Chonde chonde Jaji Waryoba, Katiba na Mungano haviwezi kukusanyiwa mawazo kwa pamoja.

jogoolashamba

jogoolashamba

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
348
195
Paka ukimpa samaki, hata mkavu, humla kuanzia kichwani. Jaribu uone anytime.

Jaji Waryoba anaongoza Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Ukubwa wa tatizo la Mungano wa Tanganyika na Zanzibar na ukubwa wa kuunda Katiba Mpya hayapishani sana. Tuwe wakweli, Tume yako Jaji Waryoba ni Tume ya Katiba siyo ya Kero za Mungano.

Nimetumia "Kero za Muungano" kwa sababu inadhaniwa kuwa Mungano hauridhishi kwa sababu ya kero hizo. Na Katiba kuwa makini ni lazima itokane na Nchi isiyo na kero kama hizo. Hii ni logic tu kuwa kero za Mungano zijadiliwe kwanza halafu ndiyo iundwe Katiba inayoendana na mwafaka wa Mungano.

Kipengere cha Kwanza cha Katiba yeyote kinatamka wazi Katiba imeandikwa kwa ajili ya nani, kukidhi mahitaji yepi!

Jaji Waryoba Unapojadili Katiba bila kujua Muungano ni sawa na paka sasa kuanza kula samaki kuanzia mkiani. Paka wa namna hiyo hakuna, vipi wanadamu tunakosa uadilifu wa kujua lipi litangulie lipi!

Kama siyo noma basi mtakeni Mheshimiwa Mkuu wa Nchi awaruhusu mkamilishe kwanza maoni kuhusu Mungano na uundwe Mungano huo ili tutakapokuwa tukichangia mawazo kuhusu Katiba tuwe wazi akilini tunachangia mawazo ya kukidhi aina gani ya Utawala. Sasa hivi hakuna anayejua Zenj wataibuka na nini (Bara wamezoea kusukumwa hata na uongo).

Chonde chonde Jaji Waryoba, Katiba na Mungano haviwezi kukusanyiwa mawazo kwa pamoja, Mungano ni lazima ukamilike kwanza ndiyo tuandike Katiba yake.
 
jogoolashamba

jogoolashamba

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
348
195
Nilidhani JF ina nguvu ya kuleta mabadiliko! Kumbe ni jamvi la matajiri kufanya utani wa "Wazaramo na Wanyamwezi?!" Akina Nape na Kinana wakizomeana na akina Slaa! Haya Jaji Waryoba, Wazenj wanataka kuvunja Muungano, utawalazimisha waendelee nao ili Katiba yako iitwe ya Tanzania? Hata Spika anataka Mabunge 2 ya MUUNGANO, lakini ukimwelewa sawasawa huyu Mama inamaanisha mabunge 4, Zanzibar 2 na MUUNGANO 2. Mheshimwa sana Jaji Waryoba ungebadilisha kwanza majukumu hili la Muungano liishe kwanza! Tutakapoanza kujadili Katiba tujue akilini ni ya nchi gani yenye mfumo gani wa utawala, sasa hivi unajadili mabadiliko ya Katiba ya nchi isiyokuwepo bado, linawezekana hilo?
 
Top Bottom