Chombo cha NASA chafanikiwa kutua Sayari ya Mirihi (Mars), kitakusanya na kurudisha sampuli za mawe duniani

Wamesikika wakisema "ushuuu!!!" maana ingetua pembeni wangebanwa
 
Naanza kuunganisha doti kuwa huwenda Ilipokuwa iikisemwa kuwa toka nchi uipendayo na uende nchi nyingine huwemda watu enzi hizo waliweza kitoka sayari moja kwenda nyingine.

Ama inaposemwa kuwa akatoka na kwenda mbali na uso wa bwana huwenda ilikua kutoka sayari moja kwenda nyingine.

Au kwa ujumla space yoote au mjumuiko wa sayari zote ndio dunia na yayari mojamoja ndio nchi ama miji. Who knows hapo mars ndio miji ya sodoma na gomorah?
We jamaa umenifikirisha
 
China walituma chombo chao chang'e mwezini na kimerudi na sample kutoka mwezini December 16 2020.

Pia nasa wana Artemis moon program ambapo 2024 watapeleka mwanamke wa kwanza mwezini na mwanaume kwa mara nyingine.
No one has ever landed on the moon


Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Shirika la Marekani la Utafiti wa Anga (NASA) limesema ndege yake ya utafiti imefanikiwa kutua katika Sayari ya Mirihi (Mars) imefanikiwa kutua salama na kushusha kifaa cha utafiti kilichopewa jina Perseverance katika sayari hiyo nyekundu.

View attachment 1705902

Hii ni hatua mpya katika utafiti wa anga za juu, ambapo kifaa hicho chenye ukubwa unaolingana na gari dogo kitakusanya sampuli za mawe kutoka katika sayari hiyo na kuyaleta duniani kwa mara ya kwanza katika historia ya mwanadamu.

Lengo la kutuma kifaa hicho cha utafiti ni kuangalia uwezekano wa kuwapo uhai katika sayari hiyo ya nne katika Sayari za Mfumo wa Jua, na kitapeleleza kwa muda wa miaka miwili.

Kwa sasa, wahandisi na wafanyakazi wa NASA wanashusha pumzi ya ahueni baada ya chombo hicho kufanikiwa kutua, kwani ni takriban nusu tu ya vyombo vya anga vilivyowahi kutumwa katika Sayari Nyekundu vimefanikiwa kutua salama!

Matokeo ya utafiti utakaofanywa na chombo Perseverance utamsogeza mwanadamu karibu zaidi na lengo la siku moja kuishi katika Sayari ya Mirihi. Licha ya kutumia gharama kubwa ya zaidi ya dola bilioni 3 (Sawa na zaidi ya Tsh. trilioni 6 na bilioni 900), NASA ina matumaini ya kupata matokeo yenye kulingana au zaidi ya thamani hiyo ya fedha kutokana na utafiti huo.

Chombo hicho kimetua karibu na eneo lililopewa jina Kreta ya Jezero, bonde lenye upana wa kilomita 12 lililopo karibu na Ikweta ya sayari hiyo. Eneo hilo linaaminika kuwahi kuwa na mto uliotengeneza delta zaidi ya miaka bilioni 3.6 iliyopita, hivyo kufanya uwezekano wa kuwapo viumbe hai au masalia ya viumbe hai kuwa mkubwa.


Marekani inapewa changamoto na mataifa ya China na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao pia wametuma vyombo vyao vya anga katika Sayari hiyo Nyekundu kupeleleza uwezekano wa uwepo wa uhai. Wingi wa shughuli za anga katika sayari hiyo kunaifanya kuwa kitovu cha utafiti wa anga za juu kwa takriban kipindi cha karne ijayo.
Hawa ndio wanasayansi, si hawa wa huku wameamua kupambana na waganga wa tiba asili katika kutafuta mizizi , magome au majani ya kutibu covid.
 
Wewe ndo unajibana.
Katika hizo sayari Tisa na dunia ikiwemo.ni moja Tu inayosapoti maisha.
Na hata ukiangalia mizunguko ya hizo sayari kulizunguka JUA.ni wazi dunia ndo ina afaa kuishi
Eti sayari 9,utafiti umeonesha ziko 11 hizo tisa wewe umezijuaje bila wazungu kukuambia? Utafiti unaonesha huenda kuna zaidi ko kadiri Sayansi inavyokua mambo mengi yatazidi kufahamika
 
Kuna vitu mi nashindwa kuviamini hasa inapotokea nguvu kubwa yakutaka niamini... sasa hiyo picha kaipiga nani aliyekua katangulia huko chombo kinapotua?
Poleni hata geografia ya la saba hamkusoma au? Hivi zile pcha za mpangilio wa sayari 9 alipiga nani?

Ndio maana kuna darubini inapiga picha na watu wanafanya analysis ya picha.Madam chombo kimefika subiri Hali halisi ya majibu
 
Kwa Sisi wa huku duniani ndo tunaenda kuanzisha maisha mapya huko mars?
Tutaenda na ndege za kawaida au Kwa hizo hizo rocket?
Hapa tuu duniani watu wanazaliwa bila kukutana kimwili mbegu zinaunganuishwa anatokea binadamu sasa hilo la kwenda kuwazalisha huko huoni ni rahisi zaidi?

Utafikaje kwani huoni zamani wakati wanaanza utafiti it used to take years kufika Mars sasa hivi ni miezi ko tech unakua na itaboreshwa zaidi.

Rocket za vita zinatumia chini ya saa moja ku hit target ya bara moja Hadi jingine ndio watashindwa vipi ku improve speed hapo?
 
Hawa mabeberu wanatuchukia na sisi wanataka kutuona kwa juu maendeleo yetu ya SGR tusikubali kabisa hawa jamaa sasa too much.
eti mzungu mwenye interchange na sgr toka miaka ya 60/70s aje kukuonea wivu ,aisee nahisi wanaweza kuwa wanatumia maelezo yetu kama vichekesho na kebehi kwa waafrika.

Ni aibu kweli kweli,wazungu walifanya maendeleo makubwa wakaysharibu kwa vita mara 2,wamefanya tena lakini bado Afrika hatujafikia hata yale ya enzi za uvumbuzi wa machine
 
Sisi tutabakia kuwa wa maonyesho tu ushahidi ni hii peofile picture BBC
Hata wakitufanya laboratory apparatus ni sawa maana we are doing nothing zaidi ya kutiana tuu
 
Watapeleka na oxygen?.
Hicho ndo kitu ambacho najiuliza.
kwenda wanaweza wakaenda swali wataishi vipi bila oxygen?
Cha kwanza wameenda ,hayo mengine ubongo utazidi kuchapa kazi,hata robots wanaweza kuwekwa huko au anything different

Majuzi niliona bbc wanataka waanze kuunganisha genes za binadamu na wanyama wengine Ili kitokee kiumbe mpya
 
Kwanini inakua rahis mars na mwezini inakua ngumu kufika Wala kutuma vifaa??

Mwenye kujua anijibu

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
Sidhani kama ni ngumu,mwezi umefanyiwa Sana utafiti na ni subset ya dunia na ikumbukwe kila planets ina mwezi au several moons

Pengine pameonekana hapana tija zaidi ngoja waende kwenye planets wanakoamini huenda kuna maisha mengine
 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom