Chonde Chadema nendeni Mpanda mkamlete bungeni MM/Mkiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chonde Chadema nendeni Mpanda mkamlete bungeni MM/Mkiti

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Nov 11, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,919
  Likes Received: 12,106
  Trophy Points: 280
  TUME ya Taifa ya Uchagzu (Nec) imetangaza kuwa uchaguzi wa wabunge katika majimbo saba ambayo haukufanyika Oktoba 31 mwaka huu, utafanyika Jumapili ijayo.
  Kwa mujibui wa taarifa iliyolewa na Nec kwa vyombo vyahabari jana, uchaguzi huo unafanyika katika majimbo ambayo hayakufanyakia kwa sababu mbalimbali ukiwemo upungufu wa vifaa vya kupigia kura.

  Mkurugenzi wa Nec, Rajabu Kiravu aliyataja majimbo yatakayofanya uchaguzi huo kuwa ni Mpanda Mjini, Mpanda vijijini, Nkenge ya Tanzania bara na Mwanakwerekwe, Mtoni, Magogoni na Wete kutoka Zanzibar.

  "Watakaohusika katika kupiga kura ni wakazi wa majimbo hayo waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura," alieleza Kiravu.
  Kiravu alifahamisha kuwa upigaji kura katika majimbo hayo utafanyika katika vituo vya kupigia kura vilivyokuwa vimepangwa kutumika wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 30, mwaka huu.

  Hata hivyo, Kiravu alifafanua kuwa watu ambao namba za kadi zao za kupigia kura zitatofautiana na namba zilizomo kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, hawataruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo.

  "Vituo vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa 11:00 jioni kama ilivyofanyika kwenye uchaguzi uliopita," imeeleza taaarifa hiyo na kuongeza kuwa
  hakutakuwa na kampeni kabla ya uchaguzi huo kwa kuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu kilishamalizika.
   
 2. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tunamtaka Mzee Arfi bungeni.
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Slaa, Sugu, Msigwa,Mdee, Mnyika wakapige kambi Mpanda waje wote (Mpanda Mjini na Vijijini), Mwenyekiti, Zito, Wabunge wote wa kanda ya ziwa wakalilete jimbo la Nkenge. Uchaguzi wa Spika ni lini?
   
 4. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na kama hizo namba ziantofautiana, ni wajibu wa mwananchi mwenye kadi au NEC? Hapa kuna harufu ya mwendelezo wa uchakachuaji kwa njia ya kuwazuia TENA baadhi ya watu wasipige kura.
   
 5. Marunda

  Marunda Senior Member

  #5
  Nov 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tunayahitaji sana Majimbo haya at least kuwa more strong bungeni. Hata kwenda tu bila kufanya kampeni yoyote pale mpanda mjini SLAA ANAWEZAKUSHAWISHI WAPIGA KURA KUMPIGIA MGOMBEA WA CHADEMA KURA
   
 6. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashauri baada ya kikao cha kamati kuu basi Slaa eelekee huko mpanda, wakati hawa wengine wakilazimika kusubiri bungeni ili kuapishwa, yeye akapambane huko. hivi viti vikipatikana vitaongeza na idadi ya wabunge wa viti maalum. na angepatikana kamanda mwingine kama Shibuda au Zitto akapige tafu Nkenge na ukichukulia mpango wa hawa CCM kutaka kubariki ufisadi kwa kuweka spika mdhaifu utaipa CHADEMA more credit...
   
 7. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni muhimu!!
   
 8. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Muda wa kampeni si umeshaisha? au kampeni zinaruhusiwa kuendelea btn NOW and Sunday?
   
Loading...