Chonde chonde, pamoja na uroho ulionao usile mifupa au ngozi ya hiki kiumbe.

View attachment 674642
Ulaji wa nyama ya kuku wa kisasa umeenea sana mijini kwa sasa.

Lakini jua kuwa madawa yote na kemikali zote apewazo kuku ili akue fasta hubaki kwa mda mrefu kwenye mifupa na ngozi yake. Kwa maana hiyo humuingia mlaji kwa njia ya kula sehemu hizo za kitoweo.

Embu jiulize kiumbe kinatotolewa leo na baada ya wiki 6 kinaliwa, kimekuaje hapo?
No wonder matatizo ya kiafya yanazidi pamoja na gyms zetu.

Shtukaa!
Mkuu angalia nyakati za kuandika mambo haya,toka nilikula harusin.hv watu hatujala kuku tuna mwaka leo unaniambia wana sumu,neema ya Mungu naihitaji sana
 
Mnatisha watu bure, mtu anakula kuku mwaka mara moja tena kipande tu cha nyama ya kuku. Aisee tembeeni muone. Africa kusini mboga kubwa ni kuku, nyama na ng'ombe na boga za majani. samaki huliwa na wachache sana. Na wala sikupata kusikia mtu alopata magonjwa kwa sababu ya kula kuku wa kisasa. Na watu wanakula kuku si mchezo.
Afu wanapigana miti si mchezo
huku nguvu zikipungua wanasema broiler
 
Ni mambo ya uongo sana haya.
Sayansi na tecknolojia kila inapokuwa katika nchi husika na LIFE EXPECTANCY huongezeka.
Acha kutupeleka kwenye ujima.
Stori za wauza dawa za kuongeza nguvu za kiume Kariakoo zimewaharibu wengi sana.
Wale jamaa wa Kariakoo ni wajanja sana, huwa nikitaka kucheka nakwenda kuwacheki.
SOMA wastani wa umri wa kuishi duniani utaona kuwa zile nchi zinazofanya kila kitu kwa usasa( kwa viwanda) ndizo huishi sana.
Kama haitoshi tembelea nchi kama US. au Singapore uone kama wanakula ugali uliotwangwa kwenye kinu.
 
Back
Top Bottom