Chonde chonde, watumishi hewa na vyeti fake mtuokoe tafadhalini

Jan 13, 2017
67
49
Ni muda wa miaka miwili umepita kuanzia nihitimu chuo na baada ya hapo suala la ajira limekuwa mtihani kwa yalifuatia matamko mfululizo kuhusu kushitishwa ajira.

Basi nikaamua kupambana kivingine ila mtaani channel zinabana sana faraja ilikuja pale rais aliposema ataajiri atakapowaondoa wenye vyeti fake ila kwa hali ilivyo kama vile wanatoka taratibu tena kwa kulaumu na kulaani.

Jamani kumbuke tayari mna mikopo na mitaji kutokana na mishahara yenu, ni muda wenu kuutumia ule ushauri mliokuwa mnatupatia eti tukajiajiri, haya hima mkajiajiri maana mvua zinaelekea kukata.

Kumbukeni kufa kufaana.
 
Mtuachie Na Sisi Tuonje Hiyo National Cake,,,, Na sisi tutafute mitaji tukajiajiri na ili baadae sisi pia tuwaachie wadogo zetu wafaidi,,,,,
 
Ni Muda Wa Miaka Miwili Umepita Kuanzia Nihitimu Chuo Na baada ya hapo suala la ajira limekuwa mtiani kwa yalifuatia matamko mfururizo kuhusu kushitishwa ajira , basi nikaamua kupambana kivingine ila mtaani channel zinabana sana,,,,, faraja ilikuja pale Rais aliposema ataajir atakapo waondoa wenye vyeti fake ila kwa hali ilivyo kama vile wanatoka taratibu tena kwa kulaum na kulaan,,,\,,, Jamani Kumbuke Tayari Mna Mikopo Na Mitaji Kutokana Na Mishahara Yenu,,, Ni Muda Wenu Kuutumia Ule Ushauri Mliokuwa Mnatupatia Eti \,,{TUKAJIAJIRI},, haya hima mkajiajir maana mvua zinaelekea kukata .. Kumbukeni KUFA KUFAANA ,
Mkuu unasaka ajira huku hata kuandika kunakushinda.Mm,haya bwana.
 
Ni Muda Wa Miaka Miwili Umepita Kuanzia Nihitimu Chuo Na baada ya hapo suala la ajira limekuwa mtiani kwa yalifuatia matamko mfururizo kuhusu kushitishwa ajira , basi nikaamua kupambana kivingine ila mtaani channel zinabana sana,,,,, faraja ilikuja pale Rais aliposema ataajir atakapo waondoa wenye vyeti fake ila kwa hali ilivyo kama vile wanatoka taratibu tena kwa kulaum na kulaan,,,\,,, Jamani Kumbuke Tayari Mna Mikopo Na Mitaji Kutokana Na Mishahara Yenu,,, Ni Muda Wenu Kuutumia Ule Ushauri Mliokuwa Mnatupatia Eti \,,{TUKAJIAJIRI},, haya hima mkajiajir maana mvua zinaelekea kukata .. Kumbukeni KUFA KUFAANA ,

.......mtiani ....... mfururizo...... ataajir. Mkuu umemalizia chuo gani? pole sana
 
  • Thanks
Reactions: SDG
hawa vijana wanaokaa makwao wanasumbua na mtakoma zimetangazwa nafasi 15,000 na huwez juwa wakachukuwa buku tu hawasomeki skuiz
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwa uandishi huo..mmmhhh ukipewa written exam wewe ushafeli interview AM TELLING YOU...
Usaili wa Serikali wa kuandika..siku hizi nasikia maswali yake...maana zamani watu waliingia direct kutoka vyuoni.

.Zitaje wizara zote na mawaziri wake.

Andika Wimbo wa Taifa.

Tanzania imepakana na nchi ngapi? Zitaje
 
Duuuh
 
Nimejikuta natafakari kwanza jina la mleta uzi kisha ndio nikaanza kuchambua mada kama komedi flan hivi au kufa kufaana kiukweli hali ni mbaya kwa yaliyo wakuta wahanga wa kadhia hii
 
Kama wewe ni mhitimu wa shahada au stashahada basi ulikuwa huzingatii masomo ya lugha.
Kwa kifupi Magufuli hana mpango wa kuwafurahisha wasomi kwa kuwaajiri au kuwalipa mshahara mnono.
Lishike hilo, lisije kukupokonyoka.
 
Back
Top Bottom