Chonde chonde watanzania nipo chini ya miguu yenu 2015 tusichague tena rais limbukeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chonde chonde watanzania nipo chini ya miguu yenu 2015 tusichague tena rais limbukeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Mar 22, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,
  Mojawapo ya udhaifu wa kiongozi wetu wa sasa ni kitu tunachoita ulimbukeni. Kwa wasio wachunguzi wa mambo ni vigumu kuamini nachosema. Lakini rais wetu ni limbukeni tena haswa. Anajisikia, analinga na kwa lugha ya wenzetu akina dada anajishaua. Kwa sisi tuliobahatika kuwa karibu nae, tunamfahamu. Tabia yake hiyo ni 'unique', inamtofautisha sana na marais waliopita. Ni limbukeni ambaye urais kwake ni fahari na ndiyo maana pamoja na gharama yake kubwa, safari za nje haziishi. Ebu fikiria kiongozi wa nchi akiwa kwenye ziara za kiserikali katika nchi ya kigeni anapataje muda wa kubembea na mkewe kama watoto wa chekechekea na mbaya anakubali hata kupigwa picha!!! Hata iweje, Mzee Mkapa hawezi kufanya jambo hilo kamwe.

  Ndiyo maana nasema tatizo ni ulimbukeni, upenda majivuno, kujisikia na ku-pretend kujua kila kitu. Anapokuwa anajadiliana na surbodinates hujifanya kila kitu anajua. Kwa tabia hiyo, anakosa mawazo mengi mazuri kutoka kwa wasaidizi wake. Kuna rafiki yangu mmoja ambaye mpaka sasa bado ni waziri aliwahi kuniambia kwamba wanapokuwa kwenye vikao vya baraza la mawaziri ambavyo yeye huwa ndiye mwenyekiti, huwa wanakuwa na fursa finyu sana ya kuchangia mawazo yao hata kama suala linalojadiliwa linahusu sekta fulani ambayo waziri wake yupo. Muda mwingi anaongea mwenyekiti tena basi bora hata maongezi yenyewe yangekuwa ya maana. Huyo waziri anasema walikuwa wanamfurahia sana Dr. Shein anapoachiwa uenyekiti wa kikao kwani yeye hakuwa mwongeaji sana na alikuwa anatoa fursa kwa waziri mwenye sekta kuelezea jambo na kutoa mapendekezo yake. Na walikuwa wanatumia muda mfupi zaidi kujadilia masuala mengi na ya msingi.

  Ndugu zangu rais wetu ana udhaifu mwingi lakini huu wa ulimbukeni nao umechangia kuyumba kwa nchi yetu kiuongozi. Wito wangu kwenu ni kama kichwa cha thread hii kinavyosema 'tusidiriki tena kuchagua kiongozi mwenye tabia ya ulimbukeni'. Badala ya kukaa na kufikiria matatizo ya wananchi na namna ya kuyatatua, yeye atakuwa anafikiria ni suti ipi atakayovaa kesho kwenye hafla fulani au atembelee nchi gani (kwa kisingizio cha kuomba misaada). Tukifanya hivyo, tutaliwa tena.
   
 2. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sawa mkuu nimekuelewa ila naomba ujibu swali langu;Utamjuaje mgombea si limbukeni?Watu wana tabia kubadilika wanapopata madaraka,je hilo wananchi watazuiaje mtu asibadilike?Nauliza hivyo kwa sababu pengine wote waliomchagua JK wanaamini hana hiyo sifa ya ulimbukeni na kutokukubali ushauri.
   
 3. P

  Percival JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Uongozi unaonekana kwa mambo matatu muhimu :

  1) Uchumi - Data zinaonshesha Tanzania inapanda
  2) Afya na Elimu - Huduma za matibabu zinaongezeka, Elimu - mashule na vyuo vinaongezeka na watu wengi sasa wanapata elimu ya sekondari na wengine wanaendelea vyuoni
  3) Usalama - Tanzania bado inajulikana kuwa nchi yenye usalama

  Kitu kingine ambacho kitachakua muda ni kupambana na ufisadi. Ufisadi wa ngazi za juu nadhani utaisha miaka karibuni ijayo sababu ya uwazi na uhuru wa vyombo vya habari.
   
 4. c

  cancerian Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtu mwenye busara huwa anasikiliza zaidi ya maneno machache anayoongea
   
 5. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Mtu limbukeni kumtambua ni ngumu kidogo japo baadhi wanajidhihirisha kama akina Lazaro Nyarandu. Kimsingi, makibaliana na mleta hoja. Rais mpenda starehe hawezi kujali shida za wananchi.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kumgundua kimbukeni ni raisi sana wakuu!
  JK alionekana limbukeni na chekbob toka zamani saana sema MITANDAO ilimbeba saana!
  hv kwa mtu kama MEMBE unategemea maendeleo kweli!?
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Na Loliondo usisahau ni sera ya CCM kuwezesha waganga na wachawi
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kumbe ni sera ya ccm!! Sikuwa najua jambo hilo!! Ndiyo maana hata mkuu wa nchi ana uhusiano mzuri na shekhe yahaya.
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  Mzee hoja yako ni nzuri ila sahihisha usemi wako ondoa ile "kuwa chini ya miguu yetu" sisi wengine makabila yetu hiyo ni dharau au tusi.

  Ukimaliza kutuomba radhi then tuendelee kujadili hoja yako.
   
 10. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mkuu sisi wa 2010s,hatujakuelewa,sisi hatujui maana ya Limbukeni. Au linafanana na 'sharobaro' au ndo brazamen?au tozi? Kwa iyo rais ni Sharobaro? Ebu weka sawa ili nasi tuelewe mana Lugha jamani ngumu. Anyway kama sitakuwa mbali na mada nivumilie mi nadhani tuelekeze nguvu zetu kwa watu wenye akili nzuri na afya njema pamoja na hekima. Kuna mtawala mmoja nimenukuu semi zake chache ambazo hata mwl.wa std5 anaweza kuogopa kuzitamka mbele ya darasa,mfano: 1. akili ya kuambiwa changanya na yako,ni mtaala gani unafundisha kugereza?au kuchanganya akili? 2. Walimu wakigoma tutatumia hata silaha za moto kuwatuliza. Ivi ndo suluhu ya mgomo?Leo sa7,nimepita s/m Hananasifu sijaamini macho yangu,yani walimu wamekuja na mifuko ya nailon wanachambua mchicha wakati pembeni kuna rundo la daftari za mazoezi ya wanafunzi mwingne wanasukana nywele na mmoja anapinda kanga kwa mkona,ofisi nzima ni kioja-siwalaumu ila je rais alifuta mgomo?au anadhan mgomo ni kufunga barabara?. Nilienda shule ya Sekondari Rukindo,Muleba,wanafunzi wa kidato cha tatu wakanijia nilipofikia kwa ndugu yangu eti niwasaidie hesabu na kemia kwa kuwa walimu wapo ofisini ila hawafiki darasani,eti tangu january wamewaona walimu watatu nao wamekuja si zaidi ya mara tano tangu january. Unaweza kuona kama adithi ivi ila je hapa rais alifuta migomo au aliwaraisishia njia? 3. Wanaopata mimba mashuleni wana vihelehele. Ni kauli ya mtawala. 4. Ukitaka kula lazima uliwe,unataka kula bila kuliwa?Haiwezekani!! Pia ni kauli ya mtawala. 5. Sijui kwa nini watanzania ni maskini. 6.Ukiona msongamano wa magari dar,ujue watanzania ni matajiri na wana maisha bora. 7. Kumchagua Tundu Lissu kuwa mbunge ni heri mumchague Dr.Slaa awe rais-mtawala akimwogopa raia wake kama ukoma! 8. Mkewe akaongeza: wanafunzi wakatae mafataki,msifanye ngono,mkimaliza shule mtafanya mpaka mchoke! Ni kauli ya ubavu wa mtawala. Waziri wake,sofia akamalizie-WANAUME wakienda kwenye maandano ya wapinzan wakirudi tusiwape unyumba! Je hapo kuna mtawala? Kwa kweli kuchagua watu wa upeo huu kutuongoza ni dhambi kubwa! Nadhani mleta mada alitaka afike huku ila muda na karatasi vikaisha. Kweli ulimbukeni ni ujinga!
   
 11. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #11
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45

  Uchumi Unakua Ikulu na Kwa Mafisadi wanaoporomosha Magorofa?? Umewahi Kufika Nagaga Masasi, Kilimarondo huko Lindi ambako Nyumba za Makuti yaliyozeeka, na madirisha mengimengi inayotumiwa na wananchi Maskini ambao RAIS anawaambia 'Ichukieni Chadema ..na Muuzoee Umasikini Wenu'????
  Afya Inakua ,Unaongelea Loliondo ambako watu wanakimbilia baada ya kukata Tamaa kwa Huduma Mbovu Mahospitalini? Afya Inakuwa Pale Dispensary zinakosa Dawa Kwa zaiodi ya Miezi miwili huko Vijijini?
  Elimu Inakua kwa Wanafunzi wengi wa Shule za serikali Kufeli na Kuishia kwenye Biashara ya Daladala za Baiskeli Huko Shinyanga?

  Amani Gani inakuwa kwa Umasikini? Unajua maana ya 'Peace of Mind'? Unategemea Mtu atakuwa Maskini awe na Peace of Mind?? Je Akikata tamaa amani itakuwepo??. Kuna Amani wakati Wananchi wanavamia Mashamba Ya Vigogo na kugawana? Wanachoma na kuharibu Mashamba ya Wawekezaji??? Migogoro ya Umiliki wa ardhi Mabondeni je?

  Kama kila siku unashinda ndani ya Ghorofa Lako lenye Kiyoyozi Unaangalia na Kusikiliza Radio na TV za nje kama DSTV, DEUTCHE Welle, BBC,Sky News n.k? Badala ya Kusikiliza TBC Fm ya Lindi, Sfari Fm ya Mtwara, Aboud ya Morogoro, Victoria ya Mara Utajuaje Kinachoendelea Nchini mwako...NDIYO MAANA UNALOPOKA TU ATI UCHUMI UMEKUA! Kaa Kimya!!!!!
   
Loading...