Chonde chonde Slaa/Chadema, unganeni na wanamageuzi wenzako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chonde chonde Slaa/Chadema, unganeni na wanamageuzi wenzako

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BongoTz, Oct 10, 2010.

 1. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingawa tunajua kwamba nchi yetu bado ni changa kwa siasa za vyama vingi kutokana na ufinyu wa elimu ya uraia waliyonayo watanzania walio wengi hususani sehemu za vijijini, lakini pia, uroho wa madaraka wa baadhi ya viongozi wa vyama vya Mageuzi umechangia kwa kiwango kikubwa kwa chama tawala kuendelea kuviburuza vyama hivyo katika kila chaguzi zilizowahi kufanyika--ukianza na ule wa mwaka 1995, 2000 na 2005. Na wasiwasi wangu mkumbwa ni kwamba, matokeo ya mwaka huu yatafanana na yale ya miaka ya nyuma kama wanamageuzi watashindwa kuunganisha nguvu mwaka huu ili kuing'oa CCM.

  Mtu yeyote mwenye akili timamu atakaa na kufikiri kuwa baada ya mageuzi kufanya vibaya katika chaguzi zote tatu zilizopita, upinzani ungekaa pamoja na kufikia uamuzi wa pamoja wa kuandaa mikakati kabambe ya kukabili uchaguzi wa 2010. Lakini badala yake, bado kila chama kinadhani kuwa kina ubavu wa kutosha kupambana na CCM ambayo imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 49 (ukiunganisha na miaka ya TANU).

  Watanzania walio wengi wangependa kuona vyama vya upinzani vikiungana au hata kushirikiana ili kukiondoa chama kinachotawala madarakani. Lakini kutokana na uroho wa madaraka wa baadhi ya viongozi wachache wa upinzani hilo linaweza lisitokee tena kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwani kila dalili zinaashiria kuwa huenda tena vyama vya Mageuzi vitarudia makosa yaleyale (kwa Kila chama kuamua kuingia kivyakevyake) kwa matumaini bandia kuwa huenda pengine muujiza utatokea na hivyo kuwashindisha viti vingi vya ubunge na hata kuwaweka ikulu.

  Umefikia wakati sasa kwa vyama vya Mageuzi nchini kuachana na ndoto za mchana na kutambua kuwa mfumo wowote ule wa vyama vingi unahuishwa na uimara na uthabiti wa vyama hivyo ambavyo vinakuwa tayari kuchukua fursa za kuongoza nchi kama chama tawala kikidorora. Wakishatambua hilo, basi waache kabisa kulalamika eti chama tawala kinatumia dola kuwatisha na kuwamaliza nguvu; na badala yake waunganishe nguvu kama wanataka kuwa na nafasi ya kukishinda chama tawala kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

  Sambamba na hilo, vyama vyote vya Mageuzi nchini vikae pamoja na kuandaa mbinu za kukabiliana na nadharia ambayo chama tawala kimefanikiwa kupandikiza vichwani mwa watanzania kwa muda mrefu sasa. Nadharia kuwa, "Mageuzi ni upinzani." Semina ziendeshwe nchini kote kuelimisha wananchi kuwa Mageuzi sio upinzani, bali Mageuzi ni mbadala wa chama fulani kuiongoza nchi pale chama kilichopo madarakani kinapokuwa kimedorora. Mabango yenye sera-mbadala yabandikwe sehemu zenye mikusanyiko ya watu wengi kuainisha mapungufu ya chama tawala na kutoa mbadala toka Mageuzi. Pia matangazo kwa njia ya Radio na Runinga yatumike kueneza kampeni ya kuzima nadharia kuwa "Mageuzi ni upinzani." Vyama vya mageuzi vina wasomi wengi, tunaamini kabisa hawawezi kushindwa kulielezea jambo hili kwa ufasaha zaidi.

  Pia, vyama vya Mageuzi vitafute njia nzuri ya kuelimisha wafuasi wao kuhusu umuhimu wa kura hata kama ni kura moja. Ukweli ni kwamba: ufinyu wa elimu ya uraia kwa wanachama wengi wa vyama vya upinzani [Mageuzi] umechangia kwa kiwango fulani kuvikosesha vyama hivyo kura halali tena nyingi tu katika chaguzi nyingi zilizopita. Mfano, wadadisi wa mambo ya kisiasa wanadai kuwa wananchama wengi wa chama cha CUF waliongozwa na jazba zaidi kuliko hekima katika uchaguzi mkuu wa 2005 na badala ya kupiga kura ya "HAPANA" kwa mgombea wasiyemtaka, wengi wao waliishia kuandika matusi na maneno ya kejeli mbele ya picha za mgombea wa chama tawala. Matokeo yake: kura hizo zilihesabiwa kama zimeheharibika.

  Kadhalika, badala ya kupoteza muda mwingi kutoa malalamishi mengi yasiyo na msingi dhidi ya chama tawala, vyama vya Mageuzi vinatakiwa kuweka sera za kueleweka mahala pake. Malalamiko tunayoyasikia kila siku toka upande wa Mageuzi kuwa: "oh, CCM ni wala rushwa..., CCM haijafanya lolote lile kwa kipindi chote chote ilipokuwa madarakani...blah blah blah..." hayawaingii wananchi maskioni kabisa endapo kama malalamishi hayo hayaambatanishwi na sera-mbadala zinazo onyesha kuwa ni nini tofauti ambacho Mageuzi wangefanya kama wao ndio wangekuwa madarakani. Kinachotakiwa sio kelele na lawama tu dhidi ya chama tawala, bali ni sera za kueleweka zenye makusudi ya kulichukua taifa letu kwenda hatua nyingine, hatua iliyo bora zaidi.

  Kimsingi, ili vyama vya Mageuzi viwe na nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni vema wahakikishe kuwa wanasimamisha mgombea mmoja (kiti cha urais) chini ya kivuli cha chama kimoja cha mageuzi chenye nguvu na mvuto mkubwa kwa wananchi. Kwasababu, hata kama mgombea watakayemsimamisha atakuwa hovyo, bado atabebwa na kuchachaguliwa kwa sababu tu ya nguvu na mvuto wa chama atakachowakilisha. Lakini kama Mageuzi watashindwa kufanya marekebisho haya mapema, basi wakae wakijua kuwa chama tawala kitaendelea kushinda na kuisabaratisha ngome ya Mageuzi tena na tena na tena...

  P.S. Mimi si mwanachama wa chama chochote. Ila ningependa kuona ushindani wa kweli kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

  Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!​
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi Chadema na Dr. Slaa wanazuia vp vyama vingine kuungana??????????
   
 3. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  No, hawazuii vyama vingine kuungana...
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa nini basi wanakuwa heading ya thread yako??????????????????
   
 5. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vyama vingi mi naona ni kama makampuni ya watu, watu wanashindwa kukaa na kuelewena pamoja!! but anyway akili itawaijia taratibu na kuacha mifumo dume ya kikabila, kifamilia, kidini na kuweka mbele maslahi ya taifa siyo kama sasa.

  Now we are just like gambling on American Roulette, kuna kupata au kukosa but better try than never. Tumeona hapo nyuma jinsi inavyotugharimu kutojaribu kabisa. So, tujaribu kwanza hawa jamaa wanaoonekana na sera ya mabadiliko huku tukiwashauri kuungana ili tupate vyama vyenye ushawishi kwa watu siku zote.
   
 6. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwasababau Slaa/Chadema have strong wind at their back heading to this year's general election... So I think itakuwa vema kama wakiunganisha nguvu na vyama vingine vya mageuzi kama kweli wanauchungu wa kuing'oa CCM. Maana ukweli ni kwamba, wasipofanya hivyo, nafasi yao ya kushinda ni finyu mno.
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  kwa nini sio vyama vingine ndio viunganishe nguvu na Slaa?, unajua siku zote weak ndio anaenda kwa Strong kama kweli ulikuwa na nia nzuri ya bandiko lako basi ungevishauri vyoma vyote viungane na Chadema kwa sababu kiko juu, na hili Chadema walishawahi kulifanya pale walipoiunga Mkono CUF
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  msingi wa kuungana huo uwe nini: kwa vile vyote ni vya upinzani? kwa vile vinataka CCM itoke madarakani? Kwa vile vinataka kutawala pamoja? kwa vile?? Au waungane kwa ajili ya kuungana tu?
   
 9. Mzuvendi

  Mzuvendi JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 446
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  BongoTz:

  I beg to differ with you and also think that you underestimating the ability of majority of Tanzanian people to make their political decisions. Tanzanians from all works of life understand their best interests, and in addition are capable of changing the political landscape. However, fundamental changes come with a price tag which many of us are not ready to pay. So, according to me, it is not the lack of civic education or knowledge that prevents Tanzanians from voting out the ruling party and their candidates. Rather it is the fear of unknown or political structure.

  Let's start with the fear of unknown. Many members of JF and perhaps educated elites think and believe that Dr. Slaa is the right candidate. But electing Dr. Slaa is just a bet. There is no guarantee that he will be a better president than the current one. Even though we hear many good things about Dr. Slaa here, may be on the ground, people who really make their votes count have different opinions about the guy or his political party. Remember that Tanzanians are voting for a party and not an individual personality. For example, there are some people who like Dr. Slaa because of what he does. However, the same people might dislike the demographic of CHADEMA, and that could potential hurts his bid. In Tanzania we try to think that demographic issues do not play a major role in political decision making. Nonetheless, that is what we have been fooling ourselves for many years. Deep down many Tanzanians think demographically.

  Moreover, Tanzanian political structure does not encourage political changes. Let me clarify this one. In Tanzania, general election includes presidential and parliament elections. This is a scam because the possibility is majority of people will vote for candidates from the same party. For example, the person who votes for Parliament candidate from CCM will also vote for President Candidate from CCM. One might argue that this shows lack of civic education or political naiveté. However, to associate political parties with successful campaigns of their few candidates is not a new phenomenon. Even in well developed countries, mediocre candidates could rely on the star power of other candidates in their party to win elections.

  For example, the star power of Barack Obama helped other democrat candidates to win elections in the 2008. However, some of them will have to contest their seats this year on their own, others in 2012 and other 2014. In the US, having different elections in different time period forces voters to shift their political affiliations, and thus encourage political discourse and changes.

  Another example is the political structure used in many European countries. In many European countries, the party that wins majority of seats in the parliament through proportional representation forms the government. In this type of system; people votes for their interests and it motives people take their political capital very seriously. For examples if your main concerns are environmental issues you will vote for green party. If you main concerns are immigration issues, probably you will for right wing parties and so forth.

  Now when it comes to Tanzania, let's face it squarely. We are forcing to implement a political system that does not work in our favor. For example, we have the executive branch (the presidency) which models the USA. However, we have parliament which models the British or the European. These two systems cannot fuse together because in Europe a government loses its mandate to govern when it loses its parliament majority or when it loses election. Whereas, in the US the government has a fixed period of four years to govern.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  BongoTz,
  tatizo la vyama vya Upinzani ni kwamba kila mmoja wao anataka kushika Usukani.. hakuna chama kinachokubali kwamba Dr.Slaa anaweza kushinda au kuwapa viti vya Ubunge hivyo ni bora kila chama kisimame peke yake kwa sababu ya Ruzuku..

  Moja kubwa ni kwamba Kila chama kilichojiaqndikisha mwaka huu kilipewa billioni 17 (kama sikosei) za uchaguzi mkuu sasa fanya times 18 party. Wakiungana hizo fedha hawatazipata pia Ubunge ktk Upinzani ni tombola, kila mmoja ana nafasi ya ushindi dhidi ya CCM hivyo kuna uwezekano wa chama kimoja kupata ruzuku hiyo na kuigawa ktk kundi dogo kuliko kuingia mtungo na vyama vingine hilo panga la mgao litagawanyika kwa kundi kubwa zaidi..

  Na Mwisho, lenye utata zaidi ni kwamba CCM chama kubwa kina Mapandikizi ndani ya vyama hivi na bahati mbaya kila chama kinamhofia mtu fulani ndani ya chama fulani na kwa hofu hizo kila mmoja wao anamwogopa mwenzake..Maadam kuna hofu hii nadhani sisi wananchi tunabakia pasipo uwezo wowote zaidi ya kuwapa kura zetu wale wenye nia na uwezo wa kupata ushindi..
   
 11. Mzuvendi

  Mzuvendi JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 446
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  BongoTz:

  Trust me. Political parties are cash cow machines for some oppositions. Therefore, there is no incentive to come together. If they come together, some professional political leaders will forfeit their own income. So it is better to stay where they are and enjoy the free ride at tax payers expenses.

  CCM are politically savvier than what we give them credit for. They know government funding of political party will work on their favor.
   
 12. R.Lewis

  R.Lewis Member

  #12
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  PHP:

  Ruzuku inagawiwa kufuatana na idadi ya Wabunge nafikiri na asilimia ya kura ulizopata kwenye uchaguzi wa raisi uliopita kama sikosei
   
 13. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  hii kitu ipo hivi:

  Ndani ya CUF kuna Prof LIPUMBA ambaye ni Mwenyekiti. Taka usitake!huyu bwana ni PROFESSOR tena wa uchumi. Mara nyingi palipo na mtu Prof. huwa jambo ni gumu sana kwenda,mara nyingi huyu bwana (kama Prof) hapendi ushauri toka kwa mtu aliyemzidi kielimu. (Rejea wale Maprof walio UDSM-ni majigambo tu,huwa wabishi sana na fikra zao ndo wanazoziamini).

  Isitoshe, (hata kama nitapingwa) ni kwamba Prof LIPUMBA ndani ya CUF huku bara ni kama MUNGU(rejea huyu Prof. flani(nikumbusheni jina plz) aliyegombea uenyekiti ndani ya CUF alivyopata vikwazo visivyo na msingi). Na kule Z'bar MAALIM SEIF ndie kama NABII-MUHAMAD, kwahiyo Mungu Lipumba anamtuma Nabii wake Seif,and not otherwise.

  KWA CHADEMA: Huyu mwenyekiti FREEMAN MBOWE kwa namna moja au nyingine alihusishwa sana na kifo cha WANGWE, kumbuka ilisemwa kwamba alipeleka watu wamuondoe jamaa wakati yeye yupo South Afrika, na hii iliibuliwa na watu wa CUF, na hali hii ndiyo iliyoparaganyisha hawa jamaa kuungana.

  La mwisho, kwa sasa ni too late kwa wao kuwa kitu kimoja, labda mambo yakienda kombo mwaka huu,wajaribu 2015.

  MY TAKE: CUF wafanye utaratibu, mwaka huu Prof Lipumba asipopita,basi wambadilishe asiwe tena mwenyekiti, na wakubaliane kwa kura nani asimame nafasi ya urais 2015 kati ya member toka vyamam vyote vitakavyoungana.
   
 14. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  hakika uchaguzi wa mwaka huu....unamambo!!
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Uroho wa madaraka upo CCM.
   
 16. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila chama kimeanzishwa na malengo yake. Ili kuungana ni lazima kuwepo harmonization ya sera ambayo si rahisi kama unavyoamini. Kuna anayetaka Ubebapari, kuna anayetaka ujamaa kama CCM (kuniradhi linaweza likawa ni tusi), kuna anayedai haki za kutunza mazingira, kuna wa OIC, kuna wa kutaka kuwa karibu na benki kuu (EPA nk) na mifano ni mingi. Zaidi ya hapo kuna vyama vipo kuvuraga na vinalipwa kufanya hivyo. Sasa wewe unataka iweje?

  Lakini mbona Zanzibar hakuna kuungana ila CCM imekubali yaishe! Kwa hiyo usije hapa na prejudice na kuamini hiyo ndiyo working model. Otherwise thank you for constructive ideas
   
 17. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Good point, Dictator!!
   
 18. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi sina tatizo kama vyama vingine vikiamua kunganisha nguvu na Chadema ambacho kwasasa kinaonekana kuwa strong. Lakini inabidi tuwe realistic hapa: Mwaka 2000, Al Gore na Democratic party (walikuwa very strong) lakini for some odd reasons wakakataa katakata kumuaccomodate Ralph Nader. And matokeo yake: inasadikiwa kuwa Nader alichukua baadhi ya kura toka kwa Gore (esp. jimbo la Florida) na kusababisha Bush kushinda.

  I know kuna watu hapa wata-argue vikali na kusema kuwa, mahakama kuu ya marekani iliamua kumpa ushindi Bush; lakini ukweli wa mambo ni kwamba, kama Nader asingekuwepo kwenye ballot, uwezekano wa Gore kushinda uchaguzi wa mwaka 2000 ulikuwa mkubwa sana. And that's a fact. So mimi ninawaomba Chadema waangalie watakachopoteza kwa kukataa kuungana na vyama vingine and not the other way around, that's all...

  Kama Bob Dylan alivyowahi kusema, "when you got nothing, you got nothing to lose." TLP, CUF, NCCR, DP, have nothing to lose..
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu ndicho nilichosema kuwa ndio hofu ya vyama kupoteza ruzuku waliyotegemea ikiwa wataungana na vyama vingine, kutokana na hofu kubwa ya kutopenda Ubia hata kama uwezekano wa ushindi ni mkubwa.

  Kama unafahamu ukataji wa tiketi za bahati nasibu kuna watu huunda ushirika wakakata tiketi nyingi pamoja wakitegemea kama kuna ushindi watagawana mapato kinyume cha wale wasiopenda Ubia mtu hukata tiketi yake wenyewe akitegemea kama akishinda basi fedha zote zitakuwa zake hana Ubia..(Ubinafsi).

  Ila muhimu zaidi ni hilo la kwanza, wanapopewa fungu la JK la kampeni zao billioni 17 za maandalizi ya uchaguzi ambazo JK kajisifia sana ktk facebook.
   
 20. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  All of the above, plus, waungane ili hata kama wakishinda this october, wawe na pool kubwa la kupata watu/viongozi makini wa kuongoza/run nchi. I mean, let's be honest here, Chadema hakina enough brilliant politicians wataoingia ikulu kesho na kuanza kuongoza nchi kubwa kama Tanzania smoothly (most likely, watalazimika kukopa toka vyama vingine). And so, why not unite now...?
   
Loading...