Chrisant Mzindakaya amuomba Rais Magufuli ruhusa ili ajiuzulu. Je, kasi ya awamu ya tano imemtisha?

Nimemwambia huyo jamaa aweke japo sheria moja ambayo haipo na inatokana na huyo anaye msema mtu mmoja ili watu waone namimi akiweka hiyo sheria mpya inayotoka kichwani mwa mtu nitaomba mods wanipe ban ya mwezi mmoja au miwili.
Nadhani ni mmoja kati ya wale wanaimbishwa wimbo unasema dikteta lakini hawafahamu hata maana yake.
 
JE MNA KUMBUKUMBU KUWA HUYU MZEE HATA UBUNGE ALIJIUZULU MWENYEWE???????

HIVYO SIONI TATIZO KWANI KAMA ILIVYO KWA UBUNGE NDIVYO NA HAPO NDC ANAVYOFANYA.

NI MTU AMBAYE HATAKI KUNG'ANG'ANIA MADARAKA AMEAMUA KUACHIA VIJANA WAONGOZE.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
inakuuma nin sas? hupend watu km hawa mkuu?
 
Kwenye serikali hii ambayo sheria zote zipo kwenye kichwa cha mtu mmoja, mjanja lazima ajiuzulu. Yeye ndo anaamua nani ni fisadi na nani siyo fisadi. Yeye ndo anaamua ipi ni rushwa na ipi siyo rushwa. Hovyo kabisa.
Hata mwongee vipi hamtaizuia mvua kunyesha, wazembe ni lazima wakalishwe chini
 
Naomba unitajie japo sheria moja ambayo imetolewa kichwani mwa huyo unaye muhita mtu mmoja na uiweke hapa watu waione!

Ukiweza kufanya hivyo nitaomba @modrator wanipe ban ya mwezi mmoja kama si miwili!

Naomba uweke hizo sheria .
Yeye ndo anaamua kwamba watu fulani wameibia serikali bilioni kadhaa kwa hiyo wafungwe (refer siku ya sheria) ila LUGUMI siyo fisadi na anaongezewa muda wa kufunga mashine zile.

Juzi katunga sheria nyingine kwamba elfu 5 ya kumpa polisi siyo rushwa ila kuiba pesa nyingi ndo rushwa.
 
inakuuma nin sas? hupend watu km hawa mkuu?

Inaniuma sana kwa wale wanaong'ang'ania madaraka na ikiwa kuna damuchanga wanatoka vyuoni kila mwaka. Na ukiangalia hata mawazo ya hawa ving'ang'anizi ni ya mwaka 1917 enzi za ujima. huu ni wakati wa dotcom.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
Kwenye serikali hii ambayo sheria zote zipo kwenye kichwa cha mtu mmoja, mjanja lazima ajiuzulu. Yeye ndo anaamua nani ni fisadi na nani siyo fisadi. Yeye ndo anaamua ipi ni rushwa na ipi siyo rushwa. Hovyo kabisa.
Huyu ndo anafaa. Kesi toka nipo kijana mpaka Leo hii ni mzee haijaisha. Bora yeye
 
Baada ya Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani na kuanza kwa kasi kubwa, tumeshuhudia viongozi wengi wakiondolewa kwenye nyadhifa zao na wengine kujiondoa wenyewe kabla ya makubwa hayajawafika.

Viongozi wengi waliondolewa katika nyadhifa zao ni kuhusu tuhuma za ufisadi na kushindwa kutekeleza kile ambacho walipaswa kukifanya, kwa upande mwingine wameondolewa baada ya muda wao kumalizika.

Katika hali ya kushangaza, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Dkt Chrisant Mzindakaya amemuomba Rais Magufuli amruhusu kuachia wadhifa huo aliotumikia kwa miaka sita sasa.

Hili linaweza kuzua maswali mengi, je kuna tatizo kwenye shirika hilo? au kasi imekuwa kubwa? au anataka kupumzika na kupisha nafasi kwa mtu mwingine.?

Dkt Mzindakaya aliteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo julai 8.2011.
JIPU Limetumbuka lenyewe hilo!
 
Back
Top Bottom