Babe la mji
JF-Expert Member
- Dec 14, 2019
- 983
- 2,053
Ushauli wako Mimi nimeupokea kwa Maslahi mapana ya Nchi lakini kabla ya Hilo kufanyika kwa nini usiwaase watawala waache kuumiza Tena watu?Mbowe kaumizwa kiuchumi na kimwili kwa kiasi kikubwa kipindi Cha JPM lakini amekuja mwingine nae anaendelea kumuumiza Tena Cha ajabu kwa kesi za kubambika,Sasa hapo Taifa litaponywaje?Wakati wa utawala wa dola ya Rumi, adhabu ya kusulubiwa msalabani ilikuwa ni adhabu kwa ajili ya wahalifu sugu, watu kama wauaji, majambazi na wahaini. Ilikuwa adhabu ya kudhalilisha, ya kikatili na iliyo hakikisha mateso makuu kabla ya kifo. Mtu aliye tundikwa msalabani alikuwa anaomba afe haraka ili kusitisha maumivu makali aliyokuwa anayapitia.
"Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui walitendalo", hii ilikuwa ni kauli ya Yesu Kristo mwana wa Mungu, mara baada ya kuwa ametundikwa msalabani na askari wa Rumi. Pamoja na ukatili wa hali ya juu waliokuwa wanamtendea, lakini bado aliwaombea kwa Mungu wasamehewe.
Kusamehe ni lango kuu la kuponya maumivu na mifarakano katika jamii yoyote ile, na ndio maana Yesu alifundisha umuhimu wa kusamehe tena na tena, na hata kuonesha kwa mfano pale alipowasamehe na kuwaombea msamaha wale waliomtendea uovu.
Nichukue nafasi hii kuuomba uongozi wa CHADEMA, wasameheni wabunge 19 wa viti maalum, najua 'usaliti' walioufanya umewaumiza sana ukizingatia mateso mliyoyapitia kutoka kwa mwendazake, vituko vya uchaguzi wa mwaka 2020 na hata mateso mnayoyapitia leo hii baada ya mwendazake kunyakuliwa.
Baada ya kifo cha JPM, ni vema nchi nzima tufungue ukurasa mpya ili tuweze kusongo mbele. Nawashauri CDM wapeni adhabu ya kuwavua nyadhifa za uongozi ndani ya chama lakini waacheni wawe wanachama wenu na muwape baraka zote kuwepo bungeni.
Wabunge wale 19 wamekuwa kama watoto yatima, hawawezi kutoa hoja kali bungeni kwakuwa hawana support ya chama chao, uwepo wao ni kwa fadhila za Ndugai, hivyo basi wanalazimika kuwa wapole wasimuudhi kwani anaweza kuwafukuza muda wowote kwa kigezo kuwa amepokea barua ya CDM ya kuwavua uanachama.
Kwenye kuliponya taifa hata ninyi CDM mnao wajibu wa kukiponya chama chenu. Tunaponya majereha kwa kusameheana na kushikamana zaidi, na sio kuwindana na kutesana.
Najua ndani ya CMD kuna watu wana itikadi kali (extremists), hawa wapo kwenye vyama vyote. Msikubali ushauri wao wa kuendelea kutowatambua wabunge wale, that is extreme! Si mmeshuhudia kilichoipata nchi yetu baada ya CCM kumpa nchi 'extremist' mwaka 2015?. Kaeni mbali na ma extremists.
Lakini pia, nanyi wabunge 19, kuweni wapole, tafuteni suluhu na chama chenu, ninyi ni watoto wa CDM, mmekosea lakini mtabaki kuwa watoto wa CDM. Nendeni ukonga mkamtembelee mwenyekiti wenu kule mahabusu, muanze kutafuta njia za kuyatibu majeraha ya siasa za chuki zilizopandwa na mwendazake.
Kuliponya taifa sio kazi ya SSH peke yake, kila mtu kwa nafasi yake aangalie namna ya kuboresha na kurekebisha palipo vurugwa na siasa zile za chuki.
Sent using Jamii Forums mobile app