Chongoleani, Tanga: Rais Magufuli na Museveni waweka la jiwe la Msingi mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima - Tanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959


Tayari Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefika eneo la tukio. Wapo pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa.

Wapo pia viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Naibu Spika wa Bunge, Dr Tulia Ackson na mawaziri kadhaa akiwemo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dr. Medard Kalemani.

Sasa Rais Magufuli anampokea rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni na tayari wote wawili wanaingia ukumbini. Anaanza kuzungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bw. Martin Shigella ambapo anamuomba Rais kuwafikiria kuhusu suala la upanuzi wa Bandari ya Tanga.

Baada ya Mkuu wa Mkoa anakuja Naibu Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Dr. Medard Kalemani ambaye anaelezea ugumu wa kuupata mradi huu kwa Tanzania na kumpongeza Rais. Pia anatoa taarifa kuwa Tanzania bado tunatafiti uwepo wa mafuta ktk Ziwa Tanganyika na Ziwa Eyasi.

Anafuatiwa na Bi. Irene Muloni ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda ambaye anaelezea jinsi mradi utakavyonufaisha watu wa nchi za Uganda na Tanzania kwa nafasi za ajira.

Naibu waziri wa Nishati na Madini anamkaribisha ais Magufuli ambaye anawaita Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kusema machache.

Waziri Mkuu Majaliwa: Mradi huu utaongeza mzunguko wa kifedha mkoani Tanga na mikoa mingine 7 bomba litakapopita

Kinana: Hakuna Rais aliyetembelea Tanzania mara nyingi kama Museveni. Aliwahi kuja kuhamasisha matumizi ya Bandari ya Tanga

Tanzania na Uganda si nchi marafiki bali ni ndugu. Siasa ni uchumi na uchumi ni siasa.

Makamu wa Rais mama Samia: Mradi huu utasaidia maendeleo ya pamoja ya Afrika ya mashariki.

Makamu wa rais anamkaribisha rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Hotuba ya Rais Museveni



Rais Museveni: Kwa niaba ya Waganda, nawasalimia ninyi wote watu wa Uganda na watu wa Tanzania.
Najua kiswahili cha lakini Kiswahili cha kufafanua mambo ya kiuchumi kinanishinda hivyo naomba niongee kile ninyi mnachoita Kimombo.

We are here today to lay the foundation stone of Hoima-Tanga crude oil pipeline. This is the great event for two countries in East Africa.There have found also found hydrocabon in Turkana area in Kenya.

Tukichimba mafuta tutapata petrol, diesel, mafuta ya taa, mafuta ya ndege. Zile ndege za waarabu zinapata mafuta kwa bei ya chini ndio maana wanapata mafanikio makubwa.

Nimepata taarifa mmefufua kampuni yenu ya ndege naamini mtapata mafuta ya kutosha. Na sisi Uganda tutafufua kampuni yetu ya ndege hivi karibuni.

Uganda need good coal or natural gas in order to produce steel from iron ore. Tukileta haya mafuta, tunataka na bomba lingine lipande kule kuchukua gesi.

Tanzanian governement has agreed to charging no transit fees, no VAT, no corporate tax for this pipe. Ingawa bei ya mafuta duniani imeshuka kutoka $120 kwa barrow mpaka $50 kwa barrow. Kama serikali ya Tanzania wangetupa kodi zote tusingepata faida.

Sementi ya kujenga itatoka hapa, watoto wetu watafanya biashara.

East Africa is importing goods worth $33 billion per year. For the side of export East Africa is exporting goods and service worth $13.8billion. Apart from supporting good and services produced outside they don't have enough power. This natural resources will enhance building our infrastructure easly.

In my opinion East Africa especilly Uganda is unstoppable now. There is nothing to stop us from growth and transformation.

Hatutaki peasant kuzaa peasant mwingine.

Political intergration was not enough, political federation was more important.

East Africa ni kama zile nyumba zetu za kienyeji. Vitu vingi havipo katika mpangilio. Namshukuru rais Magufuli tulipokutana Kagera tulikubaliana kujenga power station at Fulgent and Mulongo.

Safari moja nilikuwa nakuja na Waziri nikaona kibao kimeandikwa Horohoro. Nikakumbuka nilipita hapa na bunduki 14. Kwahiyo nakumbuka Tanga kwa namna hiyo, najua nyie mnaikumbuka kwa mambo ya raharaha.

As Kinana remind me, we needed a railway line from Tanga to Kigoma. Ile railway hatukuweza kuikamilisha lakini bomba tumeliweza. Tukifanya mikataba yenye haki, tutafaidika sote.

Kwa hayo machache, nawashukuru kwa ukaribisho huu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Uganda.


==================

Sasa ni zamu ya Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli



=>Rais Magufuli: Mh Yoweri Kaguta museveni, makamu wa rais, waziri mkuu, naibu spika, maspika wastaafu, kaimu jaji mkuu, mawaziri wa Tanzania na Uganda, mkuu wa mkoa wa Tanga, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

=>Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi Mungu, aliyetuwezesha tuwe hapa katika siku ya leo. Siku ambayo inatangaza maendeleo ya Tanzania.

=>Napenda nimshukuru mzee wetu Yoweri Kaguta Museveni, yeye mwenyewe ameeleza hapa aliwahi kupitisha bunduki 14 kwa magendo na akirudia tena nitakutumbua.

=>Historia ya Tanga inajulikana tangu enzi za baba wa taifa mwaka 1956, wakati anadai uhuru alikuja Tanga wakamuombea. Wakafunga siku tatu na viongozi wa hapa.
Kwa hiyo alipata baraka kutoka hapa.

Neno Tanga huenda ndilo lililozaa neno Tanganyika yaani nchi yenye nyika.

=>Kuweka mradi wa bomba la mafuta lenye urefu wa kilometa 1445 ambalo litagharimu dola bilioni 3.5 sawa na trilioni 8.

=>Ndugu zangu lazima niwaambie ukweli, najua wengi walikuwa wanataka mradi huu

Katika uamuzi wa bomba hili, ilitubidi tukubali baadhi ya mambo.

=>Kwa sehemu kubwa imefanywa na wataalamu wa Uganda. Aliwaleta wengine wakawa wanasumbua.

=>Ziwa Eyasi na ziwa Tanganyika napo kuna mafuta, tukishachimba tutaunganisha kwenye bomba hili.

=>Faida ya bomba hili ni kubwa

=>Tunamthibitishia rais Museveni kuwa ulinzi ni wa uhakika.

=>Hili bomba linalojengwa ni la aina yake duniani, linasafirisha crude oil inayokuwa heated.

=>Lipo lingine India lenye urefu wa km 600, lakini haliwezi kufikia hili la Hoima hadi Tanga.

Na mimi namhakikishia akitaka gesi kutoka Mtwara, tutajenga bomba la kutoka Mtwara hadi Uganda ili kusudi wakafufue viwanda vyao.

=>Hivi karibuni tutajenga barabara toka Tanga hadi Bagamoyo 175km ambayo ipo utatekelezwa na Afrika Mashariki na na kufadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika.

=>Hili swala la bandari nitalibeba kuhusu ombi la mkuu wa mkoa wa Tanga, kuhusu kupanua bandari ya Tanga. Ili kina kiongezeke na bidhaa zishushiwe hapa na wananchi wazipate kwa bei nafuu.

=>Hili bomba limeletwa na serikali ya Magufuli na serikli ya CCM, asijitokeze mtu yeyote akasema amelileta yeye.

=>Tuna polis wa kutosha na hili bomba kwa Tanzania litapata ulinzi wa kutosha

=>Napenda kuwapongeza kampuni ya total na kampuni zote zilizopenda kuja kuwekeza katika nchi ya Uganda

=>Sioni sababu ya kusubiri miaka mitatu tukisubiri ujenzi ukamilike. Ujenzi unatakiwe uende kwa kasi.

=>Waweke sub-contractors ili kusudi waende kwa spidi inayotakiwa. Niwaomba make sure you finish this project before 2020.

=>Hili ndiyo ombi langu ambalo naamnini mzee wangi Museveni ukilisimia vizuri litakamilika.

=>Niwashukuru sana waimbaji mlioimba hapa

=>Ruge hebu njoo hapa, na Makonda njoo. Mkafanye kazi kwa ajili ya watanzania.Nendeni mkashikane mikono huko.

=>Na naamini wakati wa jiwe la msingi huko Hoima nitakuwepo.

=>Baada ya kusema hayo sasa, mimi na mzee Museveni tuko tayari kwenda kuweka jiwe la msingi.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Uganda, Mungu bariki mradi huu ukapate kukamilika kwa wakati

Nawashukuruni sana
 
Television kongwe na kubwa kuliko zote nchini ITV imetia aibu leo katika kurusha matangazo yake mubashara kutoka Tanga ukilinganisha na television zingine katika upande wa ubora wa picha.. Picha zirushwazo na ITV ni chafu na zimefifia mno zinatia aibu.. Hongera sana kwa Clouds Tv kwa kurusha picha zenye ubora wa HD na zenye mng'ao na wa hali ya juu.. Yaani hadi TBC imeizidi ITV kwa ubora wa picha za mubashara kwa leo aisee aibu sana ITv.

Sent from iphone 7 plus
 
Back
Top Bottom