Chonde Chonde CDM isithubutu kuchukua mawaziri watakaojivua magamba

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Wakuu kwa jinsi upepo wa kisiasa unavyovuma ni wazi hao mawaziri wanaosemwa watajiuzuru.

Inaweza ikatokea baada ya kujiuzuru wakavaa taswira ya ukombozi au upambanaji maana watakuwa wanajua mengi na kuleta ghiba kuwa endapo mambo yatawachachia watajiengua na kuzama CDM kwani tayari watakuwa wamevaa ngozi ya upambanaji wa kinafiki.

Chonde Chonde viongozi wa CDM kuanzia kamanda Mbowe na uongozi mzima wa CDM msikubali kupokea makapi toka CCM ambayo baadae itakuwa chanzo cha migogoro.

Uzoefu unaonyesha watu waliowahi kushika madaraka makubwa kama uwaziri wakihamia vyama fulani bado hujikweza na kujiona wana nguvu kuliko chama. Ni bora likaepukwa hilo ili kuepusha kutumia muda mwingi kusuluhisha migogoro badala ya kuendele M4C.

I stand to be corrected,

Nawasilisha.
 
Nakuunga mkono kwa % zote,,icje ikaonekana CDM ndio jalala la vilaza...waanzishe C.C.M C,, maana C.C.M B, tayari ipo.

Usidhani kama watatoka watatoka kwa mioyo miyeupe, wengi watatoka na mavinyongo na muda si mrefu wataanza kubwabwaja na kutufurahisha sisi ambao tunapenda anguko la CCM.

Wakiona huko wanabanwa au kiswahili cha mtaa wamenyea kambi watajitia kubisha hodi kambi ya ukombozi ili waje wanajisi mchakato wa ukombozi.

Katu tusilikubali hilo, tuwaache wapigane, watoane mangeo hadi wazikane sisi tuwe mashahidi tu.
 
Open Group mpya imefunguliwa facebook kwa jina la Ukombozi Tanzania. Unaruhusiwa kujoin pamoja na kuinvite watu mbalimbali kwenye group. Aim ni kuwa na kila mtanzania anayetumia mtandao wa internet awe kwenye hili group tayari kupashana habari pamoja na Kuikomboa nchi yetu. Ndio kwanza tumeanza kuchukua hatua sio kila siku maneno.. Jiunge na hiyo group sasa na unganisha na wenzako.


Ukombozi Tanzania Admin
 
Open Group mpya imefunguliwa facebook kwa jina la Ukombozi Tanzania. Unaruhusiwa kujoin pamoja na kuinvite watu mbalimbali kwenye group. Aim ni kuwa na kila mtanzania anayetumia mtandao wa internet awe kwenye hili group tayari kupashana habari pamoja na Kuikomboa nchi yetu. Ndio kwanza tumeanza kuchukua hatua sio kila siku maneno.. Jiunge na hiyo group sasa na unganisha na wenzako.


Ukombozi Tanzania Admin

Ni wazo zuri mkuu ngoja tulifanyie utafiti kisha tulitolee maamuzi. Katika hilo naomba sana kuwajuza msiamini kila mtu, wengine ni manyokaa watakuja kuwauza mpewe kesi za kihaini.

Si unajua mtu akitaka kufa kila kitu anaona nuksi kwake.
 
Unataka kutuambia Zitto ahangaike kuwafanya wajiuzulu halafu the next day awapokee kwenye chama chake basi atakuwa hana akili nzuri.
 
Unataka kutuambia Zitto ahangaike kuwafanya wajiuzulu halafu the next day awapokee kwenye chama chake basi atakuwa hana akili nzuri.

Feedback inafikiri watafanya haraka hivyo? Wataanza kwanza kuharibu huko waliko kwa kujivika ngozi ya upambanaji halafu ndiyo watashift baada ya kuona hawatakiwi na huko.
 
Wakuu
kwa jinsi upepo wa
kisiasa unavyovuma ni wazi hao mawaziri wanaosemwa watajiuzuru.

Inaweza ikatokea baada ya kujiuzuru wakavaa taswira ya ukombozi au
upambanaji maana watakuwa wanajua mengi na kuleta ghiba kuwa endapo
mambo yatawachachia watajiengua na kuzama CDM kwani tayari watakuwa
wamevaa ngozi ya upambanaji wa kinafiki.

Chonde Chonde viongozi wa CDM kuanzia kamanda Mbowe na uongozi mzima wa
CDM msikubali kupokea makapi toka CCM ambayo baadae itakuwa chanzo cha
migogoro.

Uzoefu unaonyesha watu waliowahi kushika madaraka makubwa kama uwaziri
wakihamia vyama fulani bado hujikweza na kujiona wana nguvu kuliko
chama. Ni bora likaepukwa hilo ili kuepusha kutumia muda mwingi
kusuluhisha migogoro badala ya kuendele M4C.

I stand to be corrected,

Nawasilisha.

Lusambo,
U sound like Jenesta Mhagama who wants people to believe that the falls
of big shorts is a credible work done by ccm MPs! MWENYE AKILI YEYOTE
HAWEZI KUHANGAIKA KUWATEGA PANYA WAHARIBIFU ILI AWAUE LKN BAADA YA MTEGO KUWADAKA
ANAWAHAMISHIA STOO YA NAFANA NA KUWAACHA HURU! CDM are not that stupid
 
ccm c ipo sahivi umeshau chama kilichoanzishwa juzi hapa ambacho kinatafuta wanachama ,basi watakimbilia huko ,hatuwataki kabisa waje cdm maana sisi tnatafuta kunyakua dola
 
naunga mkono hoja

ingawaje naona kama mbowe amegeuka mchagga halisi, ananunua maskrepa yote tu hata yenye vibomu
 
Unfortunately not true!! Inategemea sana na namna ambavyo CHADEMA watakavyoamua kuwatumia. Iwapo watakuja na actionable intelligence ambayo haitaleta madhara kwa CDM, ni vizuri wawakaribishe kama wanachama wa kawaida bila kuwaweka katika positions zozote zinazowafanya waonekane kama image ya CDM.
 
Hivi ccm itafika kweli 2015? I have very serious doubts about this..
 
nafahamu watafanya kama mh lowasa, watajiuzuru uwaziri lakini ubunge no! ccm wanaufahamu mziki wa kurudia uchaguzi nauhakika bado hawajasahau arumeru, kitakachofanyika ni makubaliano maarumu yakuwa achia uwaziri lakini baki na ubunge chama kitakulinda na hizo tuhuma zako.
 
Wale ni wezi,waongo na wahujumu uchumi! Nadhani ni muda muafaka wakamatwe kwa hayo makosa kwani ushahidi upo wazi. Nitashangaa kama watawaacha waendelee kujinafasi ndani ya bunge huku waliotoa hoja kung'olewa wakikutana nao laivu. Ni hatari kwa usalama wa wapambanaji, wabunge wengine pamoja na viongozi wengine kuwaacha wakichekelea mitaani na ndani ya bunge.
 
Back
Top Bottom