Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
Mabalozi wa amani ambao mwezi uliopita waliunda umoja ujulikanao kama Amani Forum wamewakosoa wanaharakati wanaoandaa maandamano dhidi ya Bunge kwa kusema kitendo hicho ni choko choko zinazoashiria uvunjifu wa amani unaofanywa na watu wenye maslahi binafsi.
Mabalozi wa Amani Forum ambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Dk Walid Kabourou, Augustine Mrema, Gilbert Ngua, Mariam Tawfik na Risasi Mwaulanga(katibu) walisema tamko hilo la wanaharakati ni miongoni mwa viashiria ambavyo vimeanza kuonekana yakiwemo maneno ya chini chini ya kuvunja amani ya nchi.
Wamesema katika kuhakikisha kuwa umma unaelewa ukweli wa mambo juu ya suala zima la kulinda amani, Amani Forum kesho itafanya mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke, mwezi ujao AF itafanya mikutano mingine miwili Dar es Salaam katika maeneo ya Manzese na Buguruni kabla ya kuhamia kwenye mikoa waliyoitaja kwamba ni yenye utata waliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mara, Arusha, Mwanza, Mbeya na ya Kusini.
Mrema alisema, "unaposema ni maandamano nchi nzima, ni dalili kwamba yanapinga serikali nzima, Hizi choko choko ni za nini?, alihoji Mrema na kukumbushia kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere huku akisisitiza kwamba watu wanaohamasisha chuki lazima umoja wao ukemee vinginevyo nchi itasambaratika.
Mrema alisema maeneo mengine ambayo mikutano yao itayazungumzia, ni juu ya maneno ya chini chini kuhusu masuala ya dini ambayo yanaashiria kuleta mgawanyiko. Alisema suala la Mahakama ya Kadhi na mchakato wa Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ni miongoni mwa mambo ambayo watayatolea ufafanuzi zaidi ili kuondoa hali ya kukinzana miongoni mwa wakristo, waislamu na Serikali.
Alisema kitendo cha kumwondoa Rais kabla ya muda wake ambao Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijiwekea, kinaweza kikaleta vita. Rais hachezewi. Kikwete mkimtishia nyau mnadhani hawezi kukitosa CCM? Katiba inampa madaraka makubwa, akitangaza.