Chonde wanasisa, tamaa na ubinafsi wenu ni mauti kwetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chonde wanasisa, tamaa na ubinafsi wenu ni mauti kwetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chatumkali, Jan 30, 2012.

 1. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Juzi nililazimika kumsidikiza rafiki yangu ambae alimpeleka mtoto wake wa miaka minne ambae alimeza pini ya kubania karatasi.Katika hospitari ya rufaa ya mkoa wa Dodoma hakupata huduma kutokana na mgomo wa madaktari.Pale nlikutana na mgonjwa<kijana wa kama miaka 32 hivi>Baada ya kumtaka maoni yake kuhusu mgomo,lawama alizimimina kwa Spika Makinda kama ni "imediate cause" ya mgomo wa madaktari.Alidai madaktari pamoja na kuwa na madai ya msingi ya muda mrefu,waliendelea kuwa wavumilivu.Ni tamko la kitamaa la spika Makinda la kutaka kuhalalisha posho mpya ya wabunge ndilo lililotifua nyongo ya madaktari na wao kuona waanze kudai haki zao kwa mtindo huu.Kijana anaamini kwamba bila lile tamko la posho ya wabunge mgomo huu ambao umemuacha akiwa wodini kwa siku nne bila tiba usingekuwepo. Baada ya kuyatafakari kidogo maoni yake,nikaona yana ukweli ndani yake.Na hapo ndipo nilipokuja kutambua ubaya wa ubinafsi na tamaa za wanasiasa!Chonde akina Makinda maana tamaa,ulafi,uchoyo na ubinafsi wenu ni MAUTI kwetu.
   
 2. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tawile!
   
Loading...