Chongolo hukijengi chama bali unakibomoa kwa kurudisha makundi ndani ya CCM. Hisia zangu chama kineanda kukatika vipande viwili

Ngoja ukweli tuuseme hapa hapa ili kuweka kumbukumbu sawa.

Unapomtaja Chongolo maana yake unamtaja Samia na unampotaja Bashiru maana yake unamtaja Magufuli. Hivyo kama ni pongezi au lawama zinapaswa kuwalenga Samia au Magufuli kwa siasa zao ndani ya CCM, tusikwepeshe maneno.

Pili, ukweli ni kwamba anachokifanya Samia sasa (kupitia Chongolo) ndio kitu kile kile alichokuwa anakifanya Magufuli (kupitia Bashiru), yaani kufumua mfumo wote wa watendaji wa CCM uliokuwepo halafu simika mfumo mpya uliojaa watu wako tu. Na kwanini wanafanya hayo, jibu ni moja tu, wote wawili (Samia na Magufuli) hawakuwahi kuwa na nguvu au mtandao mpana wa kisiasa ndani ya CCM kabla ya kuzawadiwa urais na kisha uenyekiti wa CCM. Yaani hawakuwa wanakubalika vyema na wanaCCM waandamizi kabla ya kupata madaraka.

Magufuli alikuwa ovyo....
Samia yuko ovyo....
CCM iko ovyo ovyo.
Ndo umeandika ugoro Gani Sasa hapo
 
Ni ukweli pasipo shaka Magufuli alikirudisha Chama kwenye mstari.
Je utakubaliana na mimi kuwa ndani yake kulikuwa na kikundi cha wasiojulikana?

Huku mitaani wanasema Hangaya amejiwekea mazingira magumu kuuzika kwa chama 2025.
Sababu kuu in
1.Issue ya Machinga.
2.Kamatakamata ya wapinzani.
3.Kurithi kesi zakusadikika.
4.Umeme kukatika ovyo.
5.Kuwateua waliodharau taasisi nyingine za vyama.
6.Mkuu wa bunge hapendeki ndani na nje ya bunge.

Anachohubiri Chongolo nikama anachochea makundi.Kipimo wanadai aamuru kila mbunge aitishe mikutano ya hadhara wananchi wawe guru kuuliza maswali.
Kwasababu alitumia Bunduki kupitisha mabegi ya kura
 
Kwahiyo chadema ndio taasisi imara?

Kama sio imara vyombo vya dola vinatumia nguvu kupambana nacho kwanini? Kushurutisha kuogopwa kwa kutumia vikundi vya mungiki hakujawahi kukipa uimara chama chochote cha siasa. Na mkilogwa kuingia kwenye uchaguzi wa halali, ndio mtajua mlishapitwa na wakati muda mrefu sana.
 
Nakumbuka ilifikia mahala tuliona aibu kuvaa sare za hiki chama ,chama kilijaa wapigaji waliojimilikisha raslimali za chama chetu,
Chama kiliishi kwa kutembeza bakuri kwa watanzania wenzetu wenye ukwasi , wahindi ,waarabu ,ambao ni wafanyabiashara wakubwa ,ambao nao walitumia nafasi hiyo kukwepea kodi za serikali,

Alipoingia Magufuli,alikusanya Assets zote za CCM,alihakikisha kwamba chama ni kikubwa kuliko mwanachama yoyote,akahakikisha CCM inajitegemea kilaslimali fedha ,chama kikaondokana na utegemezi, account ya chama ikanona kwelikweli, umimi ndani ya CCM ukatoweka ,chama kikarudi kwa wanachama na kuwa taasisi imara zaidi.

Cha kustajaabisha chama unakifumua kwa maslahi binafsi ukilenga chaguzi ijayo. Hili linajidhihirisha kwa kutengua makatibu wa CCM wengi kwa mkupuo na haraka sana ,ukizingatia hili halijawahi fanyika toka tupate uhuru.

Hapa umejikita kwa kuamini unamsaidia mwenyekiti,fahamu unamchimbia kaburi tu la kisiasa . mwenyekiti salama yake kama kiongozi ipo katika uwajibikaji uliotukuka kwa kutatua kero sugu za wananchi hasa rushwa kubwa na ndogo ndogo.

Aliyofanya hayati Magufuli kwa upande wa CCM yalikuwa yenye tija sana na sisi wanachama wa chini wa kawaida tulimuelewa .

Tulianza kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama pasi kuhofia kutokuwa na pesa ,lakini kabla ya Magufuli ilitegemea nani yuko juu yako mwenye maamuz,i au fedha ulionayo.

Nionavyo ,kwa kasi kubwa unaturudisha huko tulipotoka ,kumbuka chama legelege huzaa serikali legelege

Nikuhakikishie sisi wafia chama hatutakubali kurudi utumwani misri,na huko tuelekeako ndio mwisho hii taasisi ambayo mnataka kuirudisha kwenye umimi .

Fukuto ni kubwa na hatukubaliani na kinachondelea ndani ya chama na serikali. Zipo hujuma za wazi kabisa dhidi ya miradi ya kimkakati lakini chama kipo kimya serikali ipo kimya .hii haikubaliki hata kidogo.

Nimekusikia ukiwa mkoani Kagera na wazee wa CCM unasema siasa sio uadui ,lakini unarudisha safu kuleta makundi na uadui ndani chama .mshauri wako anakudanganya.nijuacho waliomlalamikia Magufuli ni wale walionyanganywa mali za CCM,mengine ni uzushi tu.

Nikufahamishe ,kwa sasa tumeelimika,hatudanganyiki tena mkituzingua tutawazingua,

Mwisho, kama hutajali achieni taarifa ya ukaguzi wa mali za chama ,maarufu kama ripoti ya Bashiru, na ripoti yako wewe Chongolo dhidi ya Bashiru na sekretarieti yake kipindi cha Magufuli, tulinganie ni kipindi kipi chama kilifanya vizuri au vibaya ili twende sawa, lengo tufahamu ipi ni CCM makini ya kuanzia kwa Makamba, Kinana na sekretarieti zake, au ya Magufuli na Bashiru, tuna jambo tunahitaji kujifunza
Si muuane tu nchi iwe shwari,chongolo anaupiga mwingi kma mama
 
Chongolo anakijua chama , Ni zao la Chama, Magufuli ,Bashiru na Polepole walikuwa hawakijui Chama ndio maana , Chama kiliyumba na kuendeshwa Kidikteta maana kilikuwa na wageni na mamluki
 
Bashiru alikijenga na kukishape sana hilo lichama takataka la ccm,walioingia sa hivi nafikir wanaisaka ile report ya bashiru waichome moto kabisa
Wakifanya hovyo ma wewe siuta pona , kwani ripoti ilisema hakuna msafi
 
Chongolo anakijua chama , Ni zao la Chama, Magufuli ,Bashiru na Polepole walikuwa hawakijui Chama ndio maana , Chama kiliyumba na kuendeshwa Kidikteta maana kilikuwa na wageni na mamluki
Anachojua changolo ni kutengeneza makundi ndani ya CCM,hana jipya,ndio kipindi chao chama kilikuwa tegemezi
 
Bashiru alikijenga na kukishape sana hilo lichama takataka la ccm,walioingia sa hivi nafikir wanaisaka ile report ya bashiru waichome moto kabisa
To me katika miaka 20 iliyopita Bashiru ndio katibu mkuu wa CCM aliyekuwa Makini na Mwerevu na mtaalamu kuliko wote waliopita...

Nilichojifunza Mama Samia si mtu muumini wa watu makini na walio vizuri kichwani.

Mama Samia ni mwanasiasa ambaye si msomi, ila Magufuli alikuwa ni msomi na anaamini Elimu
 
Magufuli yupi.
Aliyesema aliandikiwa barua Mara 3 na Maalim seif lakini hakumjibu.
Aliyeingia Ikulu akaanza kusema ikulu kumeoza,mambo ovyoovyo tu.Waliomtangulia alikuwa sehemu ya mawaziri na chama kilekile(alikosa heshima)
Huyu aliyewaita ngozi nyeupe MABEBERU huku akijua betri na gunzi mpaka warecharge wao.

Huyu aliyesema ukiona bendera zenye rangi nyekundi ujue hao ni nyonya damu,huku akijua kuna China nk bendera zao ni nyekundu.

Huyu aliyekuwa ananunua ndege cash huku wanyonge hawana maji,huyu aliyekuwa anasafiri njia nzima nikutumbua kwa kauli huku akiwa anasema Goverment goes with paper.
Msomi yupi unayetuaminisha.
 
Jpm aliwajali sana wasomi nchi hii,ndo Mana KWA wakati wake maproffesor,madr na wengi walosoma walipewa vitengo vya kuendesha.

Mama KWA Sasa anaenda na wapiga dili,ndo Mana hata watu ambao Wana ukakasi wa vyeti feki wanarudishwa kisa tu ni watoto wengi wa makada ambao yeye anataka wamuunge mkono,nchi KWA Sasa haipo ktk mikono salama kabisa.Tumuombee tu Ili walau astuke
 
Magufuli yupi.
Aliyesema aliandikiwa barua Mara 3 na Maalim seif lakini hakumjibu.
Aliyeingia Ikulu akaanza kusema ikulu kumeoza,mambo ovyoovyo tu.Waliomtangulia alikuwa sehemu ya mawaziri na chama kilekile(alikosa heshima)
Huyu aliyewaita ngozi nyeupe MABEBERU huku akijua betri na gunzi mpaka warecharge wao.

Huyu aliyesema ukiona bendera zenye rangi nyekundi ujue hao ni nyonya damu,huku akijua kuna China nk bendera zao ni nyekundu.

Huyu aliyekuwa ananunua ndege cash huku wanyonge hawana maji,huyu aliyekuwa anasafiri njia nzima nikutumbua kwa kauli huku akiwa anasema Goverment goes with paper.
Msomi yupi unayetuaminisha.
Maji Gani,maji haya ya mgao!

Acha mihemuko isiyo na msingi wewe vyeti feki
 
tofautisheni magufuli na Samia
Magufuli alikua anaitengeneza ccm yake binafsi(dictator) wakati Samia anaitawanya kwenda mashinani ili kwenda sawa na chadema ni msingi
Unarekebisha CCM wakati unafukuza wamachinga bila na kuwa sehemu ya kuwapeleka, unaweka mgao wa umeme na maji. Hivi nyie mnasahau hali ya CCM mwaka 2015
 
Nakumbuka ilifikia mahala tuliona aibu kuvaa sare za hiki chama ,chama kilijaa wapigaji waliojimilikisha raslimali za chama chetu,
Chama kiliishi kwa kutembeza bakuri kwa watanzania wenzetu wenye ukwasi , wahindi ,waarabu ,ambao ni wafanyabiashara wakubwa ,ambao nao walitumia nafasi hiyo kukwepea kodi za serikali,

Alipoingia Magufuli,alikusanya Assets zote za CCM,alihakikisha kwamba chama ni kikubwa kuliko mwanachama yoyote,akahakikisha CCM inajitegemea kilaslimali fedha ,chama kikaondokana na utegemezi, account ya chama ikanona kwelikweli, umimi ndani ya CCM ukatoweka ,chama kikarudi kwa wanachama na kuwa taasisi imara zaidi.

Cha kustajaabisha chama unakifumua kwa maslahi binafsi ukilenga chaguzi ijayo. Hili linajidhihirisha kwa kutengua makatibu wa CCM wengi kwa mkupuo na haraka sana ,ukizingatia hili halijawahi fanyika toka tupate uhuru.

Hapa umejikita kwa kuamini unamsaidia mwenyekiti,fahamu unamchimbia kaburi tu la kisiasa . mwenyekiti salama yake kama kiongozi ipo katika uwajibikaji uliotukuka kwa kutatua kero sugu za wananchi hasa rushwa kubwa na ndogo ndogo.

Aliyofanya hayati Magufuli kwa upande wa CCM yalikuwa yenye tija sana na sisi wanachama wa chini wa kawaida tulimuelewa .

Tulianza kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama pasi kuhofia kutokuwa na pesa ,lakini kabla ya Magufuli ilitegemea nani yuko juu yako mwenye maamuz,i au fedha ulionayo.

Nionavyo ,kwa kasi kubwa unaturudisha huko tulipotoka ,kumbuka chama legelege huzaa serikali legelege

Nikuhakikishie sisi wafia chama hatutakubali kurudi utumwani misri,na huko tuelekeako ndio mwisho hii taasisi ambayo mnataka kuirudisha kwenye umimi .

Fukuto ni kubwa na hatukubaliani na kinachondelea ndani ya chama na serikali. Zipo hujuma za wazi kabisa dhidi ya miradi ya kimkakati lakini chama kipo kimya serikali ipo kimya .hii haikubaliki hata kidogo.

Nimekusikia ukiwa mkoani Kagera na wazee wa CCM unasema siasa sio uadui ,lakini unarudisha safu kuleta makundi na uadui ndani chama .mshauri wako anakudanganya.nijuacho waliomlalamikia Magufuli ni wale walionyanganywa mali za CCM,mengine ni uzushi tu.

Nikufahamishe ,kwa sasa tumeelimika,hatudanganyiki tena mkituzingua tutawazingua,

Mwisho, kama hutajali achieni taarifa ya ukaguzi wa mali za chama ,maarufu kama ripoti ya Bashiru, na ripoti yako wewe Chongolo dhidi ya Bashiru na sekretarieti yake kipindi cha Magufuli, tulinganie ni kipindi kipi chama kilifanya vizuri au vibaya ili twende sawa, lengo tufahamu ipi ni CCM makini ya kuanzia kwa Makamba, Kinana na sekretarieti zake, au ya Magufuli na Bashiru, tuna jambo tunahitaji kujifunza
Mtamkumbuka Mwamba JPM, CCM ilikuwa kubwa kuliko mtu wakati wa JPM kuliko wakati mwingine wowote.

Sasa hivi hali ni tofauti mtaona nishai hata kuvaa hizo sare zenu, Mzee VASCO DA GAMA anawaongoza kwa remote na anawarudisha kwenye ile awamu yake ambapo mambo yalikuwa yakifanyika kienyeji enyeji tu, uswahili mwingi, na watu kujipigia hela tu.

Wengine tulikuwa tukimkubali JPM sio kwa sababu ya ushabiki wa Chama, ni kwa sababu ya Principles zake tu, na Nchi ilikuwa inanyooka kila mtu alikuwa akiwajibika kwenye eneo lake, hapakuwa na kucheka na kima. Principles zake za kiuongozi ndizo zinazotakiwa hasa kwa Nchi kama zetu hizi za Kiswahili swahili ambazo waswahili hifikiria kucheka cheka tu, kusafiri safiri tu, kuomba omba tu.
 
Ukweli mchungu
 
Back
Top Bottom