Chonde chonde 'Mafisadi' Msiende Mahakamani-Jaji Bomani

Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
751
65
Jaji mstaafu awaonya wanaotaka kumshtaki aliyewaita mafisadi

Na James Magai

WAKATI viongozi mbalimbali wa Serikali waliotuhumiwa kwa ufisadi na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willibrod Slaa wakitishia kwenda mahakamani, Jaji Mark Bomani amewaonya viongozi hao kutokuchukua hatua hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Jaji Bomani alisema wale wote waliotuhumiwa katika kashfa ya ufisadi na rushwa wanapaswa kufikiria upya kama kuna ulazima wa kwenda mahakamani kabla ya kuchukua hatua hiyo kwani kufanya hivyo kunaweza kuibua mambo mengine mazito na kuzusha mfarakano nchini.

"Malumbano juu ya suala la rushwa na ufisadi nchini yamepamba moto na yanaweza yakafikia kiwango cha kuleta mfarakano na uhasama katika jamii. Kutokana na hali hii maombi yangu ni kwamba tuwe na uvumilivu wa kisiasa na ninawaomba ndugu zangu wanaotishana kushtakiana mahakamani wafikirie upya ulazima wa kufanya hivyo," alitahadharisha Jaji Bomani.

Alisema kabla ya kuchukua hatua ya kwenda mahakani, wote waliotuhumiwa wanapaswa kuchukua muda wa kutosha kufikiri ili kupisha joto la malumbano lipite ndipo wafikirie kuchuka hatua zaidi.

"Yawezekana wamefikia hatua hii kutokana na ughafla wa jambo lenyewe na hivyo wanaweza kutoa kauli za haraka haraka kwa sababu ya kukasirishwa, lakini pengine kuna njia nyingine ambazo wangeweza kuzitumia kumaliza suala hilo pasipo kupelekana mahakamani, " alishauri Jaji Bomani.

Alionya kuwa kupelekana mahakamani kuna athari kubwa na kwamba kunaweza kuibua mambo mengine makubwa zaidi na hivyo akatoa ushauri kuwa kabla ya kuchukua hatua hiyo, wahusika wapeleka malalamiko yao katika taasisi nyingine kama vile Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Alisema ametoa tahadhari hiyo kutokana na uzoefu wake katika mambo ya sheria na kwamba hata wateja wake ambao wanamfuata katika kazi yake ya uwakili kwa nia ya kwenda mahakamani kuhusiana na suala hilo, huwa anawashauri kwanza kutafuta suluhu kwa vile anajua suala la kwenda mahakamani kwa kukurupuka lina athari zake.

Hata hivyo, Jaji Bomani, alisema madai ya kuwepo kwa rushwa na ufisadi nchini si jambo la kushangaza, kwani vitendo hivyo vipo pamoja na kuwa havikubaliki katika nchi inayoamini katika usawa wa binadamu na utawala bora.

"Kwa hili nakubaliana na Jaji Warioba kuwa kazi kubwa mbele yetu ni kuendeleza nchi yetu ili itufikishe kwenye maisha bora kwa kila Mtanzania. Nguvu zote za taifa zinatakiwa zielekezwe kwenye jambo hili na malumbano yote yanayoweza kuyumbisha jitihada hizi hayana budi yaepukwe," alisema Jaji Bomani.

Kuhusu tuhuma zinazotolewa na vyama vya upinzani juu ya baadhi ya viongozi wa serikali kujihusisha na rushwa na ufisadi, Jaji Bomani alisema vyama hivyo vina uhuru wa kutoa maoni yao, lakini akasema shutuma zinazotolewa ni za jumla jumla mno kiasi kwamba hazibainishi ni jinsi gani viongozi hao wamehusika katika rushwa na ufisadi huo.

Mwananchi 01-10-2007
 
Mimi naona afadhali waende mahakamani ili yafukuliwe mengi zaidi.
Tumechoka kufunika uchafu chini ya zulia. Sielewi kwa nini Mzee Bomani hataki ukweli ufichuliwe.
 
Hili swala ni kubwa sana na hawa wezi walikuwa wanafahamu kwamba wabongo ni wajinga sasa moto ndio umewashwa na hauwezi kuzimwa, tutakula nao sahani moja. (Wako wengi hawa na wengine bado hawajajulikana inabidi tuanze alifu).
 
Isije ikawa ni janja yake paka, wanamtuma Bomani anajifanya kuwashauri wasiende mahakamani, kumbe walikuwa hawana mpango wa kwenda huko ilikuwa ni njia ya kujikosha tu!, sasa wanatafuta pa kutokea kwamba tumeacha kwenda mahakamani kwa vile tumeshauriwa hivo!!

Hebu nendeni muache kutuchezea akili ebo!
 
1. "lakini pengine kuna njia nyingine ambazo wangeweza kuzitumia kumaliza suala hilo pasipo kupelekana mahakamani, " alishauri Jaji Bomani.

2. Alionya kuwa kupelekana mahakamani kuna athari kubwa na kwamba kunaweza kuibua mambo mengine makubwa zaidi na hivyo akatoa ushauri kuwa kabla ya kuchukua hatua hiyo, wahusika wapeleka malalamiko yao katika taasisi nyingine kama vile Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

3. huwa anawashauri kwanza kutafuta suluhu kwa vile anajua suala la kwenda mahakamani kwa kukurupuka lina athari zake.

4. Hata hivyo, Jaji Bomani, alisema madai ya kuwepo kwa rushwa na ufisadi nchini si jambo la kushangaza, kwani vitendo hivyo vipo pamoja na kuwa havikubaliki katika nchi inayoamini katika usawa wa binadamu na utawala bora.

5. "Kwa hili nakubaliana na Jaji Warioba kuwa kazi kubwa mbele yetu ni kuendeleza nchi yetu ili itufikishe kwenye maisha bora kwa kila Mtanzania. Nguvu zote za taifa zinatakiwa zielekezwe kwenye jambo hili na malumbano yote yanayoweza kuyumbisha jitihada hizi hayana budi yaepukwe," alisema Jaji Bomani.

Wakuu this is very discouraging, huyu mkuu si aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya kwanza, yaani kuna wakati naye huyu alikuwa na ambitions za urais?

Yaaani wa-Tanzania, hatuna mahali pa kukimbilia I mean hawa watu wanasema nini? Wasiende mahakamani ili waende wapi? Takuru ya Hosea, whta happened to Richmond? Mimi nafikiri tumefikia mahali pa no return, the next stop ni mhakamani tu!
 


Wakuu this is very discouraging, huyu mkuu si aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya kwanza, yaani kuna wakati naye huyu alikuwa na ambitions za urais?

Yaaani wa-Tanzania, hatuna mahali pa kukimbilia I mean hawa watu wanasema nini? Wasiende mahakamani ili waende wapi? Takuru ya Hosea, whta happened to Richmond? Mimi nafikiri tumefikia mahali pa no return, the next stop ni mhakamani tu!

Mkuu heshima yako. Kama hawana cha kuficha, basi hawana cha kuogopa katika azma yao ya kuwashtaki waliowachafulia heshima yao, lakini kama wana madudu wamefanya basi lazima wafikirie mara mbili mbili maana kuna uwezekano kesi hii wakaingia 'waliokuwemo' na wasikuwemo.
 
Mzee FMES, Jaji Bomani kaona kitu.. wakienda mahakamani... watabeba mzoba mzoba mambo mengine.. na zile siri za familia zitawekwa hadharani... Ndio ule msemo kuwa kichuguu kimekuwa mlima utatimia.
 
Mkuu heshima yako. Kama hawana cha kuficha, basi hawana cha kuogopa katika azma yao ya kuwashtaki waliowachafulia heshima yao, lakini kama wana madudu wamefanya basi lazima wafikirie mara mbili mbili maana kuna uwezekano kesi hii wakaingia 'waliokuwemo' na wasikuwemo.

Unajua mkuu heshima mbele,

Yaani sasa nimeanza kuchoshwa na hii drama, I mean ni nchi gani duniani watu wenye ushahidi dhidi ya watuhumiwa, na watuhumiwa wenye ushahidi dhidi ya wanaowatuhumu, wanashauriwa wasiende mahakamani, hivi umemsikia hata balozi mmoja toka nje akisema msiende mahakamani?

Amani itapungua? Hivi ni amani ipi hiyo wanayoisema? Mwananchi anakuwaje na amani wakati haiamini serikali yake? Mimi nilifikiri huu ndio wakati wa CCM kujisafisha na kujiweka sawa maana ni kwenda mahakamani kushinda na kuwamaliza kabisaa upinzani, I mean kweli unahitaji kuwa political science professor kuelewa kuwa kama kweli hawa viongozi waliotuhumiwa hawana makosa as of their claim, basi CCm ni kuwasafisha na kuwa-bulldoze tu upinzani for the rest of their political life au career?

Yes huu ndio utakuwa mwisho wa Zitto, na upinzani kwa ujumla iwapo watashinda mahakamani, maana kama hakuna ushahidi dhidi yao basi ni kuwafungulia Treason Charge kina Dr. slaa na Zitto, tena kwa kuhatarisha amani yetu hebu niambie ni mtu gani duniani atakayelalamika?

Tunawaambia wanayamaze, lakini hawasikiii, what a drama? Hawa walikuwa wamezoea kujificha nyuma ya Mwalimu, that party is over, mambo yawekwe hadharani tu, next stop Mahakamani tukamkome nyani mchana kweupe!
 
Hapa wasituchezee akili, waende mahakamani, na this time,

Onyo kwa Mahakama, hatutaki mambo ya kesi za Ditto kupindisha sheria na Hossea na RICHMOND, iwe haki bin haki hapo ndo Nyani atakuwa amekomwa kunako!
 
Nafikiri tumeshafika point of no return. Wananchi hawana imani tena na mahakama,Bunge chama tawala na serikali yake. Imani kwa vyombo vya dola alikadhalika, watu hawataki kujisumbua kwenda mahakamani, tume ya kuzuia rushwa wala polisi. Hivi tumebakiza nini wakuu...?
 
Mzee Es mbona unatema moto hapa ? Unaamini kabisa kwamba Zitto na Slaa wanastahili treason ? Kisa ni kusimamia maslahi ya taifa ama una maana gani ? Una uhakika kwamba Mahakamani mtashinda na hivyo kufuta Upinzani kama ambayo mnawaza ? Upinzani si Zitto na Slaa kwa taarifa yako .

Haya nendeni Mahakamani kila kitu kitawekwa wazi na Rais na Waziri wake Mkuu wataitwa Mahakamani maana mambo ni makubwa nionavyo mimi .
 
Mzee FMES, Jaji Bomani kaona kitu.. wakienda mahakamani... watabeba mzoba mzoba mambo mengine.. na zile siri za familia zitawekwa hadharani... Ndio ule msemo kuwa kichuguu kimekuwa mlima utatimia.

Mkuu heshima mbele, look at this kwa umri walionao sasa hivi Zitto, na DR. Slaaa, wana at least another 30 years ya kutusumbua CCM, sasa what an opportunity kutawala for the next 30 years bila makelele, maana watuhumiwa wanasema wako safi na wanataka kwenda mahakamani, huko wakishinda ina maana utakuwa ndio mwisho wa Zitto, Dr. Slaa na upinzani kwa ujumla, I mean kaput bin finish, maana after that hakuna mbongo mwenye akili timamu atakayewasikiliza tena, wao wala kiongozi yoyote mpya wa upinzani maana kazi yetu CCM itakuwa ni kuwakumbusha tu kila ukifikia uchaguzi kuwa hawa ni wahuni tu kazi yao ni kutengeneza majungu yaliyoenda shule, sasa hizi nyimbo za msiende mahakamani exactly anayezianzisha ni nani? Wasiende mahakamani under who's expense kama sio sisi wananchi walalahoi?


Mkuu Rwabugiri,

Heshima mbele mkuu, I am down na your theory kusiwe na dhamana ili wasiharibu ushahidi:-

Hapa wasituchezee akili, waende mahakamani, na this time,
Onyo kwa Mahakama, hatutaki mambo ya kesi za Ditto kupindisha sheria na Hossea na RICHMOND, iwe haki bin haki hapo ndo Nyani atakuwa amekomwa kunako!
 
Nafikiri tumeshafika point of no return. Wananchi hawana imani tena na mahakama,Bunge chama tawala na serikali yake. Imani kwa vyombo vya dola alikadhalika, watu hawataki kujisumbua kwenda mahakamani, tume ya kuzuia rushwa wala polisi. Hivi tumebakiza nini wakuu...?


Heshina mbele mkuu,
Yaani umesema kweli kabisa hadi nimechoka! Labda tuelekeze macho yetu kwenye masanduku ya kura, na hayo kama hayatazingirwa na FFU na kubadilisha kura zetu halali!!

Na labda tuzigeukie mahakama zetu nazo tuziseme kwa nguvu tuziumbue na kuzizomea ili zianze kutenda haki na si kupindisha sheria kwa matakwa ya watu kadhaa kama muuaji Ditto na Jambazi Nyari!!

Na pengine la muhimu zaidi tuzidishe shinikizo la kudai katiba mpya ili mabadiliko ya system nzima ya sheria kandamizi ziondolewe ili haki itendeke katika nyanja zote!
 
Mzee Es mbona unatema moto hapa ? Unaamini kabisa kwamba Zitto na Slaa wanastahili treason ?

Mzee Lunyungu,

Heshima mbele mkuu, absolutely TREASON kwa kuvuruga amani kama hawana ukweli, tena kwenye hilo sina compromise kabisaaa, mimi ninawaamini viongozi wangu wote wa taifa langu, kuanzia Upinzani mpaka CCM, wanaposema wana ushahidi,

Kwa hiyo what is the problem hapa twende mahkamani tu, hakuna suluhu nyingine, believe me mkuu atakayeshindwa ndio mwisho wake kisiasa hata iwe CCM, maana hakutakuwa na msaada wa nje tena mkuu wangu!
 
Mkuu Rwabugiri,

Heshima mbele mkuu, I am down na your theory kusiwe na dhamana ili wasiharibu ushahidi:-

Mkuu you dont have to...

Hapa ni kwamba tusiseme waende mahakamani, kumbe mahakama zenyewe ni zile za kupindisha sheria kumuachia huru jambazi Nyari na muuaji Dito!!!
Yaani hapa hata mahakama zitende haki na kutimiza wajibu wao!

Na pengine mkuu wakati we unawazia kwamba mahakama ziishie na kushindwa kesi kwa upinzani hivyo kuumaliza kabisa, kwa upande wangu nawazia mahakama itende haki na hao wezi wote/ mafisadi wote wafilisiwe hizo mali zetu zirudishwe!

Na si hilo tu, hiyo mikataba ya kihuni walio tuingiza ibatilishwe pale itakapo dhihirika kwamba hata hao wawekezaji waligawa pipi kwa hao mafisadi ili wasaini hiyo mikataba mibovu!
 
Mzee Lunyungu,

Heshima mbele mkuu, absolutely TREASON kwa kuvuruga amani kama hawana ukweli, tena kwenye hilo sina compromise kabisaaa, mimi ninawaamini viongozi wangu wote wa taifa langu, kuanzia Upinzani mpaka CCM, wanaposema wana ushahidi,

Kwa hiyo what is the problem hapa twende mahkamani tu, hakuna suluhu nyingine, believe me mkuu atakayeshindwa ndio mwisho wake kisiasa hata iwe CCM, maana hakutakuwa na msaada wa nje tena mkuu wangu!


Mzee FMES, hivi unajua maana uhaini, maana kama ni kuvuruga amani, na kutokuwa na ukweli basi wa kwanza kuwa na hatia ni CCM!! Tatizo ni kuwa CCM wenyewe hawawezi kuthubutu kwenda mahakamani kwani watakuwa siyo tu wamejikaanga kwa mafuta yao bali pia watakuwa wamejikatia kachumbari ya mlo wao wa mwisho! Binafsi, I beg them to go to court! na wakienda huko Mwanasheria Mkuu afungwe mikono hakuna cha null prosquei wala nini. So nakubaliana na wewe kwenye hilo kama CCM na viongozi waliotajwa wanahisi wamechafuliwa majina (hakuna mahali popote ambapo kuna mtu amedai wameharibu amani!) basi waende mahakamani na wawashtaki kwa kudai mabilioni ya fidia.

Kikwete mwenyewe alipodai kuwa atakwenda mahakamani kwa sababu ya kudaiwa kuwa amechukua fedha za Wairani, mbona hakwenda hadi leo hii? Na watu bado wanaamini ni msafi!
 
nafikiri sasa kuuza nchi yenyewe ili kila mtu achukue chake,la sivyo tutakapo zinduka tutakuta ccm wameshatuweka rehani.huu mkono na ndio mwanasheria wa serikali amechomoa itakuwa hao wenzangu na mimi mzungu wa reli
 
Nafikiri tumeshafika point of no return. Wananchi hawana imani tena na mahakama,Bunge chama tawala na serikali yake. Imani kwa vyombo vya dola alikadhalika, watu hawataki kujisumbua kwenda mahakamani, tume ya kuzuia rushwa wala polisi. Hivi tumebakiza nini wakuu...?

Mafuchila,

Heshima mbele mkuu.

The only option we have is the voice of the people. Vox populi, vox dei, "The voice of the people is the voice of God". Na hii ndiyo sababu kubwa imewafanya upinzani waipeleke hii kesi kwa wananchi. Wananchi wakiwasha moto, hauzimiki mpaka kieleweke.
 
Mzee FMES, hivi unajua maana uhaini, maana kama ni kuvuruga amani, na kutokuwa na ukweli basi wa kwanza kuwa na hatia ni CCM!!

Mkuu MMJ,

Heshima mbele mkuu, kwenye hili la ufisadi hakuna siasa kabisaa, ni ishu ya sheria tu, nashangaa sana viongozi wetu wanapojaribu kuligeuza kuwa siasa, sioni siasa on it ni mahakama tu kama hatuziamini za bongo twende the Haque,

Maneno ya Muungwana na hela za Iran, haikuwa ishu ya CCM, na sidhani kama ni ishu anyways maana tunajua kuwa vyama vyote wagombea wetu wote walipewa hel;a toka nje za kuogmbea urais, na tulishakubaliana huko nyuma leo kuwa hela za nje kwa the good of our nation ni sawa kabisa, kwenye hilo simalumu kiongozi yoyote aliyechukua helka nje kwa ajili ya kampeni, unless kama kuna hoja kwamba hela za Uingereza ni bora kuliko za Iran,

Anyway, sitaki kuingiza siasa tena kwenye hii ishu kwa hiyo nitatulia mpaka nitakpoona inaelekea mahakamani, maaan aliyekula hela nani mimi nianze kulumbana hapa kama mwenda wazimu sio kool mkuu, unless ikitokea an interesting story on the ishu labda ila for now nitasubiri mahakamani!

Asante Wakuu!
 
Mzee ES,

Kuambiwa kapewa fedha na Irani ilikuwa ni KUCHAFULIWA JINA (ndivyo alivyong'aka JK), nawe wasema halikuwa jambo baya?

Dr. Slaa na Zitto waliamua kwenda kwenye mahakama ya raia baada ya kugundua kwamba Sitta na Bunge la CCM walikuwa na njama mbaya. Sisi raia tulikuwa tunaona wizi wa mali ya uma ulivyokuwa unafanywa na viongozi wa CCM. Tumeyapokea mashtaka yaliyoletwa kwetu na Slaa, Zitto na Mrema kama udhibitisho tu wa yale tuliyoyadhania.

CCM ina hatia zifuatazo: Ina viongozi wanaopora mali ya uma. Imehodhi madaraka kwa njia za wizi wa kura. Imeuza mali asili za taifa bila ridhaa ya wawakilishi wa wananchi. Ina viongozi wanaowekeana mikataba ya siri na wawekezaji, na wanaokataa hata kuwaonyesha wawakilishi wa wananchi yaliyomo kwenye hiyo mikataba. Ina viongozi wanaoendeleza utawala wa kiimla.

Siku ya mahakani itakuja, lakini itakuwa ni ya kuwafikisha wezi wetu kwa Pilato, baada ya kukiweka chombo chao benchi kama ilivyotokea kwa UNIP Zambia. Hawa wanaopora mali ya uma na kulindana ndani ya CCM kwa sasa ni wafungwa wetu watarajiwa.
 
Back
Top Bottom