Chonji mfanyabiashara wa madawa ya kulevya hali tete, ikibainika kweli lazima afilisiwe

The bos

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
350
80
HALI tete, siku chache baada ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji kukamatwa na kutupwa gerezani kwa tuhuma za kukamatwa na dawa kulevya, sasa mali zake zimeanza kuchunguzwa.

Vyanzo vyetu makini kutoka jeshi la polisi zinasema kuwa mali zinazochunguzwa kutokana na tuhuma hizo nzito ni maghorofa, fedha pamoja na magari anayomiliki. “Tuliambiwa kuwa huyu bwana alikuwa akiishi maisha ya hali ya juu, sasa kutokana na tuhumza zake polisi wameanza kuchunguza kila alichonacho ili kujua uhalali wake,” kilisema chanzo.

Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo akiwemo mtoto wa meya mmoja wa zamani (jina tunalihifadhi), jijini Dar es Salaam ambaye anadaiwa kuwa alikuwemo katika mkumbo wa kukamatwa Chonji lakini alitoroka na sasa anasakwa na polisi.

Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa alipotafutwa na gazeti hili ili afafanue madai hayo alisema uchunguzi wa mali za wote wanaotuhumiwa kukamtwa na dawa za kulevya ni lazima ufanyike

“Tunachunguza mali zao wote waliokamatwa na tuhuma za dawa za kulevya na siyo kwa Chonji peke yake, inapodhihirika kuwa ni za madawa huwa wanafilisiwa,” alisema Kamanda Nzowa. Chonji na wenzake wanne walikamatwa usiku wa manane Oktoba 21, mwaka huu nyumbani kwake Magomeni Mtaa wa Kondoa jijini Dar- na inadaiwa walikuwa- na mzigo wa unga uliokuwa ukifungwa katika vifurushi vidovidogo pia anadaiwa kukutwa na sare za jeshi (JWTZ) na bastola.
 
Hamna lolote waanze kujikamata kwanza wao halafu wafuate wengine wapo wengi tu.
 
hyo cku ilikuwa balaa,kunà jamaa mmoja yupo nàe anaitwa tanaka/ tanaruza anarushwa sana na wasanii km kassim mganga ,huyu jamaa n bonge wakat watu wanaruka ukuta yy anahangaika kuvua viatu huku àlivaa manga nyeupe imejaa damu kwa kujaribu kuruka lakin akafeli wakamkamata
 
aaaahaaaa nimecheka sana
 
Wana mbwela mbwela tu hao...mwisho wa siku utasikia mahakam inasema hakuna ushahidi wa kutosha juu ya tuhuma zao , na hivyo tuna waachia huru chonji na wenzake wakale bata uraia (wakaone jua).
 
Last edited by a moderator:
huyu jamaa alikataa kula na mkuu wa kaya...yaani mkwe.re anaingiza coca cola zake na huyu nae anaingiza coca cola zake...mkuu akamwita akampiga mkwara akamwambia kama unataka tuungane nikupe mzigo uzungushe si unajua nimebakiza mwaka mmoja tu so nataka nipige hela kwa hasira mno mwaka huu...huyu mtoto wa mjini akaona huyu mkwe.re mjinga nn yaani naweza kujiajiri kwanini niajiriwe ndio akagoma kugoma mkwe.re akamwambia ngoja nikuoneashe ndio namna hiyo yamemfika mtoto wa mjini
 
hyo cku ilikuwa balaa,kunà jamaa mmoja yupo nàe anaitwa tanaka/ tanaruza anarushwa sana na wasanii km kassim mganga ,huyu jamaa n bonge wakat watu wanaruka ukuta yy anahangaika kuvua viatu huku àlivaa manga nyeupe imejaa damu kwa kujaribu kuruka lakin akafeli wakamkamata

ahh umenifanya nicheke hahaha..tanaruza kadakwa naye
 
mtoto wa meya mmoja wa zamani jijini Dar es Salaam....????*%*&%$$$
 
Back
Top Bottom