Chrisant Mzindakaya amuomba Rais Magufuli ruhusa ili ajiuzulu. Je, kasi ya awamu ya tano imemtisha?

Wala si Tanga, ni Kigoma. Alikorofishana na mbunge wa Kigoma Mjini wa wakati huo, na yeye Chris alikuwa ni Mkuu wa mkoa. Wote wakatishiana na kila mmoja akaonyesha demo
Demo gani walionyeshana? Fungukeni vizuri bana! Nini kilikuwa chanzo? Kilichokuwa demonstrated ni nini? Nani aliibuka kidedea?
 
Awamu zilizopita ni nani aliyekuwa na sheria kwenye kichwa chake?

Kama inakukera kuona Rais ni Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi, nenda kabadilishe Ibara ya 33(2) na 34(3) ya Katiba ya Tanzania 1977.

Don't hate the player, hate the game.

Kumbuka, Rais ameapishwa ili kuilinda na kuitetea Katiba ya Tanzania.
Katiba hiyo hiyo inatoa uhuru kwa vyama vya siasa kufanya mikutano yao na haki ya kukutana na wananchi walio wachagua
 
Watu wenyewe kama ni makada wa ccm basi ni janga la taifa
Serikali ni ya watu wote, Mbona kuna makada weengi tu wa ukawa kwenye halmashauri zetu hata serikali kuu, na wanafahamika, wala hata haina madhara, what is required here is patriotism...
 
hahahahaaa...
kule Israil kuna Waziri aliachia mwenyewe baada ya kuona Prime Minister ni pasua akili.
 
Nakubaliana na uamzi wa mzindakaya kwa kuwa kwa sasa umri wake ni mkubwa,na Ninaamini ana busara kuliko wengine wanaong'ang'ania kwenye uongozi, mxindakaya ni msitaarabu sana hata kwenye ubunge aliamua kustaafu mwenyewe, Pia wewe Nehemia isaya usitukane mheshimiwa rais maana kusema sheria iko kwenye kichwa cha mtu mmoja ni sawa na kwamba shule ya msingi dara la tatu hukusoma somo la siasa...au hukusoma kabisa shule ya msingi...Kabla hujatuma neno lolote tafakari,usiwe na munkari kama mwendo wa farasi ambae brake yake mpaka akanyagwe na kuminywa....Umejifunza demokrasia lakini bado hujawa mwanademoraasia..anyway jiheshimu utaheshimiwa.
 
Kwenye serikali hii ambayo sheria zote zipo kwenye kichwa cha mtu mmoja, mjanja lazima ajiuzulu. Yeye ndo anaamua nani ni fisadi na nani siyo fisadi. Yeye ndo anaamua ipi ni rushwa na ipi siyo rushwa. Hovyo kabisa.
Chaka la Mafisadi ni chadema, mzindakaya kajifiche huko
 
Serikali ni ya watu wote, Mbona kuna makada weengi tu wa ukawa kwenye halmashauri zetu hata serikali kuu, na wanafahamika, wala hata haina madhara, what is required here is patriotism...
Ccm ni janga la kitaifa
 
Ufanyike uchunguzi kama hukuna madudu hapo ndio aondoke isije ikawa ni changa la macho hilo
 
Je
Baada ya Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani na kuanza kwa kasi kubwa, tumeshuhudia viongozi wengi wakiondolewa kwenye nyadhifa zao na wengine kujiondoa wenyewe kabla ya makubwa hayajawafika.

Viongozi wengi waliondolewa katika nyadhifa zao ni kuhusu tuhuma za ufisadi na kushindwa kutekeleza kile ambacho walipaswa kukifanya, kwa upande mwingine wameondolewa baada ya muda wao kumalizika.

Katika hali ya kushangaza, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Dkt Chrisant Mzindakaya amemuomba Rais Magufuli amruhusu kuachia wadhifa huo aliotumikia kwa miaka sita sasa.

Hili linaweza kuzua maswali mengi, je kuna tatizo kwenye shirika hilo? au kasi imekuwa kubwa? au anataka kupumzika na kupisha nafasi kwa mtu mwingine.?

Dkt Mzindakaya aliteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo julai 8.2011.

Je amesukumwa au karuka?!
 
Hili linaweza kuzua maswali mengi, je kuna tatizo kwenye shirika hilo? au kasi imekuwa kubwa? au anataka kupumzika na kupisha nafasi kwa mtu mwingine.?
Huenda amemumoa kijana hana nidhamu hahahahaha nimejisemea tu
 
Kwenye serikali hii ambayo sheria zote zipo kwenye kichwa cha mtu mmoja, mjanja lazima ajiuzulu. Yeye ndo anaamua nani ni fisadi na nani siyo fisadi. Yeye ndo anaamua ipi ni rushwa na ipi siyo rushwa. Hovyo kabisa.
Naomba unitajie japo sheria moja ambayo imetolewa kichwani mwa huyo unaye muhita mtu mmoja na uiweke hapa watu waione!

Ukiweza kufanya hivyo nitaomba @modrator wanipe ban ya mwezi mmoja kama si miwili!

Naomba uweke hizo sheria .
 
Awamu zilizopita ni nani aliyekuwa na sheria kwenye kichwa chake?

Kama inakukera kuona Rais ni Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi, nenda kabadilishe Ibara ya 33(2) na 34(3) ya Katiba ya Tanzania 1977.

Don't hate the player, hate the game.

Kumbuka, Rais ameapishwa ili kuilinda na kuitetea Katiba ya Tanzania.
Nimemwambia huyo jamaa aweke japo sheria moja ambayo haipo na inatokana na huyo anaye msema mtu mmoja ili watu waone namimi akiweka hiyo sheria mpya inayotoka kichwani mwa mtu nitaomba mods wanipe ban ya mwezi mmoja au miwili.
 
Back
Top Bottom