza kutia saini anyongwe muda wowote ni adhabu mbaya hata kuliko kunyongwa kwenyewe.
 
Tuache hayo watu serikalini...Tuzungumzie jamii kwa ujumla wakiwemo hao wa serikalini bila shaka...Je, wewe mwenzangu ukiwa mwanajamii huna sifa yoyote miongoni mwa hizi nilizozitaja???
Usijitangaze weye mwenyewe acha jamii ikutangaze. Usikwepe swali langu, Nipe mfano wa mtu mmoja tu katika more than50m mwenye hizo sifa zako
 
Back
Top Bottom