Chongolo anachanja mbuga kuimarisha chama lakini Mnyika yuko ofisini anatunza mafaili, hakika CHADEMA mnafeli sana

Yaani wafuasi wa CDM wanaonekana hoi kweli kama viongozi wao duuu,, Hivi raisi Lissu anarudi lini au bado anafaili kesi ya IGP Sirro huko ICC?
Mara Amsterdam kasema ICC @#@#@, Ooh Pompeuo kasema Hakubali, tunangojea matokeo kama tungojeavyo masiha kurudi. Sasa wameamua kwenda wenyewe wameishia Space na twitter. Wakijaamua kurudi hoi ndimi nje. Wataishia "WATANZANIA HAWAJITAMBUI"
 
Mna wabunge wangapi?

Labda mioyoni mwa nyumbu
Tz kwa sasa hakuna mbunge halali hata mmoja. Ni wendawazimu kama wewe ndiyo hudhani kuna wabunge waliochaguliwa kwa uhalali. Uovu alioufanya jamaa yenu na msaidizi wake ulisababisha hata Mungu akawaondolea ulizi na leo wamebaki kuwa historia.
 
Mara Amsterdam kasema ICC @#@#@, Ooh Pompeuo kasema Hakubali, tunangojea matokeo kama tungojeavyo masiha kurudi. Sasa wameamua kwenda wenyewe wameishia Space na twitter. Wakijaamua kurudi hoi ndimi nje. Wataishia "WATANZANIA HAWAJITAMBUI"
Huko Space na Twiter wanajadili utumbo mtupu na kweli wameishiwa sana,,,lkn JPM alisema mwisho wa vyama vya upinzani umefika
Wapinzani hakuna hata siku moja waliongelea juu ya maisha wa wanyonge zaidi ya Katiba mpya na tume huru wakitegemea viwili hivyo viwape mwanya wa wao kuweza kupata ride,,, walisifia sana katiba ya Kenya wapumbavu hawa na tizama leo Kenya walivyoharibikiwa wana matatizo mengi sana kiuuongozi,,,jifunzeni kwao
 
Sasa kama nia wanayo na wanajua pia hawawezi kuwashinda hao ccm si waache siasa tuu!?

Kwanini ushindanie kitu ulichokwisha shindwa, kitu unachokiri huwezi kushinda, tena kwa njia zilezile zilizokufanya ushindwe?????
Zipo sababu za msingi sana kuendelea na mapambano, hata katika mazingira magumu kiasi gani. Mosi ni kwamba hao wakandamizaji wanabadilika, ipo tofauti kubwa kati ya Mkapa na Magufuli, na Kikwete. Pia kuna haja ya kuwaanika madhaifu yao.
Halafu binadamu tuna tofautiana. Mimi mfano, toka utotoni sipendi kabisa na ninaichukia sana DHULMA. siku zote niko against Bullies. Hata nikute mtoto mmoja anamuonea mwingine, siwezi kupita hivi hivi.

Lakini wapo ambao hayo hayana maana kubwa kwao. Hata mfano hawajiulizi hivi imekuwaje uchaguzi wa 2019 wooote nchi nzima walioenguliwa, tena kwa maelfu, ni wagombea wa vyama vya upinzani. Kwao ni sawa tu. Hawajiulizi inakuwaje ccm wanafanya mikutano watakavyo, upinzani inakuwa nongwa.

Kwa maana hiyo, ushauri wako ni kuwaachia shamba nguruwe?
 
Wakati Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongolo yuko katika ziara ya nchi nzima kuimarisha chama mwenzake J J Mnyika wa Chadema katulia tuli mtaa Ufipa halafu 2025 watalia kuibiwa kura.

Sijui CHADEMA ule ujasiri wa Dr Slaa umepotelea wapi?

Kama vipi Ukatibu mkuu apewe Ben Kigaila, yule mgogo siyo muoga.

Maendeleo hayana vyama!
Anachanja mbuga ipi? Wapi kuna mbio za marathoni huko tukaichungulie fursa
 
Back
Top Bottom