Chonde Chonde mnaopanga Ratiba za Kazi za Rais tafadhari Sana mzingatie Rais kupata Mapumziko

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,138
Bila kuwachosha,twende kwenye mada..

Nitoe tahadhari tuu kwa Nyie Wataalamu mnaopanga ratiba za mh.Rais hususani Katibu Mkuu Kiongozi na watu wako wa Usalama wa Rais.,jitahidini kumpa mapumziko mh.Rais.

Ni juzi tuu katoka Kwenye ziara ndefu tena ya kutumia magari mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,kesho Siku 2 Tanga na akitoka huko aende DRC..

Tunampenda na kumjali Rais wetu,chonde Chonde Wakuu msije kuanza kusema haambiliki mara anasema yuko fit nk nyie ndio mna dhamana hiyo 👇
Screenshot_20220814-162028.png
 
Wadai moja ya starehe yake kubwa ni kusafiri usiku akilala anawaza kusafiri kujipa visafariii na nyomi la magarii.
 
Naunga mkono hoja.Ni vizuri akawa anajipa muda kidogo wa kupumzika hasa baada ya kazi ngumu kama hii ziara aliyomaliza. Kupumzika angalau kwa siku moja ni muhimu sana kiafya.
 
Rais anatakiwa kuwa na afya njema kila wakati ili kuweza kukabiliana na matukio yote yahusuyo nchi yetu. Hivyo, aangalie namna anavyoweza kumudu shughuli zilizopo kwenye schedule. Ikiwa amechoka, awataarifu wasaidizi wake wanaomwandalia majukumu ili ku-adjust schedule, maana rais naye ni binadamu, hivyo anachoka. Waswahili husema kesho nayo ni siku, hivyo rais anaweza kuendelea na majukumu ya kitaifa siku nyingine!
 
Kwani si anao wasaidizi dunia nzima? Kwa nini asiwatumie? Makamu wa rais, waziri mkuu, mawaziri, ma RC, mabalozi.

Tatizo mama ubinafsi na kufikiria urais muda wote.

Kutwa kigulu na njia ndio maana ukigeuka huku mara hiki kimepigwa, mara kile. Taarifa hasomi. Atasoma saa ngapi? Hata hao TISS sidhani kama wanatoa tena ripoti kama enzi za jiwe. Maana tatizo ni ufuatiliaji wa hizo taarifa huyo anayepewa.

Ukitaka u shine peke yako na kuwazimia taa wengine kwa li nchi hili lilivyokuwa kubwa na matatizo lukuki hutaenea.
 
Una na unachoongea? Pili kwani ni vibaya kufikiria Urais wakati wote?

Mwisho hilo la kufikiria Urais mda wote Lina uhusiano gani na mada?
 
Back
Top Bottom