Chonde Chonde Serikali tupieni upesi ' Jicho lake Kali ' katika huu ' Usanii ' wa uwekezaji wa GSM, Sevilla na la Liga kwa Klabu ya Yanga

GSM ni mfanyabiashara, kwa hiyo kwa vyovyote vile pia anazingatia maslahi yake, Mimi ni mwanachama mtiifu wa Yanga ninachokihitaji ni burudani tu ya mpira maana hayo mambo ya fedha hayanihusu kwani hakuna siku tulishawahi kupata gawio kutoka Yanga tukiwa kama wanachama kabla hata ya kuja hao GSM, hivyo basi GSM waendelee tu, cha msingi tunataka ushindi na mpira mzuri
Good boy sisi tunataka vikombe na burudani ya mpira thats all hao kina genta wababaishaji ni Simba ambao wanajifanya yanga hawataki tuendelee
 
Nikiwa kama Mwanachama wa Klabu ya Yanga mwenye Kadi ambayo Namba yake haina ulazima wowote ule kwa Wewe Kuijua naomba niwe wa Kwanza kuiomba Serikali makini inayoongozwa na ' Jemedari ' Rais Dkt. Magufuli kupitia Vyombo vyake ' Nyeti ' kabisa vitupie Macho katika hiki kinachoitwa ni ' Mchakato ' wa Kuipeleka Yanga SC yetu katika Mabadiliko na Mafanikio.

Kwa nilichokiona tu jana pale Serena Hotel nilijua nitaona mambo yenye Kuakisi kabisa yale Mafanikio ambayo ' Muhamasishaji ' wetu Antonio Nugaz alikuwa ' akituhubiria ' kwa Wiki nzima, lakini badala yake nilichokuja Kukiona ni harufu ya ' Usamjo Usamjo ' nikimaanisha ' Uwongo Uwongo / Utapeli Utapeli ' unaotaka kufanywa na huyu ' Tajiri ' wa sasa Gharib Said Mohammed ( GSM )

Tunaambiwa sijui La Liga mara tena Klabu ya Sevilla na hapo hapo tena GSM nao wanahusishwa yaani ni ' Kutuchanganya ' tu Sisi Wanayanga na Wanachama wa Yanga SC ambao ni kwa bahati mbaya mno wengi wetu hata uwezo Wetu tu wa Kupambanua mambo ni mdogo na siyo kama Wanachama wa Simba SC na Mashabiki zao ambao wengi Wao ' wamebarikiwa ' sana Akili ( IQ ) na Mungu.

Hivi Klabu yangu ya Yanga ina ulazima wowote ule wa Kumtafuta ' Consultant ' wa Kuleta Mabadiliko Yanga SC kutokea nchini Hispania ( Spain ) wakati hapa hapa Kwetu nchini Tanzania kuna ' Consultancies Firms ' nyingi tu ambazo zingeweza Kuisaidia Klabu yetu ya Yanga tena kwa Gharama nafuu kabisa na Pesa zingine zingesaida Kulipa Madeni ambayo yanaikabili Klabu yetu?

Na ni kwanini kama Jambo ni la Yanga SC yetu lakini anayeonekana kila mara akiwa ' mbele mbele ' na ' Kiherehere ' ni huyu GSM tu pekee lakini Viongozi Wetu wa Yanga SC ni kama vile ama nao ' Wameshatekwa ' na GSM au hawana tena Sauti kutokana na ' Njaa ' zao na Kutokujiamini Kwao? Nayasema haya kwa Uchungu kabisa kwani GENTAMYCINE sitaki Yanga SC yangu ipotee.

Nilitegemea katika Hafla ya pale Serena Hotel basi nami ningeuona kweli huo ' Uwakilishi ' wa unaoitwa ' Utatu ' wa akina GSM, La Liga na Klabu ya Sevilla ila niliona tu ' Muwakilishi ' asiye na Uzito wowote ule kutokea huko Hispania ( Spain ) huku Wanachana na Wanayanga ' tukidanganywa ' kama Watoto Wadogo tukiwa na Mwanachama Mwenzetu Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.

Anachokifanya huyu ' Tajiri ' GSM ni kutaka ' Kutuzuga ' tu Sisi Wanayanga hasa baada ya Kutusoma ' Upopoma ' wetu uliotutukuka kujifanya anatutengenezea Mtandao mkubwa wa Mabadiliko na Mafanaikio Sisi Wanayanga ili atuteke Akili kisha baadae aje kuwa ' Main Bidder ' katika ' Uwekezaji ' na baadae aichukue Yanga SC na aanze ' Kujitajirisha ' nayo Kikubwa sana.

Wanayanga hatujaambiwa huu ' Mchakato ' wa GSM, La Liga na Klabu ya Sevilla una Manufaa gani kwa Klabu yetu ya Yanga hasa Kiuchumi, Kimfumo, Kibishara, Kimchezo na Kiuwekezaji kabisa badala yake GSM imetafuta tu Waandishi wa Habari kadhaa ili waendelee ' Kutuhadaa ' Sisi Wanayanga na hatimaye ' Waaminike ' na ' Waiteke ' rasmi Yanga SC na tuje Kujuta rasmi.

Rais wangu Ndugu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Waziri husika Dkt. Mwakyembe, Baraza la Michezo Tanzania, TAKUKURU na hata Watu wa TISS tafadhali msikae mbali na hili linalofanywa na hii Klabu yangu ninayoipenda ya Yanga kwani kuna kila harufu ya ' Upigwaji ' hapa na tusisahau pia kuwa kwa sasa Hispania ndiyo Lango Kuu ya Biashara za Dawa za Kulevya na ni ' Wabaguzi ' Wakuu pia duniani.

Kwa hili kama Wanachama Wenzangu wa Yanga SC msiponielewa naihama Yanga SC na nahamia rasmi ama Azam FC au kule Biashara Mara FC.
Baki huko huko Hindu Mandal fc. Hatuhitaji mawazo yako ya kibarakoa
 
Mpira wetu, siku zote hausongi mbele sababu unaongozwa na watu waliochoka , unajadiliwa na kundi lililochoka lkn Lina nafasi ya kufikiwa na media na kutoa maelezo mareeeefu ya ujuwaji kuliko uhalisia.

Kama GSM ana malengo ya kuichukua Yanga kiurahisi kwa faida yake , kutakuwa na tofauti gani MO alivyoichukua Simba kiurahisi na kwa faida yake.

Mf mdogo toka lini, Simba ikawa na jezi rangi nyeusi iliyochanganyika na nyekunfu.

MO kaweka utambuzi wa rangi yake , hakuna aliyehoji kwa sababu timu ni yake.

Yupo katika mipango ya kuweka nembo ya kampuni zake na kutoa ule mchoro wa mnyama Simba wenye akili kimyaa.

Shule/ vyuo vipo vingi Tanzania lkn kuna wazazi kutokana na UKWASI walionao hupeleka watoto wao huko.

GSM kwenda Laliga ni fursa zilizopo pale TFF wenye upeo mdogo wamezikuta kule
 
Mwambie huyo GSM wako kuwa Tanzania hii ya sasa ni ya Rais Dkt. Magufuli hivyo huo Usamjo ( Utapeli ) wake kwa Yanga SC hatoliweza Kamwe.
Acha umbea wewe umeanza kushabikia lini Yanga?!!!...yaani watani zenu wanapoamua kujikwamua kutoka hali waliyonayo mnatia kaharufu cha kifigisufigisu kama yule zeruzeru juzi alishindwa kuzuia kinyongo chake kuhusu hii ishu...Iache Yanga na mashabiki wake bakini na MO wenu awape hizo billion 20
 
Jana katika ratiba ya shughuli nikaona kipengele cha utiaji sign kati Yanga na GSM nikajiuliza kuwa tuliambiwa utiaji sign utakuwa kati ya consultant kutoka LaLiga why GSM?, wakati walisema GSM atafadhili mchakato tu!, nikajua yaleyale "janjajanja" wao kama wanataka kutoa team kwa GSM watoe tu sio "Oh, consultant kutoka LaLiga and blah blah! ".
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom