Chopa ya JWTZ yaanguka na Kuua..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
siren.gif

Habari zinazoingia sasa hivi zinasema kuwa Helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ikitokea Arusha imeanguka ikiwa njiani kuelekea Dodoma na kuua watu sita papo hapo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi Matei Basilio amethibitisha kutokea ajali hiyo ambayo amesema haikuhusisha wajumbe wa mkutano wa Sullivan kama ilivyoripotiwa awali.

Akizungumza na KLH News muda mfupi uliopita Kamanda Basilio (SACP) amesema kuwa ajali hiyo imetokea eneo la kijiji cha Matevesi-Kisongo umbali wa kama Kilomita 17 kutoka Arusha majira ya saa sita mchana. Bw. Basilio amesema kuwa waliofariki katika ajali hiyo ni watu sita wakiwemo rubani na fundi, mama na mtoto wa kike wa miaka kumi na maafisa wa jeshi hilo ambao walikuwa wamepewa lifti kuelekea Dodoma.

Kamanda Basilio amesema kuwa ndege hiyo ilianguka kwenye eneo hilo na kuwaka kulipuka na ni wanakijiji wa eneo hilo waliotoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo. Hata hivyo Kamanda Basilio amesema kuwa ndege hiyo haikusababisha madhara ardhini kwani iliangukia umbali na makazi ya watu na hilo limechangia kuepusha maafa makubwa.
 
Hizi ni habari za kusikitisha, naamini Taasisi inayohusika itakuwa tayari kutoa taarifa zaidi juu ya ajali pamoja na wale waliokuwemo.
Nachukuwa nafasi hii kutoa pole kwa wale wote ambao watakuwa wameguswa na msiba huu kwa njia moja au nyingine. Msiba ni msiba, kama watakuwa maafisa wa jeshi au raia, naamini wananchi watapata fursa ya kujua juu ya huo Mkasa. Kwa mara nyingine tena natoa pole kwa waliodhurika na mkasa huo.
 
huku ikiwa imebeba baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Sullivan ulioisha mwishoni mwa juma mkoani Arusha. Habari zinasema watu nane wakiwemo marubani wawili wamefariki dunia na tayari jitihada za kuitafuta miili na kujua chanzo cha ajali zimeanza.

.. natumaini hii ajali haitaamsha ile nyingine ya "helikopta ya JWTZ na wapiga picha za utalii"!
 
....kudadek ...sasa huu ni ujinga,,..hii ni chopa ya pili ...kati ya nne alizo supply vithlani [kwanza alisupply fake pili alisupply civilian choppers badala ya gunship]kuanguka ndani ya kipindi cha miezi mitatu...ya kwanza ilianguka pale ziwa natron...hii helicopter naikumbuka kwani ndiyo iliyokuwa ikitoa ulinzi ilipoazimwa kwa polisi wakati woote wa mkutano wa sullivan......

....natamani damu ya vithlani....HAYA NDIO MATUNDA YA UFISADI KWENYE ZANA ZA ULINZI...yanawaumiza marubani wetu na wasafiri wasiokuwa na hatia..kwa kuleta misiba!!!
 
Phillemon... kwanini unafikiri ni "chopa" hiyo? Nilikuwa na mawazo hayo lakini sina pa kuanzia.. kwanini isiwe ni nyingine..
 
ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja tayari helkopter mbili za jeshi zimeshaanguka na kusababisha maafa kwa wanajeshi!hii inauma sana kwa kuona wanajeshi wetu wakitumia vifaa vya kizamani na vichakavu kwani inawafanya wayaweke maisha yao rehani!
habari za uhakika ni kwamba helkopter hiyo ilikuwa inaelekea dar na sio dodoma,na ilikuwa na wanajeshi wanne na mke wa ofisa wa jeshi,na imeanguka kilometa tano toka iliporuka na wote wamefariki dunia!
MUNGU AZILAZE MAHALI PEMA PEPONI,AMINA
 
M'Kijiji kutengeneza Mabillionea sio kazi rahisi, so lazima wengine waumie ili wengine wapate (wawe sacrifice). Simple economics. Ingwa sipendi, lakini wengine wanaipenda hiyo njia, ya kutoa fakara wenzao, sio ile ya kiswahili, lakini kwa kuwababesha wengine mizigo yao, kama madawa mabovu, chakula mikataba feki, etc etc
 
RIP kwa marehemu na Mungu awape faraja familia zao.

Kama hii ni moja ya zile helikopta 4 za Vithlani basi kazi ipo.
 
Zile mbili zilizobakia inabidi ziwe grounded uchunguzi ufanyike, ile ya lake Natron hivi walisema chanzo cha ajali ni nini vile?
 
ooh my GOD!why this!MUNGU awalaze marehemu mahali pema peponi
Amen!
 
Hivi hawa jamaa ndege zao zina nini?kila siku tunawalaumu madereva wa mabasi ya abiria kumbe wana usalama wetu nao si lolote si chochote.Nikunganisha matukioa,kama sijasahau sana,kuna ndege ya JW ilianguka manyara nadhani mwaka huu huu,wakati nyingine ilianguka kule dodoma,haya na sasa hii,kulikoni hizi ndege za JW?Nadhani zote zinahitaji kukaguliwa ili kujua whether they are airworthy or not?na kama sio bora zifungiwe tu na mamlaka husika. Poleni sana watanzania wenzangu,mungu awalaze pema peponi marehemu wote.
 
jamani kuna mahala majina ya waliofariki yamewekwa???ujue tuna ndugu zetu kwenye idara hiyo wengine lakini the news haziko kamili
 
Mungu ibariki Tanzania yangu tuepushe na balaa hili .Wamwagie moto mafisadi kwenye magari yao ama majumba yao .
 
Nina wasiwasi na wakaguzi wao...maana kama ni za jeshi watakuwa wanawaogopa kuwakagua kama wanavyokaguaa zile za civilian ili ku maintain standard za kimataifa za usalama wa anga.....sidhani kama kweli wana access kuzikagua mara kwa mara ndege za jeshi......(kumilikiwa na jeshi)...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom