Chombo cha Voyager 2 na miaka 46 ya safari yake

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Imewashangaza sana wanasayansi wa Nasa kwa kuweza kuona ufanyaji wa kazi wa vyombo mbalimbali vya ndani ya chombo cha voyager 2 mara baada ya mara ya mwisho kutumia katika miaka 34 iliyopita.

Chombo cha voyager 2 kiliweza kufanya manuever ya kukifanya chombo hicho kiweze kukaa katika njia yake huku kikiwa kinaendelea kuelekeza antena zake huku duniani ili isijekutokea kukawa na kukatika katika kwa mawasiliano wakati wa chombo hichi kikiwa kinaelekea mbali zaidi na mfumo wa jua letu.

Ni ajabu baada ya miaka 34 kumefanyika majaribio mengine ya kuwasha engine ili kuangalia kama zitaweza kusukuma tena ila majibu yalikuwa mazuri sana sababu engine zote zilisukuma hii inaonyesha kuwa mifumo yote ilikuwa inafanya kazi sawa sawa kama awali.

Chombo cha voyager 2 kilirushwa siku chache baada ya chombo cha voyger 1 kurushwa kwa lengo kubwa sana la kwenda huko anga za mbali kufanya aina mbalimbali za uchunguzi kuhusu mfumo wa jua na sayari zake zote za mbali kama vile saturn jupiter neptune uranius.

Cha ajabu vyombo vyote hivyo viliweza kwenda mbali zaidi ya matarajio kwa kuweza kutoka katika hadi nje ya mfumo wetu wa jua na kuingia huko interstellar space yaani huko kwenye mifumo mengine ya nyota.

Kwa kutumia mfumo wa deepe space network bado tunaweza kupata signal za vyombo hivyo vyote huko anga za mbali.

Vyombo vyote hivyo vilitengenezwa na chuo cha tekinolojia cha california ambacho kipo chini ya shirika la nasa huku ndipo mission zote za robot na vyombo vinavyoenda anga za mbali zinakoratibiwa na kutengenezwa hapa nazungumzia vyombo visivyohusisha wanadamu yaani robotic.

Voyeger 2 ndio jicho letu pekee lililoweza kufika mbali zaidi yaani nje kabisa ya mfumo wetu wa nyota Jua.

Chombo hicho bado kinatembea kwa kasi ya 55,000 kph au 15 kilomita kwa sekunde kuelekea huko kusiko julikana,

Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili
FB_IMG_1674845236567.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom