Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,425
MTUNZI: IRENE MWAMFUPE NDAUKA
SEHEMU YA 01
Jumapili moja baada ya kula chakula cha usiku, baba mzazi wa kijana Nelson ambaye wengi walipenda kukatisha jina lake na kumwita Nelly, Mzee Reli ya Uhuru akiwa ameketi sebuleni na kijana wake huyo aliyehitimu kidato cha nne, alimweleza kwamba kwa wakati ule hakuwa na fedha za kuweza kumuendeleza kielimu hivyo ajichanganye mjini kujitafutia maisha.
Wakati mzee huyo aliyepewa jina la utani la Reli ya Uhuru kufuatia kuwa mmoja wa watu waliojenga reli hiyo, akimweleza hivyo, mkewe alikuwa akimsikiliza ambapo alimuunga mkono mumewe kwani hali yao kiuchumi aliielewa vizuri.
“Nelly, ni kweli kabisa kwa hivi sasa baba yako hana fedha na unaona jinsi familia yetu ilivyo kubwa na wote tunamtegemea yeye, mimi nakubaliana na ushauri wake wa wewe kujichanganya mjini kufanya vibarua ambavyo vitakuwezesha kupata riziki yako na yetu,” mama huyo alimwambia kijana wake.
Nelly kijana ambaye tangu udogo wake ni handsome boy kiasi cha kuwavutia wasichana wengi wakiwemo watu wazima, aliposikia kauli hiyo ya wazazi wake aliinamisha kichwa na kuanza kufikiria hatima ya maisha yake ingekuwaje.
“Hivi baba, huwezi kuuza lile shamba la Kimanzichana ili fedha zitakazopatikana niweze kuendelea na masomo nitimize ndoto zangu za kuwa mhasibu?” Nelly alimwuliza baba yake.
Baba yake alimfahamisha kwamba baada ya mambo yake kuanza kumwendea kombo, aliuza nusu ya shamba hilo na nusu iliyobaki asingeweza kuiuza kwani alipanga ije iwasaidie wadogo zake ambao walikuwa wadogo.
Kwa kuwa Nelly alikuwa akielewa ukubwa wa familia yao na jinsi mzazi wake alivyokuwa akihangaika kuitunza, akawa hana jinsi zaidi ya kuingia mitaani kusaka kibarua chochote ambacho kingemuwezesha kupata fedha.
“Oke baba na mama, kwa kuwa naielewa hali halisi ya maisha yetu hapa nyumbani, nitazungumza na fundi Yassin ili niongozane naye kwenye shughuli zake za ujenzi,” Nelly aliwaambia wazazi wake.
Alipotoa kauli hiyo, baba yake licha ya kujiuliza moyoni kama kweli Nelly aliyemlea kimayai angeweza kufanya kazi ya uwashi lakini hakutaka kumuonesha wasiwasi wake, akamwambia sawa.
Baada ya mazungumzo hayo, Nelly aliwaaga wazazi wake na kwenda kwenye chumba alichokuwa akilala na wadogo zake wawili kilichokuwa uani, akawa anatafakari ugumu wa maisha uliokuwa ukiwakabili.
Chumbani kwa wazazi wake, baba na mama yake walimjadili sana kijana wao kama angeweza kufanya kazi ya ujenzi lakini baadaye walikubaliana wasubiri kuona matokeo.
Alfajiri na mapema Nelly alikwenda kumgongea fundi Yassin ambaye alikuwa fundi washi aliyekuwa akisifika sana kwa umahiri wake wa kujenga nyumba maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar.
“Niambie Nelly, naona leo umenivamia alfajiri yote hii, umekwama nini?” fundi Yassin aliyekuwa akimpa fedha Nelly siku moja moja alipokwama alimwuliza.
“Ukiacha kukwama, leo nataka tuongozane huko site unakokwenda kujenga japo nikakusaidie kazi yoyote maana mtoto wa kiume kumtegemea baba kila kitu haipendezi,” Nelly alimwambia fundi Yassin.
“Yaani Nelly na huo usharobaro wako unataka kwenda kufanya kazi ya kukoroga zege au kuranda mbao, utaweza kweli?” fundi Yassin alimwuliza.