Chris Brown huenda akafukuzwa kenya kama Koffi Olomide, aivunja simu ya shabiki

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
1475938155165.jpg
Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani Chris Brown, aliwasili jijini Mombasa na kujikuta akizua gumzo baada ya kuitupa chini na kuivunja simu ya kiganjani ya shabiki mmoja.

Tukio hilo limetokea uwanja wa ndege wakati msichana wa Kenya (aliyevaa sketi nyeusi katika picha) alijisogeza kwa Chris Brown ili aweze kupiga naye picha, maarufu kama 'Selfie'

Katika hali ambayo iliwashangaza watu walioshuhudia tukio hilo ikiwa pamoja na waandishi wa habari, Mwanamuziki huyo alichukuwa simu ya dada huyo akaitupa chini na kwenda kupanda gari iliyoandaliwa kwa ajili ya kumchukua
1475938754450.jpg
Akihojiwa na vyombo vya habari baada ya tukio hilo, msichana huyo amesema amesikitishwa na kitendo cha Chris Brown ambacho amekiita ni cha udhalilishaji na amesema ataripoti polisi ikiwa ni pamoja na kuharibu simu yake

Habari inayoendelea hivi sasa kenya ni kuwepo kwa wito kwa wananchi kususia onyesho la Mwanamuziki huyo ikiwa na pamoja na kuzitaka mamlaka za nchi hiyo kumfukuza nchini humo Chris Brown kama zilivyofanya kwa Koffi Olomide miezi michache iliyopita.

Chanzo : Citizen Tv
 
U star unakuja na gharama, ukitaka u star bila kukubali kuuza faragha yako ni kama kutaka mshahara bila kufanya kazi.

Wengine tulikuwa na nafasi ya kupata u star kitambo lakini tukakataa kwa sabau ya kujali zaidi faragha.
 
hamna kesi yoyote hapo na hajamdhalilisha, maana huyo mwanamke ametaka kipiga picha na mtu bila ridhaa yake, ambayo naye kafanya kosa vile vile. tatizo letu tumeendekeza sana ujamaa kila kitu tunaona kama tunaonewa. hilo tukio la kawaida sana. waandishi wa habari wanao wahoji mastaa wengi wanakutana na hizo kero
 
U star unakuja na gharama, ukitaka u star bila kukubali kuuza faragha yako ni kama kutaka mshahara bila kufanya kazi.

Wengine tulikuwa na nafasi ya kupata u star kitambo lakini tukakataa kwa sabau ya kujali zaidi faragha.
Dah!
 
Tatizo lake chris bange zimemzidia, wewe mtu aliyetoka "rehab" unadhani atakuwa mtimamu 100%??????
 
Back
Top Bottom