CHONGOLO: Demokrasia ya kweli CCM ni kivutio cha Siasa nchini

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu,
Mbeya Jiji.

Chama Cha Mapinduzi kimesema Utulivu na uimara wa CCM ni matokeo ya kuimarika kwa demokrasia ya ndani ya chama hicho hivyo viongozi na wanachama wamesisitizwa kutotoka katika utaratibu hususani wakati chama kikielekea katika uchaguzi wa ndani.

Kimesema sababu nyingine inayoongeza imani ya CCM na kukubalika kwake na umma ni hali ya demokrasia ndani ya chama hicho kuimarika zaidi, kutoweka kwa makundi pamoja na uadilifu na uwajibikaji kupewa msukumo wa kipekee ndani na nje ya CCM.

Akihutubia mamia ya viongozi na watendaji mbalimbali wa chama na serikali katika kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Mbeya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo amesema hata ushindi wa kishindo ambao CCM iliupata katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka 2020 ni matokeo ya chama hicho kuwaletea maendeleo wananchi, kuwa wasikivu kwao na kuheshimu misingi ya haki, amani, umoja na utulivu.

"CCM ndio tumepewa dhamana ya kutoa uongozi wa nchi yetu na kuunda serikali hivyo tusikubali mambo ya hovyo yakafanyika chini ya dhamana hii tuliyopewa." Alisema Chongolo.

Chongolo amefahamisha kuwa Katika kuendelea kuhimiza umoja na mshikamano ndani ya chama hicho ni lazima wanachama wapewe nafasi ya kusikilizwa badala ya wanapotoa maoni yasiyowapendeza viongozi wakaonekana wasaliti na kutengenezewa mizengwe.

"Chama lazima kiwe kinafanya vikao na kuhakikisha vinakuwa vyenye agenda za maendeleo na sio kujadili watu, majungu au kuendeleza siasa za makundi, wakati huo huo tuhakikishe wananchi wetu wanashirikishwa na kupata majibu ya kero zinazowakabili kwani sio uungwana wao kupata majibu ya kero zinazowakabili pale tu viongozi wa kitaifa wanapowatembelea bali ni haki yao na wajibu wa lazima kwa waliopewa dhamana kufanya hivyo" alisema Chongolo.

Hata hivyo alisema wakati chama hicho kikielekea katika uchaguzi wa ndani si vyema wanachama kutengenezewa tuhuma za kupika ili wakose sifa za kuomba uongozi ndani ya chama. Jambo hilo sio sawa na chama kitakuwa makini kuhakikisha wanachama hawaonewi na haki inatendeka.

"CCM imeendelea kubaki kuwa tumaini pekee la watanzania ikiwa ni matokeo ya chama chetu kujisahihisha na kurejesha imani kubwa kwa wananchi kwa kuisimamia serikali kwa ufanisi mkubwa katika kuboresha huduma za kijamii, upatikanaji wa haki, kudhibiti vitendo vya wizi, rushwa, ufisadi, kukemea vikali matumizi mabaya ya madaraka, ulinzi wa rasilimali za nchi, kuukabili utendaji kazi wa mazoea na matumizi yenye tija kwa mapato ya serikali" alisema chongolo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na Sekretarieti yake ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wamehitimisha ziara yao katika mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya.

IMG-20210714-WA0020.jpg

IMG-20210714-WA0026.jpg

IMG-20210714-WA0024.jpg
IMG-20210714-WA0023.jpg
IMG-20210714-WA0021.jpg
 
Kama KUTUMIA Dola Kushinda UCHUGUZI ni DEMOKRASIA basi ni MAAJABU
Kama Kuogopa KATIBA MPYA ni Demokrasia basi pia ni Maajabu
 
chadema wajifunze kupitia ccm jinsi ya uongozi ndani ya chama kama kubadirishana uongozi siyo miaka nenda rudi mwenyekiti mmoja kwanza hilo ni tusi inamaana wengine wote hamjui kuongoza chama? badirikeni
 
Hii Demokrasia ya kubadilisha kura na ushindi ni kivutio cha matumb yenu.
 
Tujifunze kuiba kura au kuwatisha wakurugenzi kuwa wakiruhusu mpinzani ashinde wanaondolewa katika teuzi?
 
Hii Demokrasia ya kubadilisha kura na ushindi ni kivutio cha matumb yenu.
mtaishia majungu tu lakini ukweli mnaujuwa hivi huyo mbowe ndiyo mmemuona mwenyekiti wa kudumu? inamaana hakuna mtu mwingine anaweza kuongoza chama? nyie mkipewa madaraka ndiyo mtalazimisha kubadirisha katiba hamfai kuwa viongozi
 
Tujifunze kuiba kura au kuwatisha wakurugenzi kuwa wakiruhusu mpinzani ashinde wanaondolewa katika teuzi?
na je mbowe kuwaambia wanachama wake kuwa kujaribu kugombea uenyekiti chadema ni sawa na kuonja sumu kama alivyomwambia sumaye ndiyo democrasia yenu hiyo?
 
CHONGOLO: DEMOKRASIA YA KWELI CCM NI KIVUTIO CHA SIASA NCHINI.

Chama Cha Mapinduzi kimesema Utulivu na uimara wa CCM ni matokeo ya kuimarika kwa demokrasia ya ndani ya chama hicho hivyo viongozi na wanachama wamesisitizwa kutotoka katika utaratibu hususani wakati chama kikielekea katika uchaguzi wa ndani.

Kimesema sababu nyingine inayoongeza imani ya CCM na kukubalika kwake na umma ni hali ya demokrasia ndani ya chama hicho kuimarika zaidi, kutoweka kwa makundi pamoja na uadilifu na uwajibikaji kupewa msukumo wa kipekee ndani na nje ya CCM.

Akihutubia mamia ya viongozi na watendaji mbalimbali wa chama na serikali katika kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Mbeya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amesema ni matokeo ya chama hicho kuwaletea maendeleo wananchi, kuwa wasikivu kwao na kuheshimu misingi ya haki, amani, umoja na utulivu.

"CCM ndio tumepewa dhamana ya kutoa uongozi wa nchi yetu na kuunda serikali hivyo tusikubali mambo ya hovyo yakafanyika chini ya dhamana hii tuliyopewa." Alisema Chongolo

Chongolo amefahamisha kuwa Katika kuendelea kuhimiza umoja na mshikamano ndani ya chama hicho ni lazima wanachama wapewe nafasi ya kusikilizwa badala ya wanapotoa maoni yasiyowapendeza viongozi wakaonekana wasaliti na kutengenezewa mizengwe.

"Chama lazima kiwe kinafanya vikao na kuhakikisha vinakuwa vyenye agenda za maendeleo na sio kujadili watu, majungu au kuendeleza siasa za makundi, wakati huo huo tukumbuke wanachi wetu maana
sio uungwana wananchi kupata majibu ya kero zinazowakabili pale tu viongozi wa kitaifa wanapowatembelea bali ni haki yao na wajibu wa lazima kwa waliopewa dhamana kufanya hivyo" alisema Chongolo

Hata hivyo alisema wakati chama hicho kikielekea katika uchaguzi wa ndani Maana si vyema wanachama kutengenezewa tuhuma za kupika ili wakose sifa za kuomba uongozi ndani ya chama jambo ambalo sio sawa na chama kitakuwa makini kuhakikisha wanachama hawaonewi na haki inatendeka.

"CCM imeendelea kubaki kuwa tumaini pekee la watanzania ikiwa ni matokeo ya chama chetu kujisahihisha na kurejesha imani kubwa kwa wananchi kwa kuisimamia serikali kwa ufanisi mkubwa katika kuboresha huduma za kijamii, upatikanaji wa haki, kudhibiti vitendo vya wizi, rushwa, ufisadi, kukemea vikali matumizi mabaya ya madaraka, ulinzi wa rasilimali za nchi, kuukabili utendaji kazi wa mazoea na matumizi yenye tija kwa mapato ya serikali" alisema chongolo

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na Sekretarieti yake ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wamehitimisha ziara yao katika mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya.

photo_2021-07-14_16-15-31.jpg

photo_2021-07-14_16-15-28.jpg

photo_2021-07-14_16-15-21.jpg

photo_2021-07-14_16-15-25.jpg

photo_2021-07-14_16-15-37.jpg

photo_2021-07-14_16-15-44.jpg

photo_2021-07-14_16-15-41.jpg
 
Back
Top Bottom