Chombo cha crew dragon kitasafiri kwa jumla ya masaa 20 hadi kufika katika kituo cha anga za mbali

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Mara baada ya kufika anga za mbali huko chombo cha crew dragon kitatumia jumla ya masaa 20 kuweza kufika katika kituo cha anga za mbali na kuungana nacho

Chombo cha crew dragon kitazunguka dunia yetu kwa mara nyingi zaidi huku kikiwa kinakwenda mbali taratibu mpaka pale kitakapokuwa kimefika umbali wa km 420 kutokea usawa wa bahari umbali ambao kituo cha anga za mbali ndipo kinapopatikana hapo

Nazungumzia umbali wa kutoka hapa duniani kuelekea juu yaani piga mahesabu hayo sasa km 420 ndio umbali ambako kituo chetu cha anga kinapopatikana ni sawa na umbali kutoka dar hadi dodoma kama sikosei

Unajua kwanini umbali ni mdogo lakini chombo hutumia muda mrefu kwasababu safari nyingi za anga mara baada ya kufika katika orbit vyombo huanza kuzung
uka dunia yaani ili chombo kisiweze kutumia nishati kubwa basi inabidi kitembee neutral ( free kitonga ) halafu mara moja moja chombo huwasha mashine zake ili kwenda mbali then huzima na kuanza kutembea na kasi ile ile hadi enei fulani mpaka watakapofika katika safari yao

Marekani huwaga wanaamuaga kwenda taratibu ili kuweza kuwapa wanaanga wao muda mzuri wa kutazama anga na kuweza kupiga picha nyingi sana katika muda wote wawapo safarini

Chombo kitasafiri muda wa saa 9 mchna kwa masaa ya afrika mashariki na unaweza kutazama kwenye link hapo chini



#Gerald #Tanzaniascienceyetu #Elimuyangazambali
FB_IMG_1664973237774.jpg
 
Back
Top Bottom