Chombo cha dola kuwa ombaomba ndani ya miaka hamsini tumevuka malengo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chombo cha dola kuwa ombaomba ndani ya miaka hamsini tumevuka malengo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, May 26, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Maazimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania yametuacha na changamoto nyingi ambazo tusipokuwa makini inabidi Amiri jeshi mkuu wa Majeshi yetu ya ulinzi na usalama na mkuu wa nchi aitishe bunge na kutangaza hali ya hatari juu ya janga lililoikumba nchi yetu kupelekea nchi kuwa omba omba.

  Hali inatisha kutokana na serikali yetu kushindwa kuwajibika kuendesha nchi,au kwa makusudi ama mkakati mathubuti kuichafua serikali unaofanywa na watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia vyombo hivi.Bajeti za wizara zinapangwa kila mwaka lakini hazitoshelezi mahitaji halisi ya wizara husika,ilihali serikali kupitia bunge ikiidhinishiwa matumizi katika kipindi cha bajeti.Hali kama hii inasababisha huduma muhimu kushindwa kutekelezeka kwa wakati.

  Kitendo cha jeshi letu la polisi kuwa omba omba kwa matajiri mafuta ya magari yake ni aibu kubwa si kwa jeshi tu bali na taifa letu kwa ujumla.Ufinyu huu wa bajeti umepelekea jeshi hilikudhalilika huku wizara husika ikitenga pesa za uendesha katika kila idara ya serikali,serikali haijawa masikini kiasi hicho kushindwa kuhudumia idara zake.Tunaitaka serikali itoe ufafanuzi juu ya jambo hili ambalo linaivunja heshima ya chombo hiki cha dola.

  Hali kama hii ikizidi kukithiri athari yake ni kujenga matabaka miongoni mwetu na kuwafanya matajiri kutumia udhaifu wa jeshi hili kutekeleza matakwa yao kinyume na sheria.Aibu hii inatakiwa ipigiwe kelele kwa nguvu zote ili kulinda hadhi ya jeshi letu kama chombo cha dola.Hatupendi hali hii izidi kushamiri na kuvuka mipaka ya nchi yetu,si mafuta pekee yake,hata karatasi za kuandikia charge za kesi mbali mbali nazo ni shida,kiasi cha wananchi kuambiwa walete karatasi ili ku file kesi hizo hizo.Hili naweza kusema ni janga la kitaifa kwa serikali kushindwa kuvisimamia vyombo vyake vya dola na kutoa bajeti inayojitosheleza.

  Mungu tubariki Watanzania,tuwe wakweli na kumulika kila aina ya uozo unafanyika nchini mwetu kwa minajili ya kuimaliza nchi yetu na kupoteza heshima kama taifa kwa kushindwa kusimamia hata kile kilicho chini ya uwezo wetu.


  Nitasema kweli daima,fitina kwangu mwiko
   
Loading...