johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 82,754
- 139,571
Nimeambiwa hapa kuwa kuna kundi kubwa la madiwani hasa mikoa ya kaskazini na baadhi ya wabunge wanapanga kuachana na Chadema na kuitikia kauli ya mzee Lowassa iliyowataka wafuasi wake kumuunga mkono Rais Magufuli.
Najua hili ni jambo jema na la kupendeza kwa CCM lakini kila nikifikiria gharama za chaguzi ndogo kiukweli naihurumia nchi yangu Tanzania.
Hivyo nakuomba sana mzee Lowassa washauri wote wenye mahaba nawe waliochaguliwa kama wabunge na madiwani wasubiri 2020 ndio warejeshe kadi za Chadema ili kutuondolea gharama za chaguzi ndogo.
Nakumbuka Zitto aliwahi kutumia busara hiyo akatuepusha na uchaguzi mdogo.
Maendeleo hayana vyama!