thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Nakumbuka ilifikia mahala tuliona aibu kuvaa sare za hiki chama ,chama kilijaa wapigaji waliojimilikisha raslimali za chama chetu,
Chama kiliishi kwa kutembeza bakuri kwa watanzania wenzetu wenye ukwasi , wahindi ,waarabu ,ambao ni wafanyabiashara wakubwa ,ambao nao walitumia nafasi hiyo kukwepea kodi za serikali,
Alipoingia Magufuli,alikusanya Assets zote za CCM,alihakikisha kwamba chama ni kikubwa kuliko mwanachama yoyote,akahakikisha CCM inajitegemea kilaslimali fedha ,chama kikaondokana na utegemezi, account ya chama ikanona kwelikweli, umimi ndani ya CCM ukatoweka ,chama kikarudi kwa wanachama na kuwa taasisi imara zaidi.
Cha kustajaabisha chama unakifumua kwa maslahi binafsi ukilenga chaguzi ijayo. Hili linajidhihirisha kwa kutengua makatibu wa CCM wengi kwa mkupuo na haraka sana ,ukizingatia hili halijawahi fanyika toka tupate uhuru.
Hapa umejikita kwa kuamini unamsaidia mwenyekiti,fahamu unamchimbia kaburi tu la kisiasa . mwenyekiti salama yake kama kiongozi ipo katika uwajibikaji uliotukuka kwa kutatua kero sugu za wananchi hasa rushwa kubwa na ndogo ndogo.
Aliyofanya hayati Magufuli kwa upande wa CCM yalikuwa yenye tija sana na sisi wanachama wa chini wa kawaida tulimuelewa .
Tulianza kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama pasi kuhofia kutokuwa na pesa ,lakini kabla ya Magufuli ilitegemea nani yuko juu yako mwenye maamuz,i au fedha ulionayo.
Nionavyo ,kwa kasi kubwa unaturudisha huko tulipotoka ,kumbuka chama legelege huzaa serikali legelege
Nikuhakikishie sisi wafia chama hatutakubali kurudi utumwani misri,na huko tuelekeako ndio mwisho hii taasisi ambayo mnataka kuirudisha kwenye umimi .
Fukuto ni kubwa na hatukubaliani na kinachondelea ndani ya chama na serikali. Zipo hujuma za wazi kabisa dhidi ya miradi ya kimkakati lakini chama kipo kimya serikali ipo kimya .hii haikubaliki hata kidogo.
Nimekusikia ukiwa mkoani Kagera na wazee wa CCM unasema siasa sio uadui ,lakini unarudisha safu kuleta makundi na uadui ndani chama .mshauri wako anakudanganya.nijuacho waliomlalamikia Magufuli ni wale walionyanganywa mali za CCM,mengine ni uzushi tu.
Nikufahamishe ,kwa sasa tumeelimika,hatudanganyiki tena mkituzingua tutawazingua,
Mwisho, kama hutajali achieni taarifa ya ukaguzi wa mali za chama ,maarufu kama ripoti ya Bashiru, na ripoti yako wewe Chongolo dhidi ya Bashiru na sekretarieti yake kipindi cha Magufuli, tulinganie ni kipindi kipi chama kilifanya vizuri au vibaya ili twende sawa, lengo tufahamu ipi ni CCM makini ya kuanzia kwa Makamba, Kinana na sekretarieti zake, au ya Magufuli na Bashiru, tuna jambo tunahitaji kujifunza