Christiano Ronaldo anabebwa mno na vyombo vya habari

7e4.jpg
 
Mbona una maono finyu hivyo. Hujaona madakika yote aliyocheza kuanzaia mechi ya kwanza hadi jana final. Hajakosa ata mechi moja, hajacheza chini ya kiwango, kaivusha ureno kwenye makundi af unakuja unaongea pumba.

Ronaldo ndo mchezaji bora kwa sasa hakuna ubishi juu ya hilo. Uwepo wake tu pale kwenye benchi jana licha ya kucheza dk 24 ni hamasa kwa wachezaji wenzake.
 
ajabu mtoa mada mwenyewe katika post yako umemtaja ronaldo mara nyingi...tena umeshindwa hata kumtaja huyo aliyefunga....hauna tofauti na hivyo vyombo vya habari vinavyomuonyesha ronaldo tu!nami nipo katika same boat...simtaji mfungaji bali namtaja ronaldo tu!!!kifupi...huu mchezo hautaki hasira
 
Ronardo ameibeba saana ureno .tangu mwanzo wa mashindano.Amefanya vizuri saana.huwezi ukamlinganisha na messi ambaye aliikosesha timu yake.na hana historia ya kuibeba timu yake kitaifa.CR7 anasistahili kuwa best player2016
Ureno imepenya kibahati bahati tu. Messi alikosa penalt kama alivyokosa Ronaldo, au umeshasahau kuwa naye alikosa? Bahati ya mtende. Ureno wameokota dodo chini ya mwarubaini
 
Jana tumeshuhudia fainali ya Ulaya kati ya Ureno na Ufaransa ambapo Cristian Ronaldo alicheza kwa dakika takribani 24 na kuumia,hivyo akashindwa kuendelea na mchezo kwa bahati Ureno wakaibuka na ushindi wa goli moja na mpira kumalizika.

Cha ajabu mpira ulivyoisha ikawa tunaonyeshwa Ronaldo muda wote na kila afanyalo zaidi hata kuonyeshwa mfungaji bao pekee wa Ureno ambae angalau angestahili hata kuongelewa na kuonyeshwa zaidi lakini ikawa sasa baada ya mechi ni Ronaldo...Ronaldo tu wakati kacheza chini ya nusu saa na hakufanya kashkashi zozote mpaka anatoka.

Dah jamaa anabebwa aisee itakuwa kama David Beckam sasa looh!
Teh Teh wewe nae umerudia yale unayo yaita makosa ya vyombo vya habari maana umeshondwa hata kumtaja mfungaji....!
 
Maoni yenu yote mpunga, CR7 anabebwa sana na media za waingereza mnazokodolea mimacho kila cku kwa vile hawampendi messi. Muwe na personal judgement.
N:B Infact time will tell.
 
Cr7 keshabeba ndoo hivyo bakini chuki/husda zinazoendelea kuwatafuna.
 
Hata ungepinga mpaka asubuhi hilo kombe litambeba sana. Huu ni mwaka wake
 
Ni kweli anabebwa na media ukicheki hata uefa ilikuwa hivyo hivyo mbeleko from media.
 
Back
Top Bottom