Chonde chonde tusifike huku watanzania wenzangu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chonde chonde tusifike huku watanzania wenzangu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Jan 15, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Sunday, January 15, 2012

  MWANA-CCM ALIYEMWAGIWA TINDIKALI IGUNGA AREJEA NCHINI BAADA YA MATIBABU INDIA  [​IMG]
  MKAZI wa Igunga, Kada wa CCM, Mussa Tesha aliyekuwa katika matibabu nchini India baada ya kumwagiwa tindikali usoni na watu wanaodaiwa kuwa wa CHADAEMA, wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo mwaka jana, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, baada ya kurejea nchini.
  Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM jimboni humo.

  [​IMG]

  Na Mwandishi Wetu


  KADA wa CCM, mkazi wa Igunga, Tabora, Mussa Tesha (24)aliyekuwa akipatiwa matibabu India, baada ya kuwagia tindikali na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema wakati wa kampeni za uchagfuzi mdogo jimboni humo mwaka jana, amerejea nchini.

  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba alisema leo kwamba, Tesha amerejea juzi, akiwa amepona kiasi cha kuweza kuzungumza na kuona jicho moja huku lingine likiwa bado halioni vizuri kutokana na athari alizopata.

  Akizungumza nyumbani kwake Tegeta Mwisho, Dar es Salaam, Mwigulu ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM Igunga, alisema amemhifadhi Tesha nyumbani kwake wakati akisubiri kwenda tena India kuendelea kuendelea na matibabu madogo yaliyosalia.

  Mwigulu alisema, Chama Cha Mapinduzi ambacho kiligharamia matibabu yote, hadi sasa kinaendelea kumhudumia Tesha mpaka atakapopona kabisa na kuwa na uwezo wa kufanya kazi.

  "Hadi sasa tunashukuru kwamba amepona anaweza kuzungumza, kusikia na kuona walau jicho moja, tofauti na mwanzo alivyokuwa mara alipomwagiwa tindikali, hata hivyo hali yake haijaweza kuwa ya kufanya kazi mbalimbali kama za juani, hivyo CCM tunaendelea kumsaidia mpaka ajenge uwezo wa kujitegemea", alisema.

  Alisema, CCM imefanya mpango wa kuwaugnanisha wabunge wa CCM kumtayarishia mtaji ambao utamsaidia Tesha kuendesha maisha yake baada ya kukumbwa na madhara hayo.

  Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu amwagiwe tindikali, Tesha amewashukuru Watanzania kwa kumuombea wakati wote alipokuwa mgonjwa na kwamba anaamini dua zao ndizo zimemwezesha kubakia hai hadi sasa.

  Tesha alisema, baada ya kumwagiwa tindikali Septemba 9, mwaka jana, hakujitambua hadi alipokuwa katika hospitali ya KCMC ambako alipatiwa matibabu na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikaa wiki tatu kabla ya kupelekwa India.

  Akiwa India kwenye Hospitali ya Apollo, Tesha alikuwa chini ya uangalizi wa baba yake mdogo, Samwel Bethwel ambaye pia gharama za kuwa huko zimebebwa na CCM. Anatarajia kwenda tena India baada ya miezi mitatu.

   
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Habari mbaya na ya kusikitisha sana.
  Lakini ukiangalia CHADEMA TV wanasema ni CCM wenyewe walifanyiana unyama huu kwa kuzikana posho. Inasemekana ni wenzake wa CCM ndio walimfanyia maovu haya.
  Kumtibu huyu ndugu yetu India na kumlipia gharama zingine ni nusu ya haki anayostahili, nusu nyingine ni kuwafikisha mbele ya sheria wahusika bila kujali wanatoka chama gani.
  Kwa bahati mbaya sana dalili zote zinaonyesha huko ndiko tunakoelekea
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Siasa za maji taka at work...!
   
 4. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hi c nzuri kabisa na ikemewe kwa nguvu zote! tusifike huku jamani
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ingekua ni chadema wamemmwagia ungekuta wameshakamatwa, fungua akili baba huo ni mchezo wao wenyewe, unakumbuka huko huko igunga walichoma nyumba halafu wakaacha barua eti " NI SISI CHADEMA" kweli inakuingia akilini kuwa kweli ni chadema au ni siasa za maji taka za kubabikiziana kesi?, vipi ile kesi ya dc igunga kuvuliwa ushungi na matamko kibbao misikitini,yameishia wapi? CCM NA WASHIRIKA WAO WAACHE KUFANYA MAMBO YA KINYAMA KWA UCHU WA MADARAKA NA WAACHE KUCHEZEA HELA ZETU KUFIDIA MAOVU YAO.
   
 6. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni mbaya sana. Nafikiri dawa yake tunayo. Tuache kufanya siasa kuwa ajira. Kwa mfano ikiwa wabunge watakuwa hawalipwi posho na wala kupewa nafasi za kuwa Mawaziri au wajumbe wa bodi za wakurugenzi ambako kinachowavutia wengi ni marupurupu mazito haya mapambano ya kulishana sumu, kumwagiwa tindikali na kuendelea yatapungua na hata kutoweka. Mbunge mpya wa huko Igunga Peter toa fedha ulizojilimbikizia muda mfupi ulipokuwa kamishina wa madini kumtibu huyu kijana and may be apewe fidia kwa maisha yake yote. As long as ubunge na udiwani unampeleka mtu kwenye ufalme na kuukata. Ndio maana utaona mbio za kukimbilia Dodoma mjengoni kupata utajiri!:A S 465:
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  CCM acheni umafia mnamalizana wenyewe Mwakyembe mmemfanyaje huyu naye mmemfanyaje,
  Mwigulu asijifanye kumuonea huruma leo, anajua kila kitu.
   
 8. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Lakini wanasema ni wafuasi wa chadema ndio wanahusika na siasa hizi za kishenzi....kama kweli cdm ndugu zangu tubadilike hii sio siasa hivi ni vita!Katika hali ya kawaida ccm wasingeweza kumuumiza kada hadharani,wanao umafia lakini sio huu wa hadharani,hii wamefanya wapinzani wa ccm tu,kama c chadema basi ni nccr ama cuf,huo ndio ukweli tuache upotoshaji kwenye mabo serious!
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kardash naona uchama umekaa sana hadi fikra zako zimekuwa fupi.
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ah wapi, ccm wanauwezo wa kufanya lolote ili washinde, lengo la kumwagia tindikali kada wao ni kuwahamasisha watu wasiichague chadema kuwa ni wauaji, hapo hapo igunga ccm waliua wafuasi wa chadema na miili yao kupatikana baada ya uchaguzi.
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Waache kuzikana posho za wizi, mchezo wa kumwagiana tindikali utaisha.
   
 12. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwanini kakaangu?lakini bora uchama kama ni kweli lakini kuliko udini na ukabila,chama ni kama koti tu ukiona linakubana unalivua..
   
 13. s

  sitakuwafisadi Member

  #13
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  inahuzunisha sana lakini mbona............ dhuluma mauaji ftna na kila aina ya udhalilishaji VIPO NDANI YA CCM .........hebu watwambie kilicho muua DAUDI balali KILICHOMUUA ...sokoine.............kigoma malima na kinacho muangamiza........ MWAKYEMBE NA MWANDOSYA....ccm ndio serekali ccm ndio polisi ccm ndio usalama wa taifa MBONA watuhumiwa wa mauaji ya Gnr kombe wameachiwa alie waachia nani !!.........CCM ACHENI PROPOGANDA.........acheni kuuana.......hii sio siasa!!
   
 14. T

  TUMY JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vijana tumekuwa tukitumiwa na watu katika kufanikisha malengo yao, kisha wakishafanikiwa wanasepa zao, hilo ndilo tatizo letu kubwa.
   
 15. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ukiangalia mazingira ya nchi hii jeshi la polisi linavyotumiwa na CCM hao waliommwagia watakuwwa ni CCM kwani wangekuwa chadema wangetiwa ndani siku nyingi na dhamana wasingipewa
   
 16. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama CHADEMA wangefanya unyama huu sasa hivi wahalifu wangekuwa wanasota rumande. hebu watanzania tuwe na akili, lini CHADEMA alifanya uhalifu halafu polisi wasiwafikishe mahakamani? Nakubaliana kabisa kuwa ccm wenyewe ndo waliofanya unyama huo. mungu awalaani
   
 17. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  CDM ilistahili kufutwa kwa kitendo hiki.
  Amkeni watanzania.
  OTIS
   
 18. M

  Msharika JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wlimwagiana tindikali wakigombea posho, posho ni za CCM, CDM inausikaje hapo?
   
 19. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Inasemekana kuwa aliwadhulumu wenzake pesa ya mgao walio pewa kwa kuondoa mabango ya chadema, wakamshughulikia. Wasisingizie Chadema
   
 20. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pole sana!!
  hao hao chadema wamemlisha sumu Mwakyembe; hao hao chadema walimshughulikia kolimba; hao hao chadema walichoma nyumba wakaacha waraka; hao hao chadema walimtishia magufuli kumuuwa; hao hao chadema; ................................................... nawe ongeza mabaya yaliyowahi kutokea dhidi ya watanzania ili tuwabebeshe hawa chadema! maana angalau sasa tumepata sehemu ya kupeleka lawama zetu!!
  HAKIKA NINASEMA MIAKA MICHACHE IJAYO HATA MVUA ZITAKAPOGOMA KUNYESHA AU KUNYESHA KUPITA KIASI, BASI USISHANGAE KUSIKIA INALAUMIWA CHADEMA KWA KULETA HAYO MAAFA!!!
   
Loading...