#COVID19 Chongolo: Viongozi wa CCM wanaopinga Chanjo mchakato wa kuwashughulikia umeanza, hakuna aliye mkubwa kuliko chama

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,850
141,771
Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongolo amesema mchakato wa kuwashughulikia kinidhamu viongozi wa CCM wanaopinga chanjo kinyume na maelekezo ya chama umeshaanza na karibu utakamilika.

Mtasikia hivi karibuni hatua tulizowachukulia amesema Chongolo.

Chanzo: Channel ten
 
IMG-20210811-WA0125.jpg
 
Mambo ya mdiyo mzee kama kawaida......naona leo gazeti la Uhuru lifungiwa na katibu...........mbwa amemfuata mwenyewe hadi Msikitini
 
Ukada au uanachama wa chama chochote haujawahi kuwa muhimu kuliko afya ya mhusika.

Na hapa ndo tutawaona wanafiki wasioyaishi maneno ya vinywa vyao.

Na kwa msimamo huu wenye akili tumeanza kuelewa kwamba kumbe chanjo si hiari bali ni lazima.
 
Back
Top Bottom