Christ mtikila ni mchungaji wa kanisa gani ama bomu la serikali?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Christ mtikila ni mchungaji wa kanisa gani ama bomu la serikali??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 28, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,185
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  NAJARIBU KUFIKIRIA HIVI VYEO UCHUNGAJI VINATOLEWAJE JAMANI..NIMEJARIBU KUFIKIRIA NA HUYU BWANA ANAEMWAGIKA KILA WAKATI WA UCHAGUZI BAADA YA UCHAGUZI UMSIKII TENA ..MWISHO TUKAAMBIWA ALIKUWA ANAKULA PESA ZA ROSTAM AZIIZ HUYUHUYU ANASEMA DOWANS A WASILIPWE SIJUI NA BADO NAJIULIZA AMETOKA KANISA GANI....LEO AMEKUJA NA HIKI KISA KINGINE  Askofu atupwa gerezani akidaiwa si Mtanzania

  [​IMG]
  ASKOFU wa Kanisa la House Prayer Shield of Faith Christian Fellowship, Fredrick Mukongo, amekamatwa na Idara ya Uhamiaji na kupelekwa gerezani baada ya Mchungaji Christopher Mtikila kudai kuwa ni raia wa Congo.
  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Wakili wa Askofu huyo, Jerome Msemwa, alisema ameshangazwa na hatua ya uhamiaji kumpeleka gerezani Askofu huyo bila kutoa maandishi ya kuthibitisha kwamba si raia wa nchi hii.
  Alisema Mtikila amekuwa akiandika barua za kumtuhumu Askofu huyo kuwa sio raia ya Congo ambapo mwaka 2004 aliandika barua kwa idara hiyo mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi na kuthibitisha kuwa ni Mtanzania.
  Hata hivyo, mwaka jana Mtikila aliendelea kuandika barua katika idara hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo idara hiyo imedai kuwa uchunguzi umeonyesha kwamba askofu huyo si Mtanzania bali ni raia wa Congo.
  “Nasikitika serikali kuingilia malumbano ya kidini na kumsikiliza Mtikila dhidi ya mchunga kondoo mwenzie Mukongo… Januari 20, mwaka huu Kamishna Mkuu ametoa barua ya kumnyang’anya na kumfutia hati ya kusafiria mteja wangu,” alisema Msemwa. Alisemakuwa barua iliyotolewa na Kamishna Cuthbeth Sambalyegula haina maelezo ya kutosha zaidi ya kueleza kuwa uchunguzi umeonyesha askofu huyo sio raia wa Tanzania. “Hata kama Waziri wa Mambo ya Ndani ametoa amri hiyo mbona hakuna maelezo ya uchunguzi wao, nimeshangaa leo tumekwenda kuripoti uhamiaji wamembeba na kumpeleka gerezani,” alihoji Msemwa


  MUNGU AMREHEMU SANA AKASOME ZAB 105
   
Loading...