Chonde chonde Mh. Rais, usiwasahau wafuatao kwenye Timu ya mazungumzo

Huyu Mama nampenda saana ingawa tuko vyama tofauti...alisimamia Bunge kadiri ya uwezo wake na alikuwa kama Mzazi Bungeni....hakutukanwa.
Nilimpenda saana aliposema ukweli hapa tuna andika sheria sitaki ma bush lawyer..aliwataka kina Simbachawene...Halimaa...Tundu....nk....nk...Vivyo hivyo huko tupeleke vichwa kweli kweli ..Dr Fauzi Twaib naye Kichwa kweli kweli lakini kajificha
 
Unaanzaje kumuacha Tundu Antipas Lissu?
Anapendekeza tume ya kujadili chenji ya Acacia, sio umahiri wa kujenga hoja za kisiasa. Unaanzaje kuteua mtu anayedai kuwa tume imefanya makosa na kwamba watanzania tutanyolewa mapema asubuhi!? Yuda Iskarioti ana nafuu kwa sababu alimsaliti Jesus kimyakimya
 
Kwenye hiyo Kamati ya Mh. Rais hatuhitaji tu Academic Gurus, tunahitaji pia Economic Hitmen, swali je, tunao hao Economic hitmen?
 
Tunahitaji wabobezi kwenye sheria,madini,hisabati n.a. kubwa zaidi wenye historia ya uzalendo usio na shaka
 
Kwenye hiyo Kamati ya Mh. Rais hatuhitaji tu Academic Gurus, tunahitaji pia Economic Hitmen, swali je, tunao hao Economic hitmen?
Kwenye fani hiyo unamfananisha askari ndani ya kifaru apigane na askari mwenye bastola
 
1: Mh. Kassim Majaliwa Kassim

2. Prof. Paramagamba Kabudi.

3: Prof. Abdikalim Mruma

4: Prof. Nehemiah Ossoro.

5: Prof. Issa Shivji

6: Prof. Benno Ndullu

7: Kamishna wa TRA

8: Prof. Ibrahim Lipumba

9: Dr. Rugemeleza Nshalla, huyu ni mkurugenzi wa LEAT

Ongezeeni wengine wadau ili Kuunda timu imara itakayopambana kwa hoja na kusimamia hoja kwa maslahi ya nchi.
Wote nawakubali ila Waziri Mkuu hapana,awaachie wataalam.Kamishna wa TRA sawa, ila ni lazima awe na weledi usiyo tiliwa mashaka kwenye mambo ya kodi.Pia awe mtu ambaye sio rahisi kununuliwa. Watu wa TRA wengi ni money mongers. Nshalla anafaa sana. Professor Lipumba ni mchumi mzuri, ila simuamini sana.Anaonekana kama mtu anayeweza kununuliwa kiurahisi.Professor Ndulu naye like wise.
 
1. Hamorapa

2. Roma mkatoliki

3. Snura Yule WA chura

4. Lemutuz a.k.a KJ

5. Asumpta mshana

6.TID n.k
 
Hapo kwa Propesa Lipumba umetokota sana aisee! Harufu ya pesa haimuachagi salama huyo mzee.
 
Jamani, tuweni serious hili swala ni muhimu sana, na juzi wakati ACACIA anafanya mawasiliano ya simu na wanahisa, aliwaeleza kuwa wangependa kujua mapema timu yetu, Mh. Raia Usikubali wawajue mapema, cha msingi wateue tu then uwatangaze last minute,

hawa wazungu wanaweza kuomba Account zao za Bank ikiwa utawatangaza mapema, cha msingi hapa tunashauri tu, ila wewe ndiye utaangalia nani awemo nani asiwemo, hawa wazungu ni wajanja sana, ukiwatangaza mapema imekula kwetu, maana hawashindwi kutafuta na kupata account zao za Bank na ku-deposit milioni 300 kila mjumbe
Usiriaz uliisha pale mwizi aliingia ikulu
 
1.Job Ndugai
2.Lusinde aka Kibajaj
3. Kasheku Msukuma
4.Assumpta Mshama
5.Salma Kikwete
6.Bashite
7.Humphrey Polepole
8.Abdallah Bulembo
9.Anna Kilango Malecela
10.Prof.Maji Marefu
 
Back
Top Bottom