Chonde Chonde Serikali tupieni upesi ' Jicho lake Kali ' katika huu ' Usanii ' wa uwekezaji wa GSM, Sevilla na la Liga kwa Klabu ya Yanga

Realgp

New Member
May 15, 2020
2
45
Nikiwa kama Mwanachama wa Klabu ya Yanga mwenye Kadi ambayo Namba yake haina ulazima wowote ule kwa Wewe Kuijua naomba niwe wa Kwanza kuiomba Serikali makini inayoongozwa na ' Jemedari ' Rais Dkt. Magufuli kupitia Vyombo vyake ' Nyeti ' kabisa vitupie Macho katika hiki kinachoitwa ni ' Mchakato ' wa Kuipeleka Yanga SC yetu katika Mabadiliko na Mafanikio.

Kwa nilichokiona tu jana pale Serena Hotel nilijua nitaona mambo yenye Kuakisi kabisa yale Mafanikio ambayo ' Muhamasishaji ' wetu Antonio Nugaz alikuwa ' akituhubiria ' kwa Wiki nzima, lakini badala yake nilichokuja Kukiona ni harufu ya ' Usamjo Usamjo ' nikimaanisha ' Uwongo Uwongo / Utapeli Utapeli ' unaotaka kufanywa na huyu ' Tajiri ' wa sasa Gharib Said Mohammed ( GSM )

Tunaambiwa sijui La Liga mara tena Klabu ya Sevilla na hapo hapo tena GSM nao wanahusishwa yaani ni ' Kutuchanganya ' tu Sisi Wanayanga na Wanachama wa Yanga SC ambao ni kwa bahati mbaya mno wengi wetu hata uwezo Wetu tu wa Kupambanua mambo ni mdogo na siyo kama Wanachama wa Simba SC na Mashabiki zao ambao wengi Wao ' wamebarikiwa ' sana Akili ( IQ ) na Mungu.

Hivi Klabu yangu ya Yanga ina ulazima wowote ule wa Kumtafuta ' Consultant ' wa Kuleta Mabadiliko Yanga SC kutokea nchini Hispania ( Spain ) wakati hapa hapa Kwetu nchini Tanzania kuna ' Consultancies Firms ' nyingi tu ambazo zingeweza Kuisaidia Klabu yetu ya Yanga tena kwa Gharama nafuu kabisa na Pesa zingine zingesaida Kulipa Madeni ambayo yanaikabili Klabu yetu?

Na ni kwanini kama Jambo ni la Yanga SC yetu lakini anayeonekana kila mara akiwa ' mbele mbele ' na ' Kiherehere ' ni huyu GSM tu pekee lakini Viongozi Wetu wa Yanga SC ni kama vile ama nao ' Wameshatekwa ' na GSM au hawana tena Sauti kutokana na ' Njaa ' zao na Kutokujiamini Kwao? Nayasema haya kwa Uchungu kabisa kwani GENTAMYCINE sitaki Yanga SC yangu ipotee.

Nilitegemea katika Hafla ya pale Serena Hotel basi nami ningeuona kweli huo ' Uwakilishi ' wa unaoitwa ' Utatu ' wa akina GSM, La Liga na Klabu ya Sevilla ila niliona tu ' Muwakilishi ' asiye na Uzito wowote ule kutokea huko Hispania ( Spain ) huku Wanachana na Wanayanga ' tukidanganywa ' kama Watoto Wadogo tukiwa na Mwanachama Mwenzetu Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.

Anachokifanya huyu ' Tajiri ' GSM ni kutaka ' Kutuzuga ' tu Sisi Wanayanga hasa baada ya Kutusoma ' Upopoma ' wetu uliotutukuka kujifanya anatutengenezea Mtandao mkubwa wa Mabadiliko na Mafanaikio Sisi Wanayanga ili atuteke Akili kisha baadae aje kuwa ' Main Bidder ' katika ' Uwekezaji ' na baadae aichukue Yanga SC na aanze ' Kujitajirisha ' nayo Kikubwa sana.

Wanayanga hatujaambiwa huu ' Mchakato ' wa GSM, La Liga na Klabu ya Sevilla una Manufaa gani kwa Klabu yetu ya Yanga hasa Kiuchumi, Kimfumo, Kibishara, Kimchezo na Kiuwekezaji kabisa badala yake GSM imetafuta tu Waandishi wa Habari kadhaa ili waendelee ' Kutuhadaa ' Sisi Wanayanga na hatimaye ' Waaminike ' na ' Waiteke ' rasmi Yanga SC na tuje Kujuta rasmi.

Rais wangu Ndugu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Waziri husika Dkt. Mwakyembe, Baraza la Michezo Tanzania, TAKUKURU na hata Watu wa TISS tafadhali msikae mbali na hili linalofanywa na hii Klabu yangu ninayoipenda ya Yanga kwani kuna kila harufu ya ' Upigwaji ' hapa na tusisahau pia kuwa kwa sasa Hispania ndiyo Lango Kuu ya Biashara za Dawa za Kulevya na ni ' Wabaguzi ' Wakuu pia duniani.

Kwa hili kama Wanachama Wenzangu wa Yanga SC msiponielewa naihama Yanga SC na nahamia rasmi ama Azam FC au kule Biashara Mara FC.
Ondoka tu brother, waache wenye timu yao waendelee !! Maana uchungu wa kutembeza bakuli wanaujua wao!! Kaa pembeni angalia yanayoendelea! Muda unatasema maana ndio mwamzi sahihi !!
 
Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
9,271
2,000
Mi nadhani wanawekeza ili nao wapate faida kwa hiyo pia msitegemee kupata faida kwa kipindi kifupi ingawaje Yanga ni Timu kubwa ambayo inatakiwa mikakati sahihi inayoonekana ila ndio hivyo mikakati endelevu hakuna unaona viongozi wanashika kila tawi ili waweze kuwafunga wapinzani na kulipa mishahara kwa kupitia hao wadhamini ingawaje Mambo hayapo sawa ...
 
MUSONI

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
890
1,000
Nikiwa kama Mwanachama wa Klabu ya Yanga mwenye Kadi ambayo Namba yake haina ulazima wowote ule kwa Wewe Kuijua naomba niwe wa Kwanza kuiomba Serikali makini inayoongozwa na ' Jemedari ' Rais Dkt. Magufuli kupitia Vyombo vyake ' Nyeti ' kabisa vitupie Macho katika hiki kinachoitwa ni ' Mchakato ' wa Kuipeleka Yanga SC yetu katika Mabadiliko na Mafanikio.

Kwa nilichokiona tu jana pale Serena Hotel nilijua nitaona mambo yenye Kuakisi kabisa yale Mafanikio ambayo ' Muhamasishaji ' wetu Antonio Nugaz alikuwa ' akituhubiria ' kwa Wiki nzima, lakini badala yake nilichokuja Kukiona ni harufu ya ' Usamjo Usamjo ' nikimaanisha ' Uwongo Uwongo / Utapeli Utapeli ' unaotaka kufanywa na huyu ' Tajiri ' wa sasa Gharib Said Mohammed ( GSM )

Tunaambiwa sijui La Liga mara tena Klabu ya Sevilla na hapo hapo tena GSM nao wanahusishwa yaani ni ' Kutuchanganya ' tu Sisi Wanayanga na Wanachama wa Yanga SC ambao ni kwa bahati mbaya mno wengi wetu hata uwezo Wetu tu wa Kupambanua mambo ni mdogo na siyo kama Wanachama wa Simba SC na Mashabiki zao ambao wengi Wao ' wamebarikiwa ' sana Akili ( IQ ) na Mungu.

Hivi Klabu yangu ya Yanga ina ulazima wowote ule wa Kumtafuta ' Consultant ' wa Kuleta Mabadiliko Yanga SC kutokea nchini Hispania ( Spain ) wakati hapa hapa Kwetu nchini Tanzania kuna ' Consultancies Firms ' nyingi tu ambazo zingeweza Kuisaidia Klabu yetu ya Yanga tena kwa Gharama nafuu kabisa na Pesa zingine zingesaida Kulipa Madeni ambayo yanaikabili Klabu yetu?

Na ni kwanini kama Jambo ni la Yanga SC yetu lakini anayeonekana kila mara akiwa ' mbele mbele ' na ' Kiherehere ' ni huyu GSM tu pekee lakini Viongozi Wetu wa Yanga SC ni kama vile ama nao ' Wameshatekwa ' na GSM au hawana tena Sauti kutokana na ' Njaa ' zao na Kutokujiamini Kwao? Nayasema haya kwa Uchungu kabisa kwani GENTAMYCINE sitaki Yanga SC yangu ipotee.

Nilitegemea katika Hafla ya pale Serena Hotel basi nami ningeuona kweli huo ' Uwakilishi ' wa unaoitwa ' Utatu ' wa akina GSM, La Liga na Klabu ya Sevilla ila niliona tu ' Muwakilishi ' asiye na Uzito wowote ule kutokea huko Hispania ( Spain ) huku Wanachana na Wanayanga ' tukidanganywa ' kama Watoto Wadogo tukiwa na Mwanachama Mwenzetu Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.

Anachokifanya huyu ' Tajiri ' GSM ni kutaka ' Kutuzuga ' tu Sisi Wanayanga hasa baada ya Kutusoma ' Upopoma ' wetu uliotutukuka kujifanya anatutengenezea Mtandao mkubwa wa Mabadiliko na Mafanaikio Sisi Wanayanga ili atuteke Akili kisha baadae aje kuwa ' Main Bidder ' katika ' Uwekezaji ' na baadae aichukue Yanga SC na aanze ' Kujitajirisha ' nayo Kikubwa sana.

Wanayanga hatujaambiwa huu ' Mchakato ' wa GSM, La Liga na Klabu ya Sevilla una Manufaa gani kwa Klabu yetu ya Yanga hasa Kiuchumi, Kimfumo, Kibishara, Kimchezo na Kiuwekezaji kabisa badala yake GSM imetafuta tu Waandishi wa Habari kadhaa ili waendelee ' Kutuhadaa ' Sisi Wanayanga na hatimaye ' Waaminike ' na ' Waiteke ' rasmi Yanga SC na tuje Kujuta rasmi.

Rais wangu Ndugu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Waziri husika Dkt. Mwakyembe, Baraza la Michezo Tanzania, TAKUKURU na hata Watu wa TISS tafadhali msikae mbali na hili linalofanywa na hii Klabu yangu ninayoipenda ya Yanga kwani kuna kila harufu ya ' Upigwaji ' hapa na tusisahau pia kuwa kwa sasa Hispania ndiyo Lango Kuu ya Biashara za Dawa za Kulevya na ni ' Wabaguzi ' Wakuu pia duniani.

Kwa hili kama Wanachama Wenzangu wa Yanga SC msiponielewa naihama Yanga SC na nahamia rasmi ama Azam FC au kule Biashara Mara FC.
 
MUSONI

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
890
1,000
Kweli IQ yako imeonekana kuwa uwezo wako umeishia hapo GENTAMYCINE unahitaji hiyo dawa ya gentamycine..
1.Kwanza naomba uwatake radhi wana YANGA WOTE kwa upuuzi wa kuwaambia IQ yao ndogo.
2,Nakushauri kama hujui jambo jipe muda wa kuuuliza wahusika ujue kuna Club yako , viongozi wako, nk pata data usikurupuke mkuu….
3, Hili ni jambo zuri sana na la kuiondoa Yanga point moja kwenda point nyingine….HALI YA KIUCHUMI SIO NZURI NA KLAB INA MIAKA 85 SASA TANGU 1935 bado wakae kwenye mawazo mgando kama yako sio sahihi
4. Pata muda nenda Klabuni utaeleweshwa taratibu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom