G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Marehemu Idd nimethibitisha kuwa alikuwa akifuatiliwa na serikali kwa muda wa wiki mbili kwa kudaiwa kuonana na muathirika wa COVID 19 aliyetoka nje ya nchi. Cha ajabu marehemu alishindikana kupatikana mbali na kuwa alikuwa ndani ya jiji la Dar tena akifanya shughuli zake kama kawaida.
Marehemu kabla ya kufariki mwanzoni mwa wiki, wiki iliyopita siku ya alhamisi mchana alitinga ndani ya bohari kuu ya madawa MSD na kujinunulia sanitizer za kutosha kwa ajili ya kuzisambaza. Mbaya zaidi marehemu alikuwa akiugua mafua muda huo. (Tunaambiwa kuwa wafanyakazi wa MSD walioonana na marehemu tayari wametengwa lakini ni baada ya kusambaa taarifa za kifo cha Idd)
Weekend yote kabla ya kuzidiwa siku ya jumapili usiku Idd alikuwa akila bata kwenye baa kadhaa ndani ya viunga vya Tabata, pia tayari alishapita zahanati kutokana na mafua yaliyokuwa yakimkabili.
Idd alipelekwa Aghakan akiwa kazidiwa na ndipo alipopimwa Corona na kukutwa positive. Wakati taarifa zake zinapelekwa serikalini ili ahamishwe ndipo serikali nayo ikagutuka eti walikuwa wakimfuatilia! Too late!
Tukicheza tutaisha! Serikali inaonyesha udhaifu mkubwa. Mtu katoroka karantini kaenda kukamatwa Iringa tena akiwa ameshaishi na wenyeji siku zaidi ya nne! Huko Mbeya watu 80 wametoroka South Afrika wameingia mpaka katikati ya jiji kwa basi ndipo wanagutuka! Chonde chonde. Serikali lazima izibe mipaka kati ya mikoa na ile ya kimataifa! Tusijifanye hamnazo! Tutajimaliza aslani!