Elections 2010 Chonde chonde Slaa/Chadema, unganeni na wanamageuzi wenzako

Mkandara;
Umekosea, ni uongo; hakuna kitu kama hicho. Kwa mujibu wa sheria, kila chama hujitafutia rasilimali zake kwa ajili ya kugharamia kampeni za uchaguzi. Na hii inabainishwa na sheria ya Gharama za Uchaguzi.
Sawasawa?
Hivi kwani serikali imeacha kutoa ruzuku kwa vyama vya mageuzi sikuhizi...?
 
Mkuu nadhani ulimaanisha CHAMA na sio UPINZANI?
Hapana nimemaanisha hivyo hivyo kwa maana kubwa ya Upinzani ktk mfumo wa pili. Upinzani uliopo nchini ni baina ya watu sio wa vyama (Kiitikadi - mfumo wa kwanza) huko wamejishikiza tu kwani upinzani wetu ni baina ya watu, hata ndani ya vyama vyenyewe.(Uongozi -mfumo wa pili).
 
Ukweli utabakia kwamba sisi tunachopingana nacho ni mtawala au kundi la watu wanaotuongoza pasipo kutumia itikadi yoyote ila matakwa yao binafsi. Hakuna mtu anayeweza nambia JK anatumia itikadi gani wala mtu anayeweza kunambia Dr.Slaa anapingana na itikadi gani kwani sera zote na ahadi zao hazihusiani na itikadi zaidi ya kuzungumzia siasa za kanyaga twende...

...Hakuna mtu anayepinga CCM kwa sababu ya itikadi zake walka hakuna mtu anayepinga Chadema kwa sababu ya itikadi zake ila tunapinga vyama vyote kutokana na viongozi wao waliosimamishwa. CCM na Chadema vimesimama kama WATU badala ya chama kuwakilisha Upinzani.
Madhali unakili mwenyewe kuwa hivi vyama vimesimamisha watu badala ya chama, then inabidi mfumo wote wa vyama vya siasa nchini utizamwe upya kabisa. Personally, nisingependa kumchagua mtu. Napenda kuchagua chama chenye sera nzuri na mtizamo yakinifu wa kulipeleka taifa letu katika mahala pazuri.
 
Bila shaka hili tumelizungumza siku nyingi sana hapa JF.. Kilichotakiwa ni Nyerere kukiua kwanza chama CCM na kuanzisha makundi ya vyama kutokana na Itikadi ndani ya CCM yenyewe.. Sasa maadam Nyerere hakufanya hivyo kama inatakiwa tuanzishe vyama kutokana na Itikadi lazima CCM ife kwanza jambo ambalo haliwezekani, lakini pia tutakuwa na muda mrefu sana kujifunza kuelewa tofauti ya itikadi pasipo kujua mazuri na madhara ya kila itikadi ktk maisha yetu.. Ndio maana husisitiza zaidi kufikiria kitu kinachotokana na WATU na MAZINGIRA ya wahusika.

Hao tunaowaiga wana Mtawala wa Kimalkia ambaye hahusiki kabisa na Siasa. Wenzetu wamepitia hatua za kupinga utawala wa mtu mmoja au kundi la watu hivyo kubuni falsafa pinzani ya udhia huo na kiongozi huja na vision yake wakati sisi Mtawala ndiye mwenye fikra pasipo vision hivyo kuwafanya watawala wenye ambition..

Hivyo bado tunaweza mchagua mtu, na pengine ktk hatua hizi na kupinga mtu tutakuja fikia upinzani wa kifikra kuliko kujaribu kutumia itikadi kama sababu ya Upinzani hali hakuna kitu kama hicho..
 
Sawa mkuu. Nimekuelewa. And shukrani kwa ufafanuzi wako, japo binafsi sikubaliani kabisa na mtizamo wako katika hili [but that's a topic for another day].
 
Mkuu sawa tu hata usipokubaliana nami kwani hautakuwa wa kwanza ila tukubali tusikubali, demokrasia kwetu ni sawa na kuletewa Menu ya chakula cha kichina. Tunachokisoma hatuelewi na hata siku moja hatujawahi kupitia hatua za kuipenda au kuichukia Itikadi hivyo kuwa na maamuzi juu ya ubaya wa itikadi husika ili kufikia kuunda Upinzani wa itikadi hiyo.

Maadam tunataka demokrasia hali hatujui tunapingana kivipi ndio maana utaona leo CCM ambao ni mrengo wa kushoto wanasema kwamba Elimu na Afya bure Haiwezekani..tena wanaamini hivyo na kumpinga Dr.Slaa wakati ktk msahafu wao ndio nguzo kuu..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom