Chone chonde waandishi wa habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chone chonde waandishi wa habari

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Freetown, Oct 26, 2008.

 1. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Najua ni jinsi gani Jamiiforums ilivyoweza na inavyoendelea kurekebisha mambo mengi yanayohusu maendeleo ya nchi yetu.
  Naomba tusaidiane kuwambia waandishi wa habari kutochanganya kiswahili na kingereza hasa kwenye magazeti ambayo yanasomwa na wengi ikiwa pamoja na wasiojua kiswahili. neno wananchi limekuwa likitumika sana kwenye magazeti ya kiingereza hasa Daily News.
  Angalia habari hapo chini na mtoe maoni. najua waandishi wa habari wapo wengi tu humu ndani.


  Two held in Mbeya for murdering police officer
  JONAS MWASUMBI in Mbeya
  Daily News; Sunday,October 26, 2008 @00:
  Police here are holding two Nyalwela villagers in Mbeya District for allegedly hacking to death a police corporal, Renatus John (50) who was on duty at the Katavi National Park in Makete district, Iringa Region last Tuesday
  Mbeya Regional Police Commander, Mr Zelothe Stephen said yesterday that the two villagers Nyamba Ndosi and Petrol Ndefeti, aged 19 and 20 years old respectively, were arrested the same day, following an intensive manhunt mounted by police in collaboration with wananchi.

  During the manhunt, the suspects were found in possession of a sub-machine gun previously used by the allegedly killed policeman. Mr Stephen said the late John who was a driver was on that material day on duty together with the Tanzania National Parks (TANAPA) game scouts who during the killing had gone inside the national park to arrest pastoralists whose cattle and other livestock were grazing in the national park.

  He said after arresting the pastoralists, the TANAPA game scouts could no longer reach the police driver through his cellular phone. The deceased was later found hacked to death by sharp objects and the SMG he had been having was missing. The village government and the police in concert immediately launched a manhunt for the suspects.

  Mr Stephen said it was during the search that the two men were arrested while in possession of the SMG property of TANAPA. The two were also found with 28 rounds of ammunition and a handset that was said to belong to the deceased. The suspects would soon appear before the court to answer murder charges, Mr Stephen said.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nadhani wanalitumia neno hili wakiamini kuwqa wasomaji wao wengi wnaielewa maana yake
   
 3. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  neno wananchi / mwananchi liendelee kutumika kwenye magazeti ya kimombo maana wengi wetu ni wa-swa-nglishi.

  Chonde chonde waandishi wa habari
   
 4. kkiwango

  kkiwango Senior Member

  #4
  Oct 26, 2008
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  What is wrong wakichanganya? is it an international news paper or local? mi naona ni sawa tu endapo walengwa wa habari wanaelewa.
   
 5. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Kuna Kiingereza cha East Africa chenye maneno kama hayo, mfano Safari, Shamba, na sasa Wananchi. Ni lugha au tabia ya kawaida.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,562
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Huo ni msisitizo kama alivyoitwa Mwalimu Nyerere, hakuwahi kuitwa Teacher Nyerere. Yapo maneno mengi ya kiswahili yanatumika hivyo hivyo kwenye Kiingereza kama Mzee, Alhaji, Mkukuta, Mkumbita, Mkurabita etc. Pia yapo maneno mengi ya kiingereza yanatumika hivyo hivyo kwenye kiswahili kama propaganda, sekretarieti , milenia, etc.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hilo sina tatizo nalo kwa sababu lugha nyingine nyingi tu zinatumia maneno ya lugha nyingine pale mtumiaji anapotaka kuweka msisitizo au kwa kuwa hadhira yake imezoea kutumia maneno hayo. Mfano yako maneno mengi sana ya kiratini kwenye kiingereza na hakuna tatizo hapo.

  Shida yangu kubwa ni pale ambapo mtumiaji (hata humu kwenye JF) anaamua kuchanganya lugha kijinga jinga. Mfano, mtu anaandika ua kuongea maneno 4 ya kiswahili, 2 kiingereza, 1 kifaransa, 3 kiratini n.k. Sasa hapo ndipo inapoonekana mtumiaji hajui hata lugha yoyote kati ya hizo. Anaongea tu kila neno linalokuja kichwani mwake! Ni uzumbukuku tu,...... na viongozi wetu wakiwamo wabunge ni wahanga wakubwa wa hili tatizo.
   
 8. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  I do that most of the time; Ila si kwa makusudi. Call me whatever you want, that is OK :)
  Naamini wataalamu wa lugha wanaweza kulitolea maelezo suala hili kueleza nini kinapelekea mtu kuchanganya lugha.

  Hata hivyo, huwa navutiwa sana pale watu wanapotumia maneno ya kiswahili kwa ufasaha hasa yale ambayo nimesahau kabisa kwamba yapo.

  Kuna misamiati ya kiswahili ambayo naifahamu lakini haipo kwenye kumbukumbu niweze kuitumia kwa haraka.
  Mfano: chutama, kwayo, akisi, bobea, zuzu, asilani....  .  .
   
 9. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  The only justification of using the word "wananchi" should be derived from the English language not having a sufficiently equivalent word.In essence the journalists are rejecting the usage of "the people" as inaccurate, whether from a sentimentality point of view or purely a semantic / etimology or political science.

  An example is the use of the word "safari" in English, the world over the word "safari" is used in English because it is agreed that there is no single word that is as desriptive in the context of a game hunting expedition.

  Although I disagree with the use of wananchi in such a context, as "the people" can adequately do, I feel journalists feel especially accurate when using "wananchi" just as they do when using "bunge" instead of parliament and "Ikulu" instead of state house.

  This is why the Israeli parliament is refered as the Knesset, the Russian one the Duma etc.The use of these specifically descriptive words carry a special characteristic that is only present in the context of the country in question, like the Israeli Knesset has some distictly Israeli characteristics just as the Russian Duma has some distinctly Russian characteristics, the Tanzanian People, "wananchi", have some distinctly Tanzanian characteristics that the word "the people" would not do justice in describing just as the word parliament would not do justice to accurately describe some inherrently Russian characteristics of the Duma ditto to Knesset and Bunge.
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Ila mkuu sio siri unaandikaga kingereza kigumu sana mpaka maana inapotea jaribu kuandika lugha rahisi ili ujumbe ufike.
   
 11. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona cha kujifunzia ukubwani tu hiki? Kuna hadhira fulani ya kimataifa inafuatilia pia, kwa faida yake naandika lugha inayoifurahia. Isitoshe nimeambiwa hata kiswahili naandika kigumu pia, ni suala la msomaji.Nitajaribu kunyumbulisha kirahisi chini hapa.

  Kwa kifupi nimeunga mkono wakuu waliosema kuwa swala zima la lugha kutohoa maneno kutoka lugha nyingine si geni, ikiwa ni kwa sababu hamna neno linalofaa kutoka lugha tohoaji au kwa sababu ya ulimbwende na mikogo tu.Ukitazama historia ya lugha zote za Ulaya, ambazo nyingi ni za nasaba ya "Indo-European" utaona zilivyotoka katika Sanskrit mpaka kilatini cha kale na jinsi gani miziz hii imeweka misngi ya lugha za mkondo wa Kijerumani / Anglo-Saxon kama vile Kiingereza.Muongozo wa waandishi wa gazeti linaloheshimika Uingereza "The Economist" unashauri kutumia maneno mafupi na rahisi ambayo yana mizizi katika kiingereza halisi zaidi ya yale marefu yanayotokana na kilatini, lakini lugha ziankua na hili swala hata hawa wa "The Economist", zaidi ya kuleta ulimbwende wa kibwanyenye hawawezi kulizuia.

  Kwa mfano waingereza, ambao hawajui mambo ya hoteli na kupika kama Wafaransa, mpaka leo wanatumia neno la kifaransa maitre'd kumtaja yule mtu anayeongoza kuwapangia meza wateja katika hoteli kubwa, waingereza wanaweza kutumia maneno mengi, lakini kutumia "head waiter" inakuwa haina mikogo kama "maitre'd" inaweza hata kuchangia muonekano mzima wa hoteli na kufanya watu walipe zaidi kwenye hoteli yenye "maitre'd" ukilinganisha na hoteli yenye "head waiter".Kwa hiyo mara nyingine sababu zinaendana na historia nzima ya mizizi ya maneno haya (etimology) ukijua kusoma "katikati ya mistari" neno moja la kutohoa linaweza kukupa picha ambayo ingebidi kutumia kifungu kizima cha maneno kulielezea.Mifano ni mingi, lakini ukishaambiwa "wananchi" unajua muandishi anaongelea habari katika minajili ya kijamaa na aghalabu atakuwa yuko upande wa wananchi hao.

  Vivyo hivyo, maneno kama "safari" "khaki" na mengine mengi yameingia katika kiingereza ama kwa kuwa hakuna maneno ya kiingereza yaliyo sawa nayo, au kwa sababu ya ulimbwende tu.

  Ukiangalia neno mwananchi linavyotumiwa katika kiingereza cha magazeti yetu linatumiwa kisiasa zaidi, katika mustakabali wa watu wa nchi ya ujamaa na kujitegemea.Na ukiangalia sana utaona wanaoandika hivyo sana ni watu wa propaganda za serikali -Daily News- kwa sababu wanajua uzalendo unatoweka na dhana nzima ya uananchi inatoweka, kwa hiyo katika kutapatapa kwa mfamaji wanaishia kutaka kuweka uzalendo kwa kupika kwa kutumia maneno kama "wananchi" sehemu ambayo wangeweza kutumia "the people"

  Kuhusu hapa bodini, kwa kuwa hii bodi si mimbari rasmi, watu wana uhuru wa kutumia lugha kisanii kwa jinsi wanavyotaka, ikiwa ni pamoja na kuchanganya lugha mbili au hata kuweka kiswahili kisicho rasmi. Tumesema kwamba wanaochanganya kiswahili na kiingereza hawajui kiswahili wala kiingereza, vipi kama ni kweli hawajui kiswahili wala kiingereza na inabidi wachanganye ili kujieleza, tutawazuia wasijieleze?
   
 12. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 60
  Niliposoma tu jina la thread hii "chonde chonde waandishi wa habari" hakika taswira iliyojitokeza haraka ni kwamba mwandishi anatahadharisha jambo fulani kwa waandishi ambapo wakiachwa waendelee nalo basi pengine kuna janga linjiani, baada ya kuisoma hoja na uchangiaji nimepata taswira nyingine tofauti na iliyotangulia.
  Kwanza napingana na tahadhari hiyo ajili haistahili kwani hakuna janga lijalo kutokana na matumizi ya kiswahili ndani ya makala za kiingereza kwani kwanza hutumika vizuri pia ni njia ya kukiuza kiswahili, endapo makala hiyo itasomwa na asie mswahili itamlazimu kuitafuta maana ya msamiati huo na hivyo kujifunza jambo katika kiswahili ikawa ndio mwanzo wa kujifunza na kukijua kiswahili.
  ningepinga kama tahadhari hiyo ingekuwa ni kinyume, kwamba Makala ya kiswahili yakatumiwa maneno ya kiingereza pahala ambapo neno zuri la kiswahili lipo na linaeleweka na wengi halafu mwandishi akaazima neno jingine pengine hata halileti maana nzuri zaidi ya lile la kiswahili.

  Tukienzi kiswahili lugha yetu adhimu.
   
Loading...