Chonde chonde CHADEMA, wasameheni wabunge wenu 19 wa viti maalumu kwa maslahi ya chama na taifa

Wakati wa utawala wa dola ya Rumi, adhabu ya kusulubiwa msalabani ilikuwa ni adhabu kwa ajili ya wahalifu sugu, watu kama wauaji, majambazi na wahaini. Ilikuwa adhabu ya kudhalilisha, ya kikatili na iliyo hakikisha mateso makuu kabla ya kifo. Mtu aliye tundikwa msalabani alikuwa anaomba afe haraka ili kusitisha maumivu makali aliyokuwa anayapitia.

"Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui walitendalo", hii ilikuwa ni kauli ya Yesu Kristo mwana wa Mungu, mara baada ya kuwa ametundikwa msalabani na askari wa Rumi. Pamoja na ukatili wa hali ya juu waliokuwa wanamtendea, lakini bado aliwaombea kwa Mungu wasamehewe.

Kusamehe ni lango kuu la kuponya maumivu na mifarakano katika jamii yoyote ile, na ndio maana Yesu alifundisha umuhimu wa kusamehe tena na tena, na hata kuonesha kwa mfano pale alipowasamehe na kuwaombea msamaha wale waliomtendea uovu.

Nichukue nafasi hii kuuomba uongozi wa CHADEMA, wasameheni wabunge 19 wa viti maalum, najua 'usaliti' walioufanya umewaumiza sana ukizingatia mateso mliyoyapitia kutoka kwa mwendazake, vituko vya uchaguzi wa mwaka 2020 na hata mateso mnayoyapitia leo hii baada ya mwendazake kunyakuliwa.

Baada ya kifo cha JPM, ni vema nchi nzima tufungue ukurasa mpya ili tuweze kusongo mbele. Nawashauri CDM wapeni adhabu ya kuwavua nyadhifa za uongozi ndani ya chama lakini waacheni wawe wanachama wenu na muwape baraka zote kuwepo bungeni.

Wabunge wale 19 wamekuwa kama watoto yatima, hawawezi kutoa hoja kali bungeni kwakuwa hawana support ya chama chao, uwepo wao ni kwa fadhila za Ndugai, hivyo basi wanalazimika kuwa wapole wasimuudhi kwani anaweza kuwafukuza muda wowote kwa kigezo kuwa amepokea barua ya CDM ya kuwavua uanachama.

Kwenye kuliponya taifa hata ninyi CDM mnao wajibu wa kukiponya chama chenu. Tunaponya majereha kwa kusameheana na kushikamana zaidi, na sio kuwindana na kutesana.

Najua ndani ya CMD kuna watu wana itikadi kali (extremists), hawa wapo kwenye vyama vyote. Msikubali ushauri wao wa kuendelea kutowatambua wabunge wale, that is extreme! Si mmeshuhudia kilichoipata nchi yetu baada ya CCM kumpa nchi 'extremist' mwaka 2015?. Kaeni mbali na ma extremists.

Lakini pia, nanyi wabunge 19, kuweni wapole, tafuteni suluhu na chama chenu, ninyi ni watoto wa CDM, mmekosea lakini mtabaki kuwa watoto wa CDM. Nendeni ukonga mkamtembelee mwenyekiti wenu kule mahabusu, muanze kutafuta njia za kuyatibu majeraha ya siasa za chuki zilizopandwa na mwendazake.

Kuliponya taifa sio kazi ya SSH peke yake, kila mtu kwa nafasi yake aangalie namna ya kuboresha na kurekebisha palipo vurugwa na siasa zile za chuki.
Ushauli wako Mimi nimeupokea kwa Maslahi mapana ya Nchi lakini kabla ya Hilo kufanyika kwa nini usiwaase watawala waache kuumiza Tena watu?Mbowe kaumizwa kiuchumi na kimwili kwa kiasi kikubwa kipindi Cha JPM lakini amekuja mwingine nae anaendelea kumuumiza Tena Cha ajabu kwa kesi za kubambika,Sasa hapo Taifa litaponywaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la Mbowe wengi wamelisemea, na kwakweli SSH amepotoka mno kwenye hili.

Naamini hiyo tarehe 20, haki itatendeka.
 
Kwa kweli umewashauri vizuri CDM. Siasa zinafanyika Bungeni sasa usipokuwa na Mbunge unakosa kufanya siasa. Ni ukweli usiofichika kwamba hawa 19 wa CDM hawana hamasa tena ya kutoa hoja zenye kuichachafya serikali kwa sababu ambazo umeziweka wazi; they are not independent. Wanaweza kuondolewa na mamlaka ya Bunge kama watajimwambafy. Hawa wadada wana uwezo mkubwa wa kujenga hoja lakini siku hizi hizo hoja hatuzioni. Zi wapi hoja za Wakili Msomi Halima Mdee? Zi wapi Hoja za Cecelia Pareso? Zi wapi hoja za Ninje au Rwamlaza? Hawana uhakika wa kesho yao hivyo hawawezi kutoa hoja fikirishi!

CDM kaeni mfikirie suala hili, mnapata hasara kubwa kwa kutowasamehe hawa kuliko faida mnayoipata kwa kutowasamehe hawa watu wenu.
Nasikia walikata rufaa sijui Baraza Kuu lakini nalo halijaketi na wao wanaendelea na shughuli za Kibunge kama Wana CDM; Baraza haliketi mwaka sasa! Angalieni kama Baraza litabariki kufukuzwa kwao wakaenda Mahakamani wanaweza kuendelea kuwa Wabunge wa Mahakama hadi Bunge liishe kama ilivyotokea kwa Zitto. Kheri mkawasamehe, mkawaita mkawapa masharti na waendelee kufanya kazi za kibunge wakiwa na support ya chama chao.
Absolutely.
 
Mmeingia kwenye mtego mkubwa sana. Sameheni mfanye siasa za Kibunge. Hamuoni mmepigwa pin mikutano ya kisiasa, si vyema mkafanya siasa za Kibunge badala ya kijipiga pin huko pia?

Huko bungeni ndio wabunge wa upinzani walikuwa wanatolewa na kufungiwa kila siku. Hata Cdm wasiporuhusiwa kufanya mikutano, tayari Cdm wanafaida ya kizazi kinachojitambua. Hata wafanyiwe hila vipi, bado uhalisia utawabeba. Hilo bunge unalosema ndio hilo liko gizani, hivyo tuko vizuri maana watabana lakini wataachia.
 
Wakati wa utawala wa dola ya Rumi, adhabu ya kusulubiwa msalabani ilikuwa ni adhabu kwa ajili ya wahalifu sugu, watu kama wauaji, majambazi na wahaini. Ilikuwa adhabu ya kudhalilisha, ya kikatili na iliyo hakikisha mateso makuu kabla ya kifo. Mtu aliye tundikwa msalabani alikuwa anaomba afe haraka ili kusitisha maumivu makali aliyokuwa anayapitia.

"Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui walitendalo", hii ilikuwa ni kauli ya Yesu Kristo mwana wa Mungu, mara baada ya kuwa ametundikwa msalabani na askari wa Rumi. Pamoja na ukatili wa hali ya juu waliokuwa wanamtendea, lakini bado aliwaombea kwa Mungu wasamehewe.

Kusamehe ni lango kuu la kuponya maumivu na mifarakano katika jamii yoyote ile, na ndio maana Yesu alifundisha umuhimu wa kusamehe tena na tena, na hata kuonesha kwa mfano pale alipowasamehe na kuwaombea msamaha wale waliomtendea uovu.

Nichukue nafasi hii kuuomba uongozi wa CHADEMA, wasameheni wabunge 19 wa viti maalum, najua 'usaliti' walioufanya umewaumiza sana ukizingatia mateso mliyoyapitia kutoka kwa mwendazake, vituko vya uchaguzi wa mwaka 2020 na hata mateso mnayoyapitia leo hii baada ya mwendazake kunyakuliwa.

Baada ya kifo cha JPM, ni vema nchi nzima tufungue ukurasa mpya ili tuweze kusongo mbele. Nawashauri CDM wapeni adhabu ya kuwavua nyadhifa za uongozi ndani ya chama lakini waacheni wawe wanachama wenu na muwape baraka zote kuwepo bungeni.

Wabunge wale 19 wamekuwa kama watoto yatima, hawawezi kutoa hoja kali bungeni kwakuwa hawana support ya chama chao, uwepo wao ni kwa fadhila za Ndugai, hivyo basi wanalazimika kuwa wapole wasimuudhi kwani anaweza kuwafukuza muda wowote kwa kigezo kuwa amepokea barua ya CDM ya kuwavua uanachama.

Kwenye kuliponya taifa hata ninyi CDM mnao wajibu wa kukiponya chama chenu. Tunaponya majereha kwa kusameheana na kushikamana zaidi, na sio kuwindana na kutesana.

Najua ndani ya CMD kuna watu wana itikadi kali (extremists), hawa wapo kwenye vyama vyote. Msikubali ushauri wao wa kuendelea kutowatambua wabunge wale, that is extreme! Si mmeshuhudia kilichoipata nchi yetu baada ya CCM kumpa nchi 'extremist' mwaka 2015?. Kaeni mbali na ma extremists.

Lakini pia, nanyi wabunge 19, kuweni wapole, tafuteni suluhu na chama chenu, ninyi ni watoto wa CDM, mmekosea lakini mtabaki kuwa watoto wa CDM. Nendeni ukonga mkamtembelee mwenyekiti wenu kule mahabusu, muanze kutafuta njia za kuyatibu majeraha ya siasa za chuki zilizopandwa na mwendazake.

Kuliponya taifa sio kazi ya SSH peke yake, kila mtu kwa nafasi yake aangalie namna ya kuboresha na kurekebisha palipo vurugwa na siasa zile za chuki.
Wabunge wenyewe unaosema wasamehewe ndio hawa ambao wanawatanguliza waume zao ccm
 
Hii miaka 4 tukienda bila sauiti ya CDM pale bungeni basi wananchi wahesabu maumivu tu, wabunge wa CDM ndiyo wanaosoma kinachopelekwa pale na kuibua hoja, CDM iwatumie hawa 19 kwa maslahi ya nchi.

Ndugu zetu wa CCM wao ni wazee wa kupigapiga meza na kuunga mkono hoja.
Wenye nchi ndivyo walivyokua wameamua sasa wewe shida yako vip.hivi unajua kwenye hii dunia bado kuna binadamu kwa akili zao na usomi wao bado hawatakagi kuamini kua madaraka na maisha ni vitu vya kupita na kuna muda vinapita bila maandalizi wala kutarajia.Siasa pamoja na kwamba ni ajira kama ilivyo soka ila kukiwa na siasa za kubishana kwa hoja kunakua na faida kubwa sana kwa nchi kuliko kua na nchi yenye siasa mfu.sasa kuna watu waliamua njia ya pili badala ya kwanza ndo maana yakatokea yote hayo.Leo siasa imegeuka kua uadui badala ya ajira na kichocheo cha ajira,uwajibikaji na chachu ya maendeleo.
 
Kamanda Halima Mdee alisha sema yeye ni Chadema hadi mwisho.
na ni wabunge halali wa chadema.
Unajielewa mwenyewe kwanza?
 
Back
Top Bottom