Christiano Ronaldo ahukumiwa Kwenda Jela miaka miwili

Billy the Goat

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
566
353
Striker wa zamani wa Real Madrid ambae Kwa sasa amesign kuichezea Juventus Christiano Ronaldo, amehukumiwa kwenda Jela miaka 2 pamoja na kulipa faini ya Euro Million 19 ambazo ni zaidi ya sh Bilioni 50 za kitanzania.

Hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama ya Uhispania imekuja baada ya CR7 kukubali makosa manne ya ukwepaji Kodi yenye thamani ya Euro Milioni 14.7 Kati ya mwaka 2011 - 2014. Ingawa mwanzoni CR7 pamoja na management company yake ya Gestifute walikana mashitaka hayo.

Kulingana na taarifa za EFE Kodi hiyo ilipunguzwa mpaka Euro Milioni 5.7 baada ya CR7 kukubali kosa, ambapo ukijumlisha punguzo hilo pamoja na faini, riba na gharama nyingine jumla kuu ndo inafikia Euro Milioni 19.

Kulingana na Sheria za Uhispania, Christiano Ronaldo hataingia gerezani kabisa kutokana na kwamba hili ni kosa la Kwanza kwa mchezaji huyo, ila kama Striker huyo atafanya kosa lingine ndani ya kipindi cha miaka miwili basi ataweza kufungwa.

Mashitaka na hukumu ya aina hii karibia yafanane na yake aliyopewa hasimu mkubwa wa CR7, yule mchawi wa Barcelona Lionel Messi. Wachezaji wengine ambao wameangukia kwenye mkono wa Sheria za Mamlaka ya Kodi ya Uhispania ni pamoja na Alexis Sanchez wa Man U, na Captain wa zamani wa Argentina Javier Mascherano.
 
Afuweni kwa wanamichezo na wasanii wa Kiafrika. Huku mpunga unaula wote, kodi ni ya maji, umeme, jengo na intaneti (kama ipo)....
Sasa hapa ndio kale kamantiki ka kodi inauma kanapojulikana. Kadri unavyopata mkwanja mrefu kodi kubwa zaidi na za aina zaidi ya mbili... Muulize Ronaldo
 
Back
Top Bottom