Chongolo: Popote Duniani muda wa porojo za siasa ni kipindi cha kampeni pekee

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,192
"...hata huko kwenye Nchi vinara wa demokrasia huwa wanafanya mikutano ya hadhara na kupiga porojo za siasa kipindi cha kampeni za uchaguzi pekee na baada ya hapo aliyeshinda huachiwa aendeshe Nchi."

"...sasa huu utamaduni wa eti kila wakati wanasiasa wafanye siasa hata huko Duniani haupo na mbaya zaidi hii tabia inamsukumo mkubwa sana kwenye Nchi zetu za kiafrika hasa hapa kwetu Tanzania." Amesema Chongolo Katibu mkuu wa CCM.

My take: Mama anaupiga mwingi sana.
 
"...hata huko kwenye Nchi vinara wa demokrasia huwa wanafanya mikutano ya hadhara na kupiga porojo za siasa kipindi cha kampeni za uchaguzi pekee na baada ya hapo aliyeshinda huachiwa aendeshe Nchi...
Kweli kabisa

USSR
 
Wala usizungumzie popote duniani hata hapa nchi za jirani shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara ni miaka yote siyo wakati wa kampeni tu.

Uchaguzi mkuu kenya ni 2022 lkn ukifungulia taarifa za tv kenya mikutano inaendelea kila kona ya nchi. Raila anazindua kampeni zake keshokutwa kasarani. Hizo ndizo nchi za kidemokrasi.

Hapa bongo akina mama wa chadema wanazuiwa na maaskari kufanya jogging jmamosi kawe eti hawana kibali kwakuwa tu wamevaa jezi za kudai katiba mpya.

Ni vizuri ndugu chongolo akaelewa watanzania wanaangalia tvs na kuona kote duniani kinachoendelea. Labda kama anataka tuwaige korea kaskazini.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
"...hata huko kwenye Nchi vinara wa demokrasia huwa wanafanya mikutano ya hadhara na kupiga porojo za siasa kipindi cha kampeni za uchaguzi pekee na baada ya hapo aliyeshinda huachiwa aendeshe Nchi...
Huyu ni katibu wa chama kikongwe cha siasa barani Africa,anaongea namna hii.

Hivii yeye anachokifanya huko anakozunguka kina tija gani Kwa taifa?

Mpaka Leo watu wanalalamika umeme,maji,barabara mbovu,utendaji mbovu wa viongozi wa selikari,ufisadii nk. Wakati Tanzania imeongozwa na chama kimoja Kwa miongo yoteee,bado unaona shida ni wapinzanii?

Tukubali tumefilisika kifikra kwa sasa.
 
Ana maana viongozi wa vyama vya siasa ( hasa vya upinzani ) hawapaswi/hawaruhusiwi kuongea na wanachama wao hadharani hadi kipindi cha kampeni za uchaguzi ? Siyo sahihi
 
"...hata huko kwenye Nchi vinara wa demokrasia huwa wanafanya mikutano ya hadhara na kupiga porojo za siasa kipindi cha kampeni za uchaguzi pekee na baada ya hapo aliyeshinda huachiwa aendeshe Nchi...
Maharage gani kala huyu?? Baada ya uchaguzi kuna kukijenga chama. Mbona yeye na mtumbo wake hakai ofisini?
 
Sishangai kwa Chongolo kusema hivi...ninachoshangaa ni wahandishi wa habari kutomuhoji mbona yeye anafanya mikutano? wakati sio wakati wa kampeni?
 
"...hata huko kwenye Nchi vinara wa demokrasia huwa wanafanya mikutano ya hadhara na kupiga porojo za siasa kipindi cha kampeni za uchaguzi pekee na baada ya hapo aliyeshinda huachiwa aendeshe Nchi...
Hiyo dunia anayozungumzia Bw. Chongolo haipo ulimwengu huu, itakuwa anaota ndoto!
 
Anauhalalisha ubanaji wa demokrasia. Si ni serikali hii hii ya sisiemu enzi ya awamu ya tatu na nne siasa za upinzani zilishamiri? Kwani Nini kilitokea?

Wao waendeleze udikteta wao, nayo watatoka madarakani na historia Yao itabaki kwa vizazi vingine
 
"...hata huko kwenye Nchi vinara wa demokrasia huwa wanafanya mikutano ya hadhara na kupiga porojo za siasa kipindi cha kampeni za uchaguzi pekee na baada ya hapo aliyeshinda huachiwa aendeshe Nchi....
Bila hizi Porojo Chadema watakosa fedha za mabeberu na akina Heche watakufa njaa
 
Dah inasikitisha Sana .sikujua Kama wakati wa kampeni ni porojo .mi nlijua wana Nadi sera ambazo watatekeleza Mara wapatapo ridhaa ya wananchi . Kumbe ni po rojo ,?
 
Back
Top Bottom