Chonde chonde CHADEMA, wasameheni wabunge wenu 19 wa viti maalumu kwa maslahi ya chama na taifa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
14,618
2,000
Wewe ni mwanachama wa Chadema?
Hakutakuwa na jambo la kucheka. CCM pamoja na utopolo wao lakini hua wanajitahidi kukiweka chama pamoja kwa kuwasamehe wanachama wake. Wale wabunge 19 wana faida zaidi wakiwa CDM kuliko kuwa nje ya chama.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
14,618
2,000
Hao wabunge wa CCM wasiosoma chochote walichaguliwa na wananchi?
Hawapaswi kushupaza shingo, wafanye diplomasia chinichini wayajenge na chama chao. Ni ngumu sana ku survive ukiwa nje ya chama. Lakini CDM ni vizuri ikiwa na sauti bungeni hata kama ni kidogo tu, kwa maslahi ya taifa.

Wabunge wa CCM hawasomi chochote kinachopelekwa pale, mwisho wa siku wanaumia watanzania.
 
Sarri

JF-Expert Member
May 25, 2018
994
1,000
Hakutakuwa na jambo la kucheka. CCM pamoja na utopolo wao lakini hua wanajitahidi kukiweka chama pamoja kwa kuwasamehe wanachama wake. Wale wabunge 19 wana faida zaidi wakiwa CDM kuliko kuwa nje ya chama.
Ok. Msameheni Membe basi
 
mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
1,613
2,000
Hao wabunge wa CCM wasiosoma chochote walichaguliwa na wananchi?
Sote tunajua kilichotokea 2020 😁😁

Lakini cha muhimu ni kuona kama taifa tunafikaje 2025 na kuhakikisha hakitokei tena. Wale 19 wanaweza kuwa na mchango muhimu kwenye kufanikisha hilo.
 
Sarri

JF-Expert Member
May 25, 2018
994
1,000
Viongozi wa chama walio 'moderate' hawawezi kudai hatua kali kiasi hicho.

What is the alternative? wabaki na ubunge wao wa fadhila na CDM inabaki bila sauti yoyote bungeni.

Hasara anaipata mtanzania na nchi kwa ujumla. Ni wajibu wa CDM kuweka maslahi ya taifa mbele kuliko ya chama.
Apate tu tabu huyo mtamzania aliyejaa unafiki, uoga, ujinga, ushamba, kutokujitambua, utayari na uthubutu. Labda utafika wakati mtanzania ajifunze kujipigania maana sasa hivi ha appreciate mchango wa wanaharakati na upinzani
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
14,618
2,000
Kama sote tunajua sasa kwa nini unataka Chadema ndio wabebe huo mzigo na sio wote waliohusika au waliokubali hilo kutokea?

Huoni litakuwa ni somo zuri kama bunge litakosa upinzani hadi 2025 ili kuthibitisha kama ni kweli wapinzani wametuchelewesha miaka yote?
Sote tunajua kilichotokea 2020

Lakini cha muhimu ni kuona kama taifa tunafikaje 2025 na kuhakikisha hakitokei tena. Wale 19 wanaweza kuwa na mchango muhimu kwenye kufanikisha hilo.
 
mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
1,613
2,000
Kama sote tunajua sasa kwa nini unataka Chadema ndio wabebe huo mzigo na sio wote waliohusika au waliokubali hilo kutokea?

Huoni litakuwa ni somo zuri kama bunge litakosa upinzani hadi 2025 ili kuthibitisha kama ni kweli wapinzani wametuchelewesha miaka yote?
Kila mtu anafanya kwa nafasi yake. Before uchaguzi 2025 sheria ya uchaguzi itarekebishwa, hao 19 wanaweza kuwa muhimu sana kwenye maboresho hayo
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
14,618
2,000
Nani kakuhakikishia kabla ya 2025 sheria za uchaguzi zitarekebishwa? Na hao C19 wasipokuwa muhimu kwenye hayo maboresho na badala yake wakahamia kabisa CCM kama Mashinji au Nassari huoni CDM itakuwa imejiharibia zaidi na kutumika tu?
Kula mtu anafanya kwa nafasi yake. Before uchaguzi 2025 sheria ta uchaguzi itarekebishwa, hao 19 wanaweza kuwa muhimu sana kwenye maboresho hayo
 
mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
1,613
2,000
Nani kakuhakikishia kabla ya 2025 sheria za uchaguzi zitarekebishwa? Na hao C19 wasipokuwa muhimu kwenye hayo maboresho na badala yake wakahamia kabisa CCM kama Mashinji au Nassari huoni CDM itakuwa imejiharibia zaidi na kutumika tu?
Mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yalitolewa na siku ya kukabidhi ripoti ya uchaguzi 2020. (CDM hawakuhudhuria), yalipokelewa na yanafanyiwa kazi.
 
REALNEGRONEVABROKE

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
3,465
2,000
Viongozi wa chama walio 'moderate' hawawezi kudai hatua kali kiasi hicho.

What is the alternative? wabaki na ubunge wao wa fadhila na CDM inabaki bila sauti yoyote bungeni.

Hasara anaipata mtanzania na nchi kwa ujumla. Ni wajibu wa CDM kuweka maslahi ya taifa mbele kuliko ya chama.
Kama vyombo vya kutunga sheria (Bunge) vimevunja SHERIA na kuikanyaga KATIBA, Chadema haitoweza kamwe kukubali iingie katika mkondo huo.

Kukubaliana na hilo la kubariki na kusamehe its will be a CURSE
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,656
2,000
Wakati wa utawala wa dola ya Rumi, adhabu ya kusulubiwa msalabani ilikuwa ni adhabu kwa ajili ya wahalifu sugu, watu kama wauaji, majambazi na wahaini. Ilikuwa adhabu ya kudhalilisha, ya kikatili na iliyo hakikisha mateso makuu kabla ya kifo. Mtu aliye tundikwa msalabani alikuwa anaomba afe haraka ili kusitisha maumivu makali aliyokuwa anayapitia.

"Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui walitendalo", hii ilikuwa ni kauli ya Yesu Kristo mwana wa Mungu, mara baada ya kuwa ametundikwa msalabani na askari wa Rumi. Pamoja na ukatili wa hali ya juu waliokuwa wanamtendea, lakini bado aliwaombea kwa Mungu wasamehewe.

Kusamehe ni lango kuu la kuponya maumivu na mifarakano katika jamii yoyote ile, na ndio maana Yesu alifundisha umuhimu wa kusamehe tena na tena, na hata kuonesha kwa mfano pale alipowasamehe na kuwaombea msamaha wale waliomtendea uovu.

Nichukue nafasi hii kuuomba uongozi wa CHADEMA, wasameheni wabunge 19 wa viti maalum, najua 'usaliti' walioufanya umewaumiza sana ukizingatia mateso mliyoyapitia kutoka kwa mwendazake, vituko vya uchaguzi wa mwaka 2020 na hata mateso mnayoyapitia leo hii baada ya mwendazake kunyakuliwa.

Baada ya kifo cha JPM, ni vema nchi nzima tufungue ukurasa mpya ili tuweze kusongo mbele. Nawashauri CDM wapeni adhabu ya kuwavua nyadhifa za uongozi ndani ya chama lakini waacheni wawe wanachama wenu na muwape baraka zote kuwepo bungeni.

Wabunge wale 19 wamekuwa kama watoto yatima, hawawezi kutoa hoja kali bungeni kwakuwa hawana support ya chama chao, uwepo wao ni kwa fadhila za Ndugai, hivyo basi wanalazimika kuwa wapole wasimuudhi kwani anaweza kuwafukuza muda wowote kwa kigezo kuwa amepokea barua ya CDM ya kuwavua uanachama.

Kwenye kuliponya taifa hata ninyi CDM mnao wajibu wa kukiponya chama chenu. Tunaponya majereha kwa kusameheana na kushikamana zaidi, na sio kuwindana na kutesana.

Najua ndani ya CMD kuna watu wana itikadi kali (extremists), hawa wapo kwenye vyama vyote. Msikubali ushauri wao wa kuendelea kutowatambua wabunge wale, that is extreme! Si mmeshuhudia kilichoipata nchi yetu baada ya CCM kumpa nchi 'extremist' mwaka 2015?. Kaeni mbali na ma extremists.

Lakini pia, nanyi wabunge 19, kuweni wapole, tafuteni suluhu na chama chenu, ninyi ni watoto wa CDM, mmekosea lakini mtabaki kuwa watoto wa CDM. Nendeni ukonga mkamtembelee mwenyekiti wenu kule mahabusu, muanze kutafuta njia za kuyatibu majeraha ya siasa za chuki zilizopandwa na mwendazake.

Kuliponya taifa sio kazi ya SSH peke yake, kila mtu kwa nafasi yake aangalie namna ya kuboresha na kurekebisha palipo vurugwa na siasa zile za chuki.
Kwa kweli umewashauri vizuri CDM. Siasa zinafanyika Bungeni sasa usipokuwa na Mbunge unakosa kufanya siasa. Ni ukweli usiofichika kwamba hawa 19 wa CDM hawana hamasa tena ya kutoa hoja zenye kuichachafya serikali kwa sababu ambazo umeziweka wazi; they are not independent. Wanaweza kuondolewa na mamlaka ya Bunge kama watajimwambafy. Hawa wadada wana uwezo mkubwa wa kujenga hoja lakini siku hizi hizo hoja hatuzioni. Zi wapi hoja za Wakili Msomi Halima Mdee? Zi wapi Hoja za Cecelia Pareso? Zi wapi hoja za Ninje au Rwamlaza? Hawana uhakika wa kesho yao hivyo hawawezi kutoa hoja fikirishi!

CDM kaeni mfikirie suala hili, mnapata hasara kubwa kwa kutowasamehe hawa kuliko faida mnayoipata kwa kutowasamehe hawa watu wenu.
Nasikia walikata rufaa sijui Baraza Kuu lakini nalo halijaketi na wao wanaendelea na shughuli za Kibunge kama Wana CDM; Baraza haliketi mwaka sasa! Angalieni kama Baraza litabariki kufukuzwa kwao wakaenda Mahakamani wanaweza kuendelea kuwa Wabunge wa Mahakama hadi Bunge liishe kama ilivyotokea kwa Zitto. Kheri mkawasamehe, mkawaita mkawapa masharti na waendelee kufanya kazi za kibunge wakiwa na support ya chama chao.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,659
2,000
Hii miaka 4 tukienda bila sauiti ya CDM pale bungeni basi wananchi wahesabu maumivu tu, wabunge wa CDM ndiyo wanaosoma kinachopelekwa pale na kuibua hoja, CDM iwatumie hawa 19 kwa maslahi ya nchi.

Ndugu zetu wa CCM wao ni wazee wa kupigapiga meza na kuunga mkono hoja.

Kwani nani kawazuia kusoma hicho kinachopelekwa na serikali hivi sasa? Msimamo wa Cdm uko wazi, ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Kama wameenda kuhalalisha uhayawani, basi wapambane na hali zao.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,659
2,000
Never ever, CDM iko miyoni mwetu bila hata kuwa na mbunge kwenye hilo bunge la majizi ya kura. Uzuri sasa hivi hata hilo bunge lenyewe tumelidharau na hatuna muda nalo. Na uwezo wa kupata kura toka kwa wananchi bila kutegemea ushawishi wowote wa mbunge aliye ndani ya bunge la kihuni, ni mkubwa kuliko maelezo.
Kwa kweli umewashauri vizuri CDM. Siasa zinafanyika Bungeni sasa usipokuwa na Mbunge unakosa kufanya siasa. Ni ukweli usiofichika kwamba hawa 19 wa CDM hawana hamasa tena ya kutoa hoja zenye kuichachafya serikali kwa sababu ambazo umeziweka wazi; they are not independent. Wanaweza kuondolewa na mamlaka ya Bunge kama watajimwambafy. Hawa wadada wana uwezo mkubwa wa kujenga hoja lakini siku hizi hizo hoja hatuzioni. Zi wapi hoja za Wakili Msomi Halima Mdee? Zi wapi Hoja za Cecelia Pareso? Zi wapi hoja za Ninje au Rwamlaza? Hawana uhakika wa kesho yao hivyo hawawezi kutoa hoja fikirishi!

CDM kaeni mfikirie suala hili, mnapata hasara kubwa kwa kutowasamehe hawa kuliko faida mnayoipata kwa kutowasamehe hawa watu wenu.
Nasikia walikata rufaa sijui Baraza Kuu lakini nalo halijaketi na wao wanaendelea na shughuli za Kibunge kama Wana CDM; Baraza haliketi mwaka sasa! Angalieni kama Baraza litabariki kufukuzwa kwao wakaenda Mahakamani wanaweza kuendelea kuwa Wabunge wa Mahakama hadi Bunge liishe kama ilivyotokea kwa Zitto. Kheri mkawasamehe, mkawaita mkawapa masharti na waendelee kufanya kazi za kibunge wakiwa na support ya chama chao.
 
cmsuma

JF-Expert Member
Apr 18, 2015
341
250
Wakati wa utawala wa dola ya Rumi, adhabu ya kusulubiwa msalabani ilikuwa ni adhabu kwa ajili ya wahalifu sugu, watu kama wauaji, majambazi na wahaini. Ilikuwa adhabu ya kudhalilisha, ya kikatili na iliyo hakikisha mateso makuu kabla ya kifo. Mtu aliye tundikwa msalabani alikuwa anaomba afe haraka ili kusitisha maumivu makali aliyokuwa anayapitia.

"Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui walitendalo", hii ilikuwa ni kauli ya Yesu Kristo mwana wa Mungu, mara baada ya kuwa ametundikwa msalabani na askari wa Rumi. Pamoja na ukatili wa hali ya juu waliokuwa wanamtendea, lakini bado aliwaombea kwa Mungu wasamehewe.

Kusamehe ni lango kuu la kuponya maumivu na mifarakano katika jamii yoyote ile, na ndio maana Yesu alifundisha umuhimu wa kusamehe tena na tena, na hata kuonesha kwa mfano pale alipowasamehe na kuwaombea msamaha wale waliomtendea uovu.

Nichukue nafasi hii kuuomba uongozi wa CHADEMA, wasameheni wabunge 19 wa viti maalum, najua 'usaliti' walioufanya umewaumiza sana ukizingatia mateso mliyoyapitia kutoka kwa mwendazake, vituko vya uchaguzi wa mwaka 2020 na hata mateso mnayoyapitia leo hii baada ya mwendazake kunyakuliwa.

Baada ya kifo cha JPM, ni vema nchi nzima tufungue ukurasa mpya ili tuweze kusongo mbele. Nawashauri CDM wapeni adhabu ya kuwavua nyadhifa za uongozi ndani ya chama lakini waacheni wawe wanachama wenu na muwape baraka zote kuwepo bungeni.

Wabunge wale 19 wamekuwa kama watoto yatima, hawawezi kutoa hoja kali bungeni kwakuwa hawana support ya chama chao, uwepo wao ni kwa fadhila za Ndugai, hivyo basi wanalazimika kuwa wapole wasimuudhi kwani anaweza kuwafukuza muda wowote kwa kigezo kuwa amepokea barua ya CDM ya kuwavua uanachama.

Kwenye kuliponya taifa hata ninyi CDM mnao wajibu wa kukiponya chama chenu. Tunaponya majereha kwa kusameheana na kushikamana zaidi, na sio kuwindana na kutesana.

Najua ndani ya CMD kuna watu wana itikadi kali (extremists), hawa wapo kwenye vyama vyote. Msikubali ushauri wao wa kuendelea kutowatambua wabunge wale, that is extreme! Si mmeshuhudia kilichoipata nchi yetu baada ya CCM kumpa nchi 'extremist' mwaka 2015?. Kaeni mbali na ma extremists.

Lakini pia, nanyi wabunge 19, kuweni wapole, tafuteni suluhu na chama chenu, ninyi ni watoto wa CDM, mmekosea lakini mtabaki kuwa watoto wa CDM. Nendeni ukonga mkamtembelee mwenyekiti wenu kule mahabusu, muanze kutafuta njia za kuyatibu majeraha ya siasa za chuki zilizopandwa na mwendazake.

Kuliponya taifa sio kazi ya SSH peke yake, kila mtu kwa nafasi yake aangalie namna ya kuboresha na kurekebisha palipo vurugwa na siasa zile za chuki.
Kama wahusika hawajawahi kuomba msamaha wao wataanzia wapi?
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
9,442

Kweli mkuu, tunaoishi kwenye Injili ya Kristo tumekuelewa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom