TUME ya Taifa ya Uchagzu (Nec) imetangaza kuwa uchaguzi wa wabunge katika majimbo saba ambayo haukufanyika Oktoba 31 mwaka huu, utafanyika Jumapili ijayo.
Kwa mujibui wa taarifa iliyolewa na Nec kwa vyombo vyahabari jana, uchaguzi huo unafanyika katika majimbo ambayo hayakufanyakia kwa sababu mbalimbali ukiwemo upungufu wa vifaa vya kupigia kura.
Mkurugenzi wa Nec, Rajabu Kiravu aliyataja majimbo yatakayofanya uchaguzi huo kuwa ni Mpanda Mjini, Mpanda vijijini, Nkenge ya Tanzania bara na Mwanakwerekwe, Mtoni, Magogoni na Wete kutoka Zanzibar.
"Watakaohusika katika kupiga kura ni wakazi wa majimbo hayo waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura," alieleza Kiravu.
Kiravu alifahamisha kuwa upigaji kura katika majimbo hayo utafanyika katika vituo vya kupigia kura vilivyokuwa vimepangwa kutumika wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 30, mwaka huu.
Hata hivyo, Kiravu alifafanua kuwa watu ambao namba za kadi zao za kupigia kura zitatofautiana na namba zilizomo kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, hawataruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo.
"Vituo vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa 11:00 jioni kama ilivyofanyika kwenye uchaguzi uliopita," imeeleza taaarifa hiyo na kuongeza kuwa
hakutakuwa na kampeni kabla ya uchaguzi huo kwa kuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu kilishamalizika.