Chrisant Mzindakaya amuomba Rais Magufuli ruhusa ili ajiuzulu. Je, kasi ya awamu ya tano imemtisha?

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,431
2,000
Baada ya Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani na kuanza kwa kasi kubwa, tumeshuhudia viongozi wengi wakiondolewa kwenye nyadhifa zao na wengine kujiondoa wenyewe kabla ya makubwa hayajawafika.

Viongozi wengi waliondolewa katika nyadhifa zao ni kuhusu tuhuma za ufisadi na kushindwa kutekeleza kile ambacho walipaswa kukifanya, kwa upande mwingine wameondolewa baada ya muda wao kumalizika.

Katika hali ya kushangaza, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Dkt Chrisant Mzindakaya amemuomba Rais Magufuli amruhusu kuachia wadhifa huo aliotumikia kwa miaka sita sasa.

Hili linaweza kuzua maswali mengi, je kuna tatizo kwenye shirika hilo? au kasi imekuwa kubwa? au anataka kupumzika na kupisha nafasi kwa mtu mwingine.?

Dkt Mzindakaya aliteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo julai 8.2011.
 

popo1986

JF-Expert Member
Jul 30, 2014
1,121
1,250
Mheshiwa Rais naomba kazi ya mmoja wapo aliyetoka Hao inaonyesha ni jinsi gani sio waaminifu sasa wanajishtukia mapema labda vyeti tatizo
 

Muharango

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,664
2,000
Tumia akili kufikiria zaidi ya kutukiwa, utaendelea kutimika hadi lini?
#Badilika
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,431
2,000
OK.. hatuna budi kuheshimu maamuzi yake
1469011286074.jpg
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,884
2,000
Huyu ndio Chrisant Mzindakaya Maji ya Tanga.

Kama ni kweli basi apumzike tu.

Halafu, mwanae Paul hakuwa na sifa za kuwa mkuu wa wilaya, alipata nafasi hiyo kwa bahati mbaya.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,025
2,000
Kwenye serikali hii ambayo sheria zote zipo kwenye kichwa cha mtu mmoja, mjanja lazima ajiuzulu. Yeye ndo anaamua nani ni fisadi na nani siyo fisadi. Yeye ndo anaamua ipi ni rushwa na ipi siyo rushwa. Hovyo kabisa.
Awamu zilizopita ni nani aliyekuwa na sheria kwenye kichwa chake?

Kama inakukera kuona Rais ni Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi, nenda kabadilishe Ibara ya 33(2) na 34(3) ya Katiba ya Tanzania 1977.

Don't hate the player, hate the game.

Kumbuka, Rais ameapishwa ili kuilinda na kuitetea Katiba ya Tanzania.
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,929
2,000
Wala si Tanga, ni Kigoma. Alikorofishana na mbunge wa Kigoma Mjini wa wakati huo, na yeye Chris alikuwa ni Mkuu wa mkoa. Wote wakatishiana na kila mmoja akaonyesha demo
Yaani hiyo demo ilikuwa hatari iliacha isitolia isiyofutika, hivi siku hizi mambo hayo yapo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom